Ni muda sasa wa kuichukua Jerusalem

Ni muda sasa wa kuichukua Jerusalem

Antonio Conte

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2017
Posts
1,089
Reaction score
1,748
Sahivi mataifa karibu yote ikiwemo Tanzania macho yao yapo Yerusalemu hasa baada ya tamko la Trump kiongozi wa taifa kubwa duniani kuutambua mji wa Yerusalme kama mji mkuu wa Israeli, kwanini kunatahuruki hiyo? Fatana nami kwa uchambuzi wa kina dhidi ya mji huo wa kale.

Yerusalem ni mji mkongwe na wa kihistoria katika miji ya kimataifa. Hii dunia ina miji miwili ambayo ndio chimbuko la ustarabu, moja ni Babeli uliojengwa na Nimrod (Mwanzo 10:9), na wa pili ni mji wa Salemu au Yerusalem ambao inaaminika mhasisi wake alikuwa Melkizedeki, na ndivyo Wayahudi wanavyoamini, maana Melikizeki anatambulishwa katika kitabu cha Mwanzo 14:18 kama mfalme wa Salem aliyekuja kumlaki Ibrahimu baada ya kutoka vitani, na Salemu katika Zaburi 76:2 unatambulishwa kama mji wa Yerusalem. Na baade mji huo ulikaliwa na Wayebusi-wakaanani(Yoshua 15:63) chini ya mfalme Adonisedeki, Adonisedeki ni jina lingine la Melkizedeki kulingana na tamaduni za kiyahudi[Melk ni mfalme, na Adoni ni bwana au mfalme], wafalme wa Kiyebus walijiita kwa jina la mwanzilishi wa mji huo ambao baadae ulitekwa na Joshua na akawapa wana wa Yuda (Yoshua 15:8) ila hawakuwatoa Wayebusi mpaka zama za mfalme Daudi ndipo aliwafukuza kabisa na kuufanya Yerusalemu kuwa makao makuu ya Israeli (2 Samweli 5:6-9) yaliyodumu mpaka walivyopokonywa na Warumi mnamo mwaka 70 BK. Biblia inasema ‘’Basi ikawa hapo ADONI-SEDEKI, mfalme wa YERUSALEMU, aliposikia jinsi Yoshua alivyoushika mji wa Ai na kuuharibu kabisa…….’’ Mpaka hapo tumeona kwamba Yerusalem ni mji wa kitambo sana. Nimrod alikuwa kuhani wa Ibilisi, na Melkizedeki alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana, kwaiyo hiyo miji miwili ni kama visima ambavyo vinatoa maji ya ustarabu kuelekea mataifa yote. Ebu tuangalie mji wa Babeli na Yerusalem katika nyanja hizo mbili za ustarabu:-

BABELI: Neno Babeli lina maana ya lango la miungu, yaani Bab-lango, el miungu, na hapo ndipo Mungu alichafua lugha sababu ya uasi dhidi yake, na tangu hapo Babeli ikaitwa machafuko, (Mwanzo 11:9)., Biblia inasema hivi ‘’Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Bwana; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu. Yeremia 51:7. Babeli ambao ni mji wa kijiografia ulioko Iraq, sasa ni magofu, kama manabii walivyotabiri ‘’Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwa-mwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko. (Yeremia 51:37). Lakini kiroho, Babeli ni mama mchafu anayelevya mataifa yote(Ufunuo 17:5), pia anawakilisha mji mkubwa katika falme za dunia unaobubujisha maji ya uasi katika mataifa yote kiasi cha mataifa kulewa. (Ufunuo 17:1-2). ‘’Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi. Ufunuo 17:18

YERUSALEMU: Neno Yerusalemu lina maana ya mji wa amani, hapo ndipo Mungu alifanya amani na watu wake. Yerusalemu ni mji wa Mungu na patakatifu pake (Zaburi 46:4). Na Mungu anaupenda ‘’Bwana ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo. Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee Mji wa Mungu. Zaburi 87:2-3. Na ndio mji pekee duniani uliochaguliwa na Mungu, Biblia inasema hivi ‘’lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo; na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli. ‘’( 2 Mambo ya Nyakati 6:6). Bwana Yesu alisema tusiape kwa mbingu wala kwa nchi wala kwa Yerusalemu ‘’kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. (Mathayo 5:35).

Yerusalemu ni mji uliopata kibali cha Bwana, na Mungu aliuweka kati ya mataifa kwajili ya kuunganisha mataifa kiroho, na hata kijiografia. Yerusalemu umeunganisha mabara matatu, moja, Afrika, pili, Asia na tatu Ulaya, yaani ni kiungo cha mataifa. Biblia inasema hivi ‘’Bwana MUNGU asema hivi; Huu ndio Yerusalemu; nimeuweka kati ya mataifa, na nchi zauzunguka pande zote, (Ezekieli 5:5). Yerusalemu kiroho ni mama yetu anayetulea katika neema ya Kristo ‘’Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. Wagalatia 4:26.

