Ni miaka zaidi ya 60 tangu tupate uhuru, ila ni kama hatuna uhuru

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
6,503
Reaction score
18,949
Miaka 60 baada ya uhuru Tanzania hatuna wasomi wakuendesha bandari zetu mpaka tusaidiwe na waarabu?

Miaka 60 baada ya uhuru bado kumiliki gari Tanzania ni anasa!

Miaka 60 baada ya uhuru kuikosoa serikali ni makosa!

Miaka 60 baada ya uhuru bado watanzania vilio vyao ni maji na umeme?

Miaka 60 baada ya uhuru bado mitaala inafundisha mgunduzi wakwanza wa ziwa victoria na mlima kilimanjaro?

Miaka 60 baada ya uhuru wanaoenda kwenye kampeni wanapanda malori kama ng'ombe na wagombea wanapanda V8 special edition zero km!

Miaka 60 baada ya uhuru zao la kahawa limejifia, pamba haina soko, korosho ndio usiseme.

Miaka 60 baada ya uhuru hatuna ballistic missiles hata moja.

Miaka 60 baada ya uhuru hatuna viwanda vya nguo, toothpick, matairi, nyama, redio n.k

Miaka 60 baada ya uhuru mahakama hairuhusiwi kurusha kesi live, bungeni hairuhusiwi kujadili mada nyeti za watu kupotea!

Miaka 60 baada ya uhuru mitandao inafungiwa ila bado mashirika ya serikali yanatumia hiyo hiyo mitandao na wanafunga comments ☹️

*UNA NENO GANI LA KUWAPA CCM
 
Kwa kweli inasikitisha sana, hasahasa hapo kupakia watu kwenye malori kama ng'ombe, Watz akili tumefungia wapi lakini?
 

🤔🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…