Ni miezi minane leo toka serikali itoe ahadi hii kutimizwa ndani ya miezi miwili

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
837
495
Serikali kwa upande imejipanga kushirikiana na watumishi wa Benki Kuu pamoja na wafanyakazi wote nchini ili kuleta maendeleo ya haraka kwa nchi.

Mtakumbuka wakati wa Sherehe za Mei Mosi, Serikali ilifanya uamuzi wa kupunguza kiwango cha kodi ya mapato kwa watumishi wa Serikali kutoka asilimia 11 hadi 9. Tulifanya hivyo kwa lengo la kutoa motisha kwa wafanyakazi.

Kinyume na baadhi ya watu wanavyosema, Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda na kuwathamini wafanyakazi wa Serikali. Na hapa napenda kufafanua uamuzi wa Serikali wa hivi karibuni wa kusimamisha ajira mpya na promosheni zote Serikalini. Uamuzi huu umetokana na kuwepo kwa tatizo kubwa la wafanyakazi hewa Serikalini ambao idadi yake ni zaidi ya 12,000 hivi sasa.

Aidha, Serikali imebaini wapo wastaafu hewa zaidi ya 2000 ambao nao wanalipwa pensheni. Hivyo, ili kukabiliana na tatizo hili, Serikali imeamua kusitisha zoezi la kuajiri watumishi wapya na kutoa promosheni ili kujipa nafasi ya kushughulikia tatizo la wafanyakazi hewa.

Nina imani zoezi hili litakamilika ndani ya kipindi cha miezi miwili na baada ya hapo taratibu za ajira mpya na promosheni zitaendelea kama kawaida.
 
Awamu ovyo sana hii, siasa marufuku, ajira marufuku, na yenyewe haijafanya lolote la maana.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
FB_IMG_1487135683208.jpg
 
Back
Top Bottom