Babeli ni mji ambao ulishambuliwa sana na mataifa, na kila taifa kubwa liliukalia, Nebukadreza mpagani aliujenga sana, na baada yake mji huo ulikaliwa na Waajemi(Irani) na wakaufanya makao makuu yao, na baada yao, mji huo ulikaliwa na Alexandra mkuu Mgiriki na akaufanya makao yake makuu, na baadae ulikaliwa na dola ya Seliucid, kisha ulikaliwa na Rumi, na baadae Sassanid. Mji huo baadae ulitelekezwa na kuachwa ukiwa na mpaka leo ni magofu, na sasa Iraq imekaliwa na Marekani. Lakini mji wa Yerusalemi ndio mji pekee unaongozwa kwa kuvamiwa na mataifa, tangu kuwepo kwake duniani. Tazama historia ya kuvamiwa kwake mpaka sasa:-

1. Mwaka 1550-1400 BC Yerusalemu ulitwaliwa na dola ya Misri chini ya mafarao

2. Mnamo karne ya 12 BC Yerusalemu ulikaliwa na Wayebusi-wakanani

3. Mnamo 1000 BC Yerusalemu ulitwaliwa na mfalme Daudi na tangu hapo ukawa makao makuu ya Israeli.

4. Mnamo mwaka 586 Nebukadreza aliipiga Yuda na akaubomoa mji wa Yerusalemu kama Isaya 39:1-8 na Yeremia 32:28-29 walivyotabiri. Na mwaka wa 539 Babeli ilishindwa na Waajemi, na Wayahudi wakawa huru kurudi kwao na kuujenga mji wao tena kama Daniel 9 ilivyotabiri. Lakini Wayahudi walijikuta tena wapo chini ya utawala wa kigiriki wa Ptolemic empire ambao makao makuu yao yalikuwa Elexandria-Misri.

5. Mnamo mwaka 198, Yerusalemu ilitwaliwa na Seleucid empire chini ya Antiocus III, utawala huu pia ulikuwa ni wakigiriki ambao makao yake yalikuwa Syria.

6. Mnamo mwaka 63 KK, Yerusalem ulitwaliwa na Warumi chini ya Pompei, na ulidumu chini yao kwa mamia ya miaka, na Yesu alizaliwa akawakuta Warumi wanatawala, hata Herode hakuwa Myahudi bali Muidumea(Edom) ambaye alikuwa mfalme kibaraka wa Warumi, aliwekwa hapo kuanzia mwaka wa 37KK hadi 4KK, na vizazi vyake vikaendelea baada yake, na huyo ndo aliboresha na kulipamba vizuri hekalu la pili(second temple) la Suleimani. Linaitwa Hekalu la pili kwasababu ya lile la kwanza lilibomolewa na Nebukadreza mfalme wa Babeli mnamo mwaka 586 BC, na kujengwa tena na Zerubabeli, na Kuhani Ezra na Nehemia baada ya uhamisho wa Babeli, na likanakishiwa vizuri na Herode mkuu. Ndo maana watu walilisifia hilo hekalu kwa jinsi ya uzuri wake, Bwana Yesu alimwambia litabomolewa ‘’Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema, Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. Luka 21:5-6

1. Mnamo mwaka 66-70 BK, Wayahudi waliasi ufalme wa Rumi, na kukaanza machafuko, maana Wayahudi walikataa kujisalimisha, na mwaka 70 BK, Warumi walikuja na kuuangamiza mji wote na hekalu likabomolewa kama Daniel 9:26 ilivyotabiri pamoja na Bwana Yesu, Luka 19:42-44; 21:6,24

2. Mnamo mwaka 135 BK, Wayahudi tena walijipanga kuuchukua Yerusalemu chini ya Bar-Koba, aliyejinadi kuwa masihi, ila Warumi walimuua na kuvunjanja uasi wote wa Wayahudi na kuwafukuza kabisa eneo hilo na tangu hapo taifa la Kiyahudi likasambaratika kabisa duniani, ikabakia historia tu. Na Yudea-Israeli ikabadilishwa jina na kuitwa ‘’Aelia Capitolina” ili kupoteza kumbukumbu la Wayahudi. Na Warumi wakawachukua mataifa mbalimbali na wafilisti toka magharibi ya Israeli na kuwaweka hapo, na kuupa mji huo jina la Syria-Palestina, Palestina ni wafilisti, kwa Kirumi ni Palestina, na hapo ndipo chimbuko la jina la Palestina kuwepo mpaka leo. Rumi iliukalia mji huo, na katika zama za mfalme Costantino mnamo karne ya 4 BK, ukawa mji wa kikristo, na Costantino alijenga Kanisa katika eneo ambalo lilijengwa hekalu la Sulemani. Na mji ukaendelea kuwa chini ya Warumi katika sura ya kikristo.

