Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,181
- 1,579
Sasa ni wazi kuwa kila Mwana familia anayo hofu juu ya ujauzito huu wa mama yetu!
Kwani siyo siri kuwa mama-ccm umri wake wa uzazi salama umeshamtupa mkono!
Huko nyuma haikuwa shida kiivyo kwani wakati akimzaa kifungia mimba wake, mwili wake ulikuwa na nguvu za kutosha kiasi cha kutohitaji usaidizi kama ilivyo kwa wakina mama wengi leo.
Wakati huo wengi tulitiwa moyo kadri siku ya kujifungua ilivyokuwa ikikaribia na baada ya kitambo kidogo; shangwe na nderemo zilienea katika kila kona ya nchi.
Hongera mama ccm kwani umepata Mtoto mwanaume aitwae JK wa kwanza! Kijana mzuri na wapekee kabisa.
Sijui ni kwa sababu ya nguvu za ujana wa mama huyu, au ni kitu gani, mimi sijui. Kwanini nasema hivyo?
Wakati wa ujana wake huyu mama; alikuwa na malezi au tuseme miiiko ya kipekee sana, kiasi cha kumfanya huyu kijana kupata malezi ya kina, na hatimae kuja kuwa msaada na tegemeo la familia nzima mpaka kwa majirani pia.
Pamoja na kujiunga na nyota ya kijani; hata hivyo mama-ccm kwa mfuatano unaokubarika alifanikiwa kujipatia watoto wengine wa kiume watatu ambao ni Mwinyi, Ben na Jk wa pili, pasipo kupatata matatizo yoyote ya uzazi, hongera sana mama-cmm.
Muda umeendelea sana tokea wakati huo!
Ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu mama-ccm apotuletea JK wa pili; kijana mwenye haiba ya ucheshi, kipenzi cha watu wote bila kujali ni vijana au wazee.
Katika familia yetu ni nani ambaye atamsahau?
Tukiwa vijana wakubwa tunaoishi na mama yetu wa makamo; sasa tuna mashaka makubwa, kwani kumbe bi mkubwa ni mja mzito tena; na hii ni mimba yake ya tano ilihali umri wake wa uzazi salama ulishapita kama wasemavyo madaktari.
Kama wana familia kwa nini tusiwe na hofu?
Vipimo vinaonesha kuwa mtoto ni wa kiume tena, sawa, kwani kwetu tulishazoea ni wa kiume tu!
Lakini tatizo lililopo hapa ni haya mambo ya kutoeleweka yanayoendelea katika mwili wake!
Mara mtoto acheze, mara asicheze, mara ageuke mara arudi kama mwanzo! Hebu jamani tuelezeni haya ndio madhara ya uzazi katika umri Mkubwa?
Juzi juzi hapa, mama yetu alihisi kabisa utungu, baada ya muda kidogo tu, eti utungu ukatoweka ghafla!
Ndugu pengine tuombe ushauri kuwa ingawa mama huko nyuma amekuwa akijifua mwenyewe bila kufanyiwa upasuaji; je kulingana na hali aliyonayo; tumpeleke akafanyiwe huo upasuaji ili kuokoa maisha ya mama na mtoto?
Na kama ndivyo je mama yetu ambaye amechoka sasa atatoka salama labour?
Au pengine tumuache tu na hii mimba yake inayoendelea kumfanyia kichefuchefu kiasi cha kushindwa kula!
Sio siri mimba ya mama-ccm inachanganya kweli.