Ni muda gani UTUMISHI huita kwa Interview baada ya deadline?

Abdul kalaam

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
435
545
Habari zenu wadau

Naomba kufahamishwa ni muda gani inachukua utumishi kuita waombaji kwenye interview baada ya deadline.

Inategemea , kuna wengine two weeks,wengine mwezi na kuendelea.
 
ni kweli. Mtu ame-apply, shortlist bado, interview bado (written na oral interview) halafu anataka kujua muda wa kuitwa kazinì.
Kusota kitaa sio lelemama mkuu, mtu kukubaliwa tu ajiraportal kuapply anahisi kawin tayari, ndio haya maswali yanamjia kichwani na kutaka kufahamu.

Watu wenye kazi, wakiapply kazi nyingine sehemu huwa hawana muda wa kufuatilia, wengine wanakuka kushtuka kuwa wamekuitwa interview kwa kuambiwa na marafiki wa karibu.

Ukiona mtu anauliza haya maswali ujue hana kazi kabisa na anatamani aipate hata hiyo siku.
 
uzi ungenoga bila comment yako.
 
Mkuu, nipo kitaa toka 2016. Mpaka sasa nasubiria shortlist kwa kuangalia kwenye tovuti ya PSRS.
Hata kama tumekaa muda mrefu lakini hatuna budi kusubiri taratibu zao zikikamilika huwa wanaweka kwenye website yao. Kujipa presha kwa kuulizia hatua ya tatu mbele wakati hatua ya kwanza hujui ikoje itasababisha stress.
Hata mtoto mdogo huzaliwa, huanza kukaa, huanza kutambaa, husimama, hutembea kisha hukimbia. Subira yavuta heri. Time will tell.
Toka mwaka huo interview mbili (ikiwepo kwenye taasisi 1 nyeti sana ambako inasifika kwa utamu wa asali yake, yaani salary) nilitoboa hadi oral interview, tatu nikaishia written interview. Nyingine naisikilizia shortlist, ilitangazwa mwezi May.
 
Back
Top Bottom