3. Mnamo mwaka 614 Bk, dola ya Sassanid(waajemi) walivamia Jerusalem na kuitwaa na kuua wakristo 1000.

4. Mnamo mwaka 629 BK, Byzentine empire (Warumi) waliwashinda Waajemi tena na kuurudisha Jerusalem mkononi mwao.

5. Mnamo mwaka 638 BK Yerusalem ilitwaliwa na majeshi ya kislam chini ya Umar Ibn Al-kattab, na Umar Ibn Kattab alikuwa hajui eneo lilolojengwa hekalu la Suleman, akaonyeshwa na Kaab myahudi aliyesilimu, ndipo Umar akajenga msikiti wa mbao hapo, na tangu hapo waarabu/waislam wakaanza kuukalia mji huo. Na mwaka 687 BK, kiongozi wa waislam wakati huo bwana Abd al Malik alijenga Qubbat Al-Sakhra yaani dome of the rock kwa kiingereza, pamoja na kujenga msikiti wa alaqsa pembezoni mwa dome of the rock, msikiti huo ulikamilika mwaka 705 BK. Dome of the rock na msikiti wa alaqsa zimejengwa katika eneo lililokuwepo hekalu la suleman lililobomolewa na Warumi mwaka 70BK. Waislam walibomoa kanisa la mtakatifu Maria katika eneo hilo ndipo wakajenga msikiti wao hapo. Waislam wasio na elimu wanadanganya kwamba msikiti huo ulikwepo tangu Suleiman, ni wazushi tu, lengo lao ni kujimilikisha eneo hilo. Lakini baadae msikiti huo ulipata zahama ya kubomoka mara mbili sababu ya tetemeko la ardhi, mara ya kwanza ulibomoka mwaka 746 na kujengwa tena mwaka 754 na kalipha al-Mansur wa dola ya kislam ya Abbasid. Na ulijengwa tena mwaka 780 na al-Mahdi mrithi wa Al-Mansur. Na mwaka 1033 msikiti wa al-Aqsa ulibomoka kabisa na kusambaratika kwa tetemeko kubwa, miaka miwili baadae ukajengwa tena na Kalipha Ali az-Zahir wa dola ya kislam ya Fatimid, umbo hilo limedumu mpaka leo ingawa ulishafanyiwa matengenezo mara kwa mara na dola za kislam zilizofata. Mwaka 1099 ulitekwa na jeshi la msalaba lililoongozwa na Papa Urban II, na kufanywa kanisa na ghala za silaha, ila baadae tena mnamo mwaka 1187 ukarudi mkononi mwa waislam, na mnamo mwaka 1967 Jerusalem ilitwaliwa na serikali ya Israeli lakini msikiti huo ukabakia mikononi mwa wapalestina chini ya uangalizi wa nchi ya Jordan, ingawa sasa huko chini ya ulinzi wa Israeli. Waisraeli wanaamini huo msikiti utabomoka tena kwa tetemeko kubwa la tatu kupisha ujenzi wa hekalu la tatu la Suleimani ama utabomolewa kwa mashambulizi ya kivita, tusubiri tuone hilo. Tuendelee na historia ya mji wa Yerusalemu.

6. Mnano mwaka 1073, Yerusalem ulitwaliwa na Seljukid chini ya kamanda Atsis

7. Mnamo mwaka 1099, Yerusalemu ulitwaliwa na majeshi ya msalaba(Cruseder-Katholiki) chini ya Papa Urban II. Hawa waliua Wayahudi mno na Wakristo wasio katholiki pamoja na Waislam katika eneo hilo. Na wakaubadilisha msikiti wa alqsa na dome of the rock kuwa kanisa na kuweka msalaba na sanamu za Yesu na Maria. Wayahudi 6000 walichinjwa na majeshi ya msalaba kwasababu ya kupigana na jeshi hilo ili kuulinda Yerusalem wakiwa pamoja na waislam. Zama hizo Wayahudi walikuwa wamerudi na kusambaa katika mji wa Yerusalemu, Tiberias, Ramleh, Ashkelon, Caesarea, and Gaza. Jeshi la msalaba liliwatesa Wayahudi na Waislam na kuwabagua na wengine kuuzwa kama watumwa. Ila Wayahudi waliendelea kupambana na jeshi vamizi la kikristo wakiwa upande wa waislam. Mwaka 1141 Yehuda Halevi, mkuu wa Wayahudi huko Spain alitoa tangazo kwa Wayahudi kurudi katika nchi ya Israeli akiwemo na yeye.

8. Mnamo mwaka 1187, Sultan Saladini aliutwaa Yerusalem mkononi mwaka makruseda(Wakatholiki) baada ya kuhuusuru kwa siku 21, aliondoa misalaba katika msikiti huo na kuweka alama ya mwezi na nyota. Huyu aliwapa Wayahudi na wakristo uhuru wa kuja kuhiji hapo hata wa kuishi kasoro katika msikiti huo, hawakuruhusiwa kuukaribia. Wayahudi walimpenda Saladini walimwona kama Koreshi, na zama hizo walizidi kuja katika nchi ya Israeli na kuishi na kujenga masinagogi na kuishi kijamii, ila walisikitika sana na kulia kuona mji wao unakaliwa na wageni na eneo takatifu limejengwa msikiti na kanisa.

9. Mnamo mwaka 1229, Yerusalem ulitwaliwa tena na wakatholiki chini ya dola ya holy Roman empire iliyokuwa inatawaliwa na Frederick II huko Ulaya magharibi. Wayahudi walitupiliwa mbali maana papa aliwatangaza kama wapinga kristo.

10. Mnamo mwaka 1244 , Yerusalem ilitwaliwa na Khwarezimian Tatars

11. Mnamo mwaka 1247, Yerusalem ilitwaliwa na dola ya kislam ya Ayyubin iliyokuwa na makao huko Misri, waliowaondoa Khwarezimian Tatars

12. Mnamo mwaka 1258-Jerusalem ilitwaliwa na Mongolia chini ya Hulagu Khan, na kabla ya kuitwaa walivunja dola la kislam la Abbasid huko Iraq na kumuua khalifa na kumchukua mtoto wake, na waarabu wengi na kuwapeleka China kama watumwa, waliiteka Syria na nchi zote zilizokuwa chini ya dola ya kislam ya Abbasia ambayo ilidhibiti pia mji wa Yerusalemu. Hulagu Khan alisaidiwa na wanajeshi wa kikristo wachache katika vita vyake na waislam, alimwandikia ujumbe mfalme Louis IX wa Ufaransa kwamba Jerusalem iko katika mikono yao, na anaitoa kwa Wakristo. Wamongolia waliendelea kupigana na waislam na kufanikiwa kuwashinda huko mashariki ya kati, wakakimbilia Misri na na kukusanyika huko na kujenga dola la kislam la Mamluk. Mwaka 1260 Mamluki waliwashinda wa Mongolia, lakini mwaka 1299-1300 Wamongolia waliwashinda tena wa Mamluk na kuidhibiti Palestina. Historia inasema walipanga kumpa papa mji wa Yerusalem na story hiyo ilivyofika Ulaya ilileta furaha, na mnamo April 1300, Papa Boniface VIII alitoa agizo la kipapa la kusherekea tukio hilo la Wamongolia la kuirudisha Jerusalem chini ya wakatholiki, na wakafanya uhusiano wa kibalozi. Lakini mwaka huo Wamongolia waliondoka Palestina na kufanya dola la kislam la Mamluki kudhibiti tena mji wa Yerusalem.

