Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Huu utaratibu wa Raisi wa nchi kutoshitakiwa awapo madarakani na hata baada ya kustaafu najua uko katika nchi kadhaa duniani na bila shaka kuna nchi zilikuwa na huu utaratibu kwenye katiba zao ila kwa sasa wameshaondoka nao baada ya kuona utaratibu huu unatumiwa vibaya.
Binafsi naamini mijadala yote tuliyonayo sasa ni matokeo ya utaratibu huu ambao humuondolea mtu hofu ya kutamka au kutenda lolote akijua ana kinga ya kutoshitakiwa popote kwa lolote atalotenda au kutamka akiwa madarakani na hata akistaafu.
Hata utaratibu wa kutumia Bunge kumuondoa madarakani au kumshitaki nao una mapungufu mengi tu yanayomfanya mtu huyu mwenye wadhifa wa uraisi asiwe na hofu yoyote kwani anaweza hata kulivunja Bunge wakati wowote achilia mbali idadi kubwa ya wabunge wa chama chake katika Bunge.
Swali ninalojiuliza hivi katika nchi zilizoendelea za Ulaya na Marekani ni nchi ngapi zina utatatibu huu?
Na kwa nchi zenye utaratibu huu, mashariti au taratibu za kufuata katika kutekeleza nia ya kumshitaki Raisi ni kama haya ya kwetu?
Kwa mfano,Raisi wa Marekani anaweza ku-dissolve senate?
Nasikitika sana hata Katiba inayopendekezwa bado inaendeleza huu utaratibu wa kinga ya Raisi licha wahusika kutuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao mara kwa mara na katika nyakati tofauti.
Napoona nchi tajiri na iliondelea kama Ufaransa Raisi wao anaweza kushitakiwa alafu sisi vinchi masikini na ombaomba tunaendekeza huu utaratibu huwa nashindwa kuelewa na zaidi nashindwa kuelewa ni kwanini kila siku tunajadilli athari zinazotokana na huu utaratibu lakini hatujawahi kuwa hata na mjadala wa kitaifa kutathimini upya umuhimu wa hii kinga ya Raisi au kinga hii kuwekewa mashariti mapya na si kuiacha kama ilivyo hivi sasa
Wanasheria,wataalamu wa kuandika katiba na wadau wengine, wakati umefika tuwe na mjadala wa kitaifa kuhusu hiki kinachoitwa kinga ya Raisi(ifanyiwe tahimini upya kama bado inatufaa) na si kila siku kulalamika na kujadili athari za hii kinga ambazo ndio chanzo cha yote haya.