Ni mara ya tatu sasa naomba ushauri kwa huyu dada

Pendaelli

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
10,488
29,683
Habari ya mchana wadau.
Ni mara nyingine tena naingia kwenye njia panda sababu ya dada yule dada alienikataa siku si nyingi. Niliomba ushauri hapa hapa jf na niliuzingatia kwa kweli, ila nilitahadharishwa kuwa anaweza kuja kunitafuta tena. Sikuwa na mawasiliano nae tena ila nilikua nuona tu kanisani lakini kila mtu na yake.
Sasa bwana jumapili iliopita baada ya juzi alinifuata na kuniomba samahani anaomba namba yangu aliokua nayo ilipotea na simu, na bila hiana na kwakua sikua na kinyongo nae na pia bado nilikua na hisia za kumpenda nikampa tukaachana.
Jioni yake alipiga na alianza kuomba radhi sana, akasema pia Mungu amemlipia kwa alichofanyiwa na huyo mr wake na akajua wazi kwa hicho alichomfanyia hakua mume wake bali ni mimi. Tokea kipindi kile hakuacha kuniota na roho ilikua ina muuma sana. Aliomba ushauri sehemu nyingi nakila aliemshauri alimwambia aje aniombe radhi. Basi na maelezo marefu yaliochukua siku mbili ikanibidi ni kubali tuu na haikua kazi ngumu kwangu, japokua na mi nilimuhoji mengi na majibu yake yakaniridhisha isipo kua mawili, moja sababu iliopelekea kugombana na huyo mtu wake, kisa ilikua ni simu tuu huyo jamaa alimpigia sim ikapokelewa na mtu mwingine ndio ikawa sababu ya ugomvi. Pili aliniambia alishatembea nae mara moja tuu, nayo iliniumiza kwani nilimpenda. Lakini tokea siku ile nimekua ni mimi namtafuta tuu na wala si yeye, nimeshamtumia sms zaidi ya 20 hajajibu hata moja na leo ni wiki imeisha hajanitafuta, tulikubaliana mambo kadhaa ya kuthibitisha ukweli wake ikiwa moja ni tukutane na kiongozi wa dini,sasa tokea jumatano kama leo hajanitafuta wala kujibu sms yangu. Hivi kuna ukweli wowote kwake au ananiongopea tena wadau. Kuna mtu alishawahi kukutana na hali kama yangu kweli? Na nivipi aliweza kuikabili labda ushauri wenu tafadhali, kila la heri.
 
Wewe nawe Mmmh mjinga sana, unaamini kabsaa kalala nae mara moja?? huyo mwanamke kiufupi ni muongo na hakufai, endelea nae akuletee maumivu na maradhi, mana hafai kwa matumizi ya binadamu, huyo anataka kukutumia au akuweke kama second option akiumizwa na jamaa anakuja kujipoza kwako, na inaonekana anampenda sana huyo jamaa mwengien, sasa kurudi kwako nikatika kulinda penzi la kule , mana kuna tabia moja kwa mwanamke akiwa anapenda sehem ni rahisi kuvumilia lakin kama mwanaume anampenda na hataki kumuacha basi atatafuta pakupozea nafsi yake halaf anarudi tena kwa yule, wewe umewekwa kama boya tu hana mapenzi na wewe, na wala hana shida atakupotezea muda tu.
 
we kiaz kabisa umempeperusha tena mkuu.. hautamwona tena.. dhambi kubwa ni kumuuliza mwanamke maswala ya ex boyfriend n lazma ajikataee aisee..
 
Alivokuja kwako kule kwa jamaa kulikuwa kumesanuka sasa hivi wamesawazisha mambo yao umekimbiwa ... Subiri yakimchachia atarudi tena.... Nahisi wewe amekuweka kipozeo tu kwamba akizinguana huko anakuja kwako ama? Hakuna upendo wa kweli alafu sidhani kama kakutana na huyo mwanaume mara moja hilo ni tango pori.... Embu Anza mchakato wa kumtafuta mwingine
 
Hivi bado unahitaji ushauri?? Tukushauri nini hapa?? Yaonesha weye ulikuwa bikra na ulipompata huyu akachukua na ile akili yako kabisaa. Haya Pokea like langu kwa kukubali kufanywa bawaba ya mlango. We uwaingize wengine weye ubaki na mlango
 
Wewe nawe Mmmh mjinga sana, unaamini kabsaa kalala nae mara moja?? huyo mwanamke kiufupi ni muongo na hakufai, endelea nae akuletee maumivu na maradhi, mana hafai kwa matumizi ya binadamu, huyo anataka kukutumia au akuweke kama second option akiumizwa na jamaa anakuja kujipoza kwako, na inaonekana anampenda sana huyo jamaa mwengien, sasa kurudi kwako nikatika kulinda penzi la kule , mana kuna tabia moja kwa mwanamke akiwa anapenda sehem ni rahisi kuvumilia lakin kama mwanaume anampenda na hataki kumuacha basi atatafuta pakupozea nafsi yake halaf anarudi tena kwa yule, wewe umewekwa kama boya tu hana mapenzi na wewe, na wala hana shida atakupotezea muda tu.

i love your signature
 
wewe inaonekana kanisani hauendi kwa lengo la kumuabudu mungu ila unamfuata huyo mama. Eti mshikaji wangu kama yeye amekaa kimya kwani na wewe unashindwa kukaa kimya, kwanini unamtafuta?. Mwisho maelezo yako yanaonesha kua wewe ni bikira.
 
Mwenye post ameniudhi sana, ni kilaza sijapata kuona na inaonekana hana sifa yoyote ya kupendwa ma mwanamke ndio maana anang'ang'ania mschana asiyempenda.

Nimeoma views kama 500 hivi lkn response kama 10 tu, hii inaaksi uboya na umbulula wa mtoa maada.

Ndio maana huwa sishauri watu wa namna hii.
 
ila huu mtindo wa mtu anaomba ushauri mnaanza kumtukana na kumkejeli mnakatisha tamaa xn
Sio kutukana mkuu. Watu wa hivi ni lazima waambiwe kwa maneno makali ili akili zao zifunguke. Kumwambia kwa kumlealea ni kuzidi kumharibu. Tumezoea kuona mwanaume wa kiafrika akiwa jasiri na sio kuchomwa na kamwiba kadogo analia km kama kavunjika mguu. Kuna tatizo likiletwa hata unaowaita watukanaji wanasubiri wapate ushaur maana km linampata mtu anaweza kuwa chizi.
Mimi nasema mleta mada kazidiwa kila kitu na huyo dada...kielimu, kiujanja wa mjini labda hata kipato.
WANADAMU WA KIUME WAPO HATARINI KUTOWEKA
 
Back
Top Bottom