13. Mnamo mwaka 1517 , Yerusalem iliangukia mkononi mwa dola kuu la kislam la Othoman empire, na waliikalia mpaka mwaka 1917. Othoman iliweka uhuru wa pekee kwa Wayahudi, Wakristo, na Waislam hasa kipindi cha Sultan Suleiman the Magnificent. Kwa uhuru huo, Wayahudi walijiimarisha na kutaka kutengeneza senhedrin(baraza la kiyahudi) la kale, pamoja na kuunda nchi ya Israeli, lakini mtawala mpya wa Othoman alishtuka na kumfukuza Rabi Bareb aliyechaguliwa kuwa mkuu na marabi kwajili ya mkakati huo.

14. Mnamo Dec 17, 1917, British empire kwa kikosi kilichoongozwa na general Edmund Allenby wakaitwaa Yerusalem toka kwa Othoman Empire, tangu hapo Yerusalem ikawa huru bila kukaliwa na taifa lolote. Na Wayahudi walikuwepo wengi zama hizo maana walikuwa wameshaanza kurudi taratibu taratibu tangu kitambo, lakini utaifa wao haukutambulika kwa jina la nchi ya Israeli bali kwa jina la Palestina, na walianzisha gazeti la Palestina post, baaada ya uhuru likaitwa Israeli post.



Waisraeli waliishi katika maeneo yenye ukame na kuyabadilisha kuwa rubta, na wakazidi kununua maeneo ya rutuba toka kwa waarabu na wapalestina na kuanza harakati za kutafuta uhuru toka kwa Waingereza. Wayahudi walitumia akili zao kuimiliki nchi hiyo, kwasababu waliwekeza katika kilimo cha kisasa na ufugagi na viwanda, huku waarabu na wapalestina wakishika dini tu na kujikuta wamekuwa wafanya kazi wa Wayahudi, na kwa uzembe wao wakawauzia Wayahudi maeneo yao, na Wayahudi wakamiliki sehemu kubwa ya nchi hiyo. Leo Wapalestina wanalia na kutaka maeneo yao yarudishwe huku babu zao walishauza kwa mikataba ya bayana. Muyahudi hana hatia maana aliishi maeneo ya ukame na kuyafanya miji na mshamba ambayo waplestina walikuja kufanya kazi hapo kwa ujira, na maeneo ya rutuba yaliyokuwa yanakaliwa na wapelestina yakabaki kizembe tu, namwisho Wayahudi wakayanunua na kuendeleza kilimo na viwanda na kujenga miji mizuri. Watu wengi hawajui kwamba nchi yote ikiwemo Gaza inatawaliwa na Wayahudi kiuchumi, na wapalestina kwa asilimia kubwa ni watumishi wa Wayahudi, lakini wapalestina wa Gaza ndio wakora dhidi ya Israeli, na huko ndipo kuna kikosi cha Hammath kinachopigana na Wayahudi.

Na wapalestina wa Gaza hawapatani na wapalestina wa miji mingine hasa west bank, na wala hawaoleani na wa Gaza, maana wa Gaza ni wakorofi. Na si kwamba wapalestina wote ni waislam, kuna wakristo miongoni mwao. Na waarabu na waislam si kwamba wanawapenda wapalestina, la, wanawatetea wapalestina kwa lengo la kumiliki Jerusalem na si kwa mapenzi na wapalestina. Kwa kuhakiki hilo, Mwaka 1970/71 Wapalestina walipigana na serikali ya kiarabu ya Jordan ambayo ilikuwa inadhibiti msikiti wa Alqsa, zama hizo wapalestina wengi walikimbilia Jordan nakutaka kuunda serikali yao ndani ya nchi ya Jordan katika mji mkuu wa Amman, vilizuka vita vikali vilivyoua wanajeshi 15000 wa palestina waliokuwa wanajiita PLO wakiongozwa na Yesse Arafat. Mauaji hayo yaliwapa hasira wapalestina na kuanza kufanya ugaidi uliojulikana kama black September, walijitoa muhanga na mwisho walifanikiwa kumuua waziri mkuu wa Jordan Wasif al-Tel huko Cairo Misri, na kusabisha mgogoro mkubwa sana baina ya serikali ya Jordan. Ndipo serikali ya Jordan ikawafukuza wapalestina huko Jordan, na Yesse Arafat alitoroka huku amevaa nguo za kike, lakini ugaidi wa black September uliendelea zaidi hata umoja wa waarabu ulishindwa kuzuia, ni Serikali ya Israeli ndio iliingilia kati na kuanza kuwaua magaidi kupitia shirika lake la kijasusi la Mossad na kuwafutilia mbali. Kwaiyo vurugu zote hizi za Waislam ni kuutaka mji wa Yerusalem, Wayahudi wakimiliki nchi yote na kuwapa waislam Jerusalem utaona wanatulia tuli. Kwaiyo hizi kelele za kutetea wapalestina ni kasumba tu, lengo ni kutengeneza dola la kislam lenye makao matatu, Makka, Madina na Yerusalemu kama walivyofanya zamani.

Itaendelea......
 
Katika mada zote humu JF kuihusu Jerusalem hii imeenda shule; ni ya kufungia mwaka 2017. Hongera sana Mkuu kwa historia ya kweli iliyoenda shule. Yaani ni facts tupu.
 
Waislamu hawana pakutokea
Wana madai ya kijinga kweli hao jamaa; eti msikiti ule ulijengwa tangu enzi za Sulemani; jinga kweli. Kumbe support yao kwa mafilisti ni ili kupata uhalali wa kuumiliki Jerusalem uhalali ambao hata hao mafilisti hawana labda kwa mbaali wayebusi na wakanaani wangeweza kujenga hoja wakaeleweka ila ndio hivyo tena walishafutika juu ya uso wa dunia.
 
Mwanzo mzuri, conclusion mbaya.

Palestina wanataka nchi yao based on mipaka ya mwaka 1967 ambapo wao wanataka East Jerusalem na Waisraeli wabaki na West Jerusalem Full stop. Hakuna mahali Wapalestina wanadai Jerusalem yote.

Kitu kingine Waisrael wamekuwa wakijenga settlements kibabe katika ardhi za Wapalestina, Resolution kibao za UN na baraza la usalama zimepinga hili, kwa mfano UN security council resolution number 2334 ya mwezi January mwaka 2017 ilikemea vikali hatua za Israel kunyakua na kujenga katika ardhi za Wapalestina kinguvu.

Pia mleta mada lazima ufahamu kwamba wakati Wa kuanzishwa kwa Taifa la Israel mwaka 1948 kulitokea vita kati ya nchi za kiarabu ( Misri na Jordan) na israel ambapo Mamilioni ya Wakazi Wa Palestina walikimbia vita , hats hivyo mpaka leo hii Israel haitaki hao watu warudi nyumbani, tunajua Kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa kuwazuia wakimbizi kurudi nchi zao za asili wakihisi Kuwa ni salama kurejea baada ya vita.

Mleta mada umezungumzia suala la Wayahudi kununua ardhi za wapalestina, hii ilitokea miaka ya mwanzoni kabla ya Taifa la Israel halijasimama, ambapo wapalestina walikuwa wakiuza ardhi kwa watu waliodhani ni binadamu wenzao kama Mimi na wewe tunavyoweza kuuziana ardhi, hawakujua wenzao wana nia mbaya ya kuwatoa katika nchi mazima, hata hivyo Hawakuuza maeneo yote ndiyo maana walibaki kwa wingi sana kabla ya malaki kuswagwa na jeshi la Israel ilibkuwafukuzia ukimbizini Jordan wakati Israel inaanzishwa.

Halafu mleta mada, unajustify vipi Waisrael kuwatangazia wayahudi wenye utaifa Wa Mataifa mengine kuhamia Israel halafu wakati huohuo Israel kuwapora ardhi watu wenye historia yao ya vizazi na vizazi ambao wapo na wanaishi hapohapo na kisha ardhi hiyo kuwapa hawa wahamiaji wasio na shida ya nchi huko walipo?, hawa Wapalestina waliozaliwa hapohapo, mababu zao wamezikwa hapo hapo, babu za mababu zao wamezikwa hapohapo unataka waende wapi?

Kitu kingine ambacho hukisemi ni Kwamba Palestina kuna Wakiristo wengi kuliko walioko Israel, na hawa Wakiristo maslahi yao Juu ya Mji Wa Jerusalem yanalindwa kwa nchi yao ya Palestina Kuwa na share katika mji huo!. Ifahamike Kuwa Wapalestina Wakiristo nao wanafeel connection na mji mtakatifu kwa sababu nao wapo hapo maelfu ya miaka!
 
Mwanzo mzuri, conclusion mbaya.

Palestina wanataka nchi yao based on mipaka ya mwaka 1967 ambapo wao wanataka East Jerusalem na Waisraeli wabaki na West Jerusalem Full stop. Hakuna mahali Wapalestina wanadai Jerusalem yote.

Kitu kingine Waisrael wamekuwa wakijenga settlements kibabe katika ardhi za Wapalestina, Resolution kibao za UN na baraza la usalama zimepinga hili, kwa mfano UN security council resolution number 2334 ya mwezi January mwaka 2017 ilikemea vikali hatua za Israel kunyakua na kujenga katika ardhi za Wapalestina kinguvu.

Pia mleta mada lazima ufahamu kwamba wakati Wa kuanzishwa kwa Taifa la Israel mwaka 1948 kulitokea vita kati ya nchi za kiarabu ( Misri na Jordan) ambapo Mamilioni ya Wakazi Wa Palestina walikimbia vita , hats hivyo mpaka leo hii Israel haitaki hao watu warudi nyumbani, tunajua Kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa kuwazuia wakimbizi kurudi nchi zao za asili wakihisi Kuwa ni salama kurejea baada ya vita.

Mleta mada umezungumzia suala la Wayahudi kununua ardhi za wapalestina, hii ilitokea miaka ya mwanzoni kabla ya Taifa la Israel halijasimama, ambapo wapalestina walikuwa wakiuza ardhi kwa watu waliodhani ni binadamu wenzao kama Mimi na wewe tunavyoweza kuuziana ardhi, hawakujua wenzao wana nia mbaya ya kuwatoa katika nchi mazima, hata hivyo Hawakuuza maeneo yote ndiyo maana walibaki kwa wingi sana kabla ya malaki kuswagwa na jeshi la Israel ilibkuwafukuzia ukimbizini Jordan wakati Israel inaanzishwa.

Halafu mleta mada, unajustify vipi Waisrael kuwatangazia wayahudi wenye utaifa Wa Mataifa mengine kuhamia Israel halafu wakati huohuo Israel kuwapora ardhi watu wenye historia yao ya vizazi na vizazi ambao wapo na wanaishi hapohapo na kisha ardhi hiyo kuwapa hawa wahamiaji wasio na shida ya nchi huko walipo?, hawa Wapalestina waliozaliwa hapohapo, mababu zao wamezikwa hapo hapo, babu za mababu zao wamezikwa hapohapo unataka waende wapi?

Kitu kingine ambacho hukisemi ni Kwamba Palestina kuna Wakiristo wengi kuliko walioko Israel, na hawa Wakiristo maslahi yao Juu ya Mji Wa Jerusalem yanalindwa kwa nchi yao ya Palestina Kuwa na share katika mji huo!. Ifahamike Kuwa Wapalestina Wakiristo nao wanafeel connection na mji mtakatifu kwa sababu nao wapo hapo maelfu ya miaka!
Mada itaendelea haraka ya nini ndugu?
 
Mleta mada anajua historia Ila ni mbaguzi. Mdini na muuaji.
 
Mleta mada anauendekeza udini. Ila ujue kuwa wayahudi(akina netanyau) ndio waliomtesa yesu. Na mpaka kesho hawatomkubalk
 
El ni Mungu alie juu,the most high na sio miungu.
Melkizedeki aliabudu huyu mungu mkuu na pia abraham aliabudu huyuhuyu mungu,
actual huyu mungu aliabudiwa na makabila mengi pale caanan,ndo maana unakuta majina kama BabEl-lango la mungu

ishmael-Mungu kasikia

israel-mungu kashinda
etc.

Na unakuta hata Nebukdenezer kaitwa mtumishi wa huyu mungu
na pia yule mtawala wa persia koreshi nae kaitwa mtumishi wa mungu huyuhuyu.

Lakini pia baadhi ya watu katika jamii hizi waliabudu miungu wengine kama baal,Dagon ,salem etc,
lakini the most high God alikuwa ndo El.

Mwenyewe sasa tafuta connection ya El na Allah,na kwanini waislamu husema abraham,adam etc walikuwa waislam.

Elewa kuwa maana ya muislamu ni mtu anaemnyenyekea mungu
 
Kitu kingine mleta uzi kapotosha melkzedeki na adon zdek ni mtu na mwanae,yaani baada ya melki baadae Adon ndo akatawala.

Kitu kingine,wafalme wa israel walikuwa wakitawala kwa kusimikwa na empire kubwa,mfano egypt walikuwa wakitawala eneo lote hilo na walichagua mtu kutoka eneo hilo awe mfalme na awasilishe kodi kwa wamisri,
na misri ilipopigwa na waasyria,vilevile watawala wa israel ama yuda waliwajibika kwa superpower alikuwa anatawala eneo hilo,hali hii iliwakuta watawala wengi wa israel kuachia Saul,daud na solomon ambao hata uwepo wao bado unatiliwa shaka kama kweli waliwahi kuwepo.
Mfano kuna baadhi ya wafalme kama josia walijikuta wakiuawa na farao pale walipoasi,kuna wafalme wengine waliwekwa jela babel walipoasi na kurudishwa tena madarakani walipokubali kulipa kodi kwa babel,
kitu kingine kinadhihirisha kuwa mungu El hakuwa mungu wa taifa la israel pekee ni uwepo wa mfalme wa syria aliekuwa akiitwa Hazael,
pia kwa mjibu wa bibilia Nebukedner alikuwa mtumisha wa mungu,na mungu ndo alimtuma kuungusha utawala wa yuda baada ya madhambi kuzidi,
lakini pia mfalme wa persia aliitwa mtumishi wa mungu,na ndio aliwatoa wayahudi utumwani babel na kuwasaidia kujenga hekalu lao,
bible haikumuongelea alexandra za great ambae nae katawala eneo hilo baada ya kuwaangusha wapersia,
 
NI MDA SASA WA KUICHUKUA JERUSALEMU. (2)

Neema na iwe kwako msomaji, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Kama mtumwa wa Mungu Jafari Massawe nitangulize samahani kwa kuchelewa kutuma sehemu ya pili kwasababu zisizozuilika. Katika sehemu ya kwanza tuliishia mwaka 1917 mwaka ambao Yerusalemu ilikuwa huru (no man land). Sasa tutaendelea sehemu ya pili ambayo tutaanzia tulipoishia mpaka wakati huu, hatua kwa hatua. Fatana nami sasa:-

15. Mnamo mwaka 1948 Israeli ikazaliwa chini ya kibali cha umoja wa mataifa na serikali ya waingereza iliyokuwa inatawala eneo hilo. Na mwaka huo vikatoa vita vikali baina ya waarabu na wayahudi, vilivyoigawa nchi hiyo, lakini Wayahudi waliwashinda waarabu kwa aibu, na kupanua eneo zaidi. Lakini Jerusalem haikuguswa maana ilikuwa chini ya uangalizi wa umoja wa mataifa kupitia utunzaji wa Jordan, na Wayahudi walizuiliwa kuhiji katika temple mount-mlima wa mizeituni na baadhi ya maeneo matakatifu.

16. Mnamo mwaka 1967, Waarabu na waislam walivamia Israeli kwa majeshi makubwa sana yaliyopewa msaada na Warusi, na vikazuka vita vya siku 6, lakini walishindwa vibaya mno na kusababisha Israeli ikalie west bank(ukingo wa magharibi wa mto Yordan), Sinai-Misri, wakachukua eneo la Golani-toka kwa Syria, na kuitwaa Jerusalem moja kwa moja iliyokuwa chini ya uangalizi wa Jordan. Golani ni sehemu ya Israeli ambayo ilikaliwa na kabila la Manase, na ulikuwa mji wa makimbilio ya mwenye kuua bila kukusudia( Kumb 4:41-43). Tangu hapo Wayahudi walijenga mji mkubwa na mzuri upande wa magharibi wa Yerusalemu, lakini walizuiliwa na UN kukaribia msikiti huo wa alaqsa wala dome of the rock ambayo zimejengwa Yerusalemu mashariki, ingawa Wayahudi wenye msimamo mkali mara kwa mara waliitaka kuingia humo lakini walichomwa visu na wapalestina, na hali hiyo ilisababisha machafuko yaliyofanya Wayahudi kulipiza kisasi kwa kuua wapalestina zaidi ya 170 mwaka 2006. Na tangu mwaka 1967 vita vya mara kwa mara vilizuka baina ya Israeli na waarabu ili kuikomboa Jerusalem lakini mwaka 1980 walishuhudia Israeli ikiutangaza Yerusalem kama makao makuu ya Israeli, na hali hiyo iliwatia hasira Waarabu na Waislam lakini walishindwa na kunyamazishwa kabisa mpaka leo.

Mpaka hapo tumepata historia fupi dhidi ya mji mkongwe wa Jerusalem, sasa twende tukaangalie mkakati wa kutwaa na kuuondoa msikiti wa Alqsa na ili hekalu la 3 lijengwe na kuanza zama mpya, lakini kabla ya yote yanaweza kutokea machafuko makubwa sana baina ya ulimwengu wa magharibi na waarabu kwasababu ya msikiti huo wa al-aqsa au mji wa Yerusalem kwa ujumla, na sasa tunaona ishara hiyo. Ebu tuangalie kiini cha mgogoro wa mji huo ambao hasa upo katika eneo la mlima Moria-temple mount au alaqsa:-

Mlima Moria ama mlima wa mizaituni ndipo Hekalu la Mungu na Ikulu ya ufalme wa Daudi ilijengwa(2 Nyakati 3:1), na utukufu wa Mungu ulijidhihirisha sana katika eneo hilo, ni eneo zuri sana, na hapo ndipo Ibrahimu alimtolea Isaka kafara(Mwanzo 22:2), na ndipo Bwana Yesu alisulubiwa, na hapo ndipo Bwana alipenda kwenda na wanafunzi wake kupumzika, kuwafundisha, na sauti ya Mungu ilisikika hapo toka mbinguni, (Mathayo 17:1-7; 24:3), na ndipo Yesu alipokamatiwa, kusulubiwa, kuzikwa, kufufuka na kupaa tokea hapo, (Mathayo 26:30-57; Yohana 19:41, Matendo 1:4-12), na kwa mujibu wa unabii eneo hilo ndilo Yerusalemu mpya itatua na kukaa. Na waislam wanasadiki kwamba mtume wao Muhamad alipalia hapo katika safari yake ya Miraji(kwenda mbinguni) ni eneo bora kwa dini kubwa tatu, Wayahudi, Wakristo na Waislam. Kwaiyo linagombaniwa sana hasa na Wayahudi wenye msimamo mkali, Wakatholiki na Waislam wenye msimamo mkali, ila kwa mujibu wa mafundisho ya mitume wa kikristo, walifundisha kwamba wakristo hawana haja ya kupigania mambo yao kwa nguvu za kijeshi bali kiroho, (Waefeso 6:12), na Bwana Yesu ambaye ndiye kiongozi wa wakristo hakufundisha hayo bali aliwafundisha wakristo kwa maneno haya ‘’….saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika MLIMA HUU, WALA KULE YERUSALEMU. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Yohana 4:21-23.

Kwaiyo ibada za mlima au mji wa Yerusalem zilishakoma kwa mujibu wa fundisho la kristo, kwaiyo mkristo mwenye mtazamo na Yerusalem wa sasa kiimani na kiroho, hatakuwa tofauti na dini zingine zenye mtazamo wa dunia wa kugombania ardhi hiyo kwa nguvu za dola. Kwa mujibu wa mafundisho ya mitume wa kikristo, Mji wa Wakristo ni Yerusalem mpya ijayo, ambayo kwa imani tayari imeshafikiliwa-kufikiwa (Waebrania 12:22-24), na mji huo ndio mababa (Ibrahimu, Isaka na Yakobo) waliutazamia, Biblia inasema hivi ‘’Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. (Waebrania 11:10). Mtume Yohana katika Roho aliuona na akaunenea hivi ‘’Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. (Ufunuo wa Yohana 21:2). Swali linakuja, je Yerusalemu wa sasa unahusika na utabiri wa siku za mwisho? Jibu ni ndio. Tutaenda kuona hilo sasa kwa habari ya unabii wa biblia nje ya historia tuliyoiona, swala hili bilashaka litagusa imani zetu lakini hatuna budi kujifunza.

Kuna mambo matatu juu ya utabiri na mipango ya siku za mwisho kupitia mji wa Jerusalem. Nitaenda kuyachambua yote ili tupate jumla, hiyo mipango na utabiri ipo katika nyanja tatu kama ifuatavyo:-

I. Biblia
II. Wayahudi
III. Illuminat

BIBLIA: Katika agano la kale mji wa Mungu ulikuwa ni Yerusalemu na hapo ndipo Yahweh aliongoza kiroho, ‘’Kibanda chake pia kiko Salemu, Na maskani yake iko Sayuni, (Zaburi 76:2.), na sasa mji wa Mungu ni Yerusalem wa mbinguni ambapo Bwana wetu utawala kuanzia hapo ‘’…tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, (Ufunuo 1:5). Baada ya Wayahudi kumkataa Yesu, mji wa Yerusalem uliachwa ukiwa yaani bila Mungu, na uliwekwa chini ya mataifa ambao waliukanyaga na kutesa wayahudi, kama Bwana Yesu alivyotabiri ‘’[WAISRAELI] WATAANGUKA KWA UKALI WA UPANGA, NAO WATATEKWA NYARA NA KUCHUKULIWA KATIKA MATAIFA YOTE; NA YERUSALEMU UTAKANYAGWA NA MATAIFA, HATA MAJIRA YA MATAIFA YATAKAPOTIMIA. LUKA 21:24

Majira ya mataifa ya kuukanyaga Yerusalemu yalikoma mwaka 1917 mwaka ambao Yerusalemu ulikuwa huru, haukuwa tena mji wa mtu (NO MAN LAND). Na mwaka 1948, Taifa la Israeli lilizaliwa, na Wayahudi wengi walizidi kuja kwa wingi, hasa baada ya kusumbuliwa na kuteswa huko katika nchi za kiarabu walizokuwa wanaishi baada ya kusambaratika kama taifa, na mateso hayo yalitokea sababu ya uhusiano mbaya baina ya taifa la kiyahudi na waislam kuanzia mwaka 1948. Na mwaka 1967 Israeli ikautwaa Jerusalemu mpaka leo hii mji huo upo chini ya Israeli. Lakini bado kuna mivutano ya mataifa ambayo bado hawakubali mji huo ni wa Wayahudi, nayo ni mataifa ya kiarabu na Kislam na baadhi ya mataifa ya kikristo na mengineyo, wameugawa mji huo mara mbili, Wapalestina-mashariki, na Wayahudi-magharibi kwa mujibu wa umoja wa mataifa. Ila upande wa mashariki ndio kuna mji mkongwe ambao una historia ya Biblia amabao Wayahudi wanautaka na tayari wameshauteka tangu 1967, na Waislam pia wanautaka kwa madai ni makao yao matakatifu ya tatu ya dini ya kislam, na wakristo hasa wakatholiki wanautaka maana kuna makanisa yao hapo ambayo wanajipatia kipato kupitia hija za wakristo, lakini pia wanamalengo makubwa dhidi ya mji huo kama tulivyoona kule juu, walishauteka mara kwa mara kiasi cha kuwaua Wayahudi eneo hilo, inasemekana papa analihitaji sana eneo hilo kwa lengo la kuufanya mji huo kuwa makao makuu ya dini ya ulimwengu ijayo. Kwaiyo kuna mivutano mikubwa sana ya kimataifa dhidi ya Yerusalem ambayo itaenda kutimiza unabii wa Biblia, mivutano hiyo pia itachangia Wayahudi wengi wamjue Yesu sababu ya hofu ya kuangamizwa. ‘’Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao. Warumi 11:26-27. Unaweza kusema je Mungu si aliwatupa Waisraeli, iweje tena awasaidie?, katika Makala hii nitagusia swala hilo lakini zaidi unaweza kurejea somo hili: Mungu hajawaacha Wayahudi:LINK:

Ila kabla hawajaokoka sharti utimilifu wa mataifa ukome kabisa, ina maana gani? Unabii huo upo kama ifuatavyo ‘’Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. Warumi 11:25. Ugumu unaoongelewa hapo ni wao kuikataa injili ya Kristo, na huo ugumu ni kwa sehemu, kwamba nafasi bado wanayo na hata sasa kuna Wayahudi 200,000 ni wakristo, lakini mwamko mkubwa wa uongofu wao utaonekana baada ya mataifa kuikataa injili kabisa na kuanza kupigania mji huo badala injili ya kristo, na hapo ndipo utimilifu wa mataifa utafikia kabisa, na Waisraeli watafunguliwa mlango wa ugumu wa ufahamu wao na kumwona Yesu kama ndiye masihi wao waliyemkataa kwa miaka 2000 iliyopita, ndipo watalia na kuomboleza kama Zakaria alivyotabiri. ‘’Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; NAO WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. Zakaria 12:10.

Sehemu ya unabii huu ulitimia siku ya kusulubiwa kwa Yesu, maana unabii waga unajirudia, ‘’Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma, (Yohana 19:37 ), na Roho wa neema alimwagwa siku ya pentecost, waliokoka Wayahudi 3000 kwa siku hiyo baada ya mahubiri ya Petro (Matendo 2:41). Lakini unabii huu utatimia zaidi siku hizi zijazo, Wayahudi wengi wataondolewa ugumu(utaji) na watamwona masihi Yesu kama Bwana na mwokozi wao, na wataanza kujuta na kulia kwa uchungu na kuomba rehema. Biblia inasema hivi ‘’Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi. Zakaria 31:1. Roho ya neema ni Roho Mtakatifu, Waebrania 10:29. Mtume Paulo pia anasema hivi ‘’Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao?....Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama SI UHAI BAADA YA KUFA? Warumi 11:12,15. Ni Dhahiri uongofu wa Israeli ni ishara ya kurudi kwa Yesu na mwisho wa dunia. Ebu tuamke sasa.

Je mataifa watapata suluhisho juu ya Yerusalemu?

Itaendelea…
 
Mleta mada, acha uongo wako hapa,

Hujui historis ww rejea maktaba ukasome
 
Ha ha ha,mleta mada anafurahisha kweli,
anadhani kila mtu hakwenda shule,

nikimwambia wafilist kama wanavyojitahihidi kuwaponda nao mungu aliwaleta nchi ya ahadi kaanan atabaki anang'aa macho wakati maandiko yapo tena ndani ya bibilia,
 
Wana madai ya kijinga kweli hao jamaa; eti msikiti ule ulijengwa tangu enzi za Sulemani; jinga kweli. Kumbe support yao kwa mafilisti ni ili kupata uhalali wa kuumiliki Jerusalem uhalali ambao hata hao mafilisti hawana labda kwa mbaali wayebusi na wakanaani wangeweza kujenga hoja wakaeleweka ila ndio hivyo tena walishafutika juu ya uso wa dunia.
Ipo siku watasema ulikuwepo tangu adamu na hawa,kama ambavyo wanasema adamu alikuwa muislamu
 
Back
Top Bottom