Narudia tena siwezi kuwa na wema wa mshumaa.Pole sana mwalimu, hizo ni baadhi tu ya changamoto za ualimu. Mwalimu kuna mahali unakosea sana, tena naweza kusema hata mbele ya muumba wako unafanya kosa kubwa.
Ulijifunza Ethics and codes of conduct za mwalimu, unajua wajibu wako kwa serikali yako, jamii inayokuzunguka, mwajiri wako, na KWA MTOTO.
Nasikitishwa na ulichokisema, ..."shuleni naenda kuonekana tu na sifanyi maandalizi ya kufundisha hivyo darasani ni mwendo wa kutimiza wajibu sio kuwaelimisha wanafunzi.." hivi kweli mwalimu unadhani anayekandamiza haki zako ni nani? je ni MTOTO/MWANAFUNZI unayetakiwa kuwajibika juu yake kama ulivyoelekezwa na taratubu za ualimu?
Haudhani kufanya hivyo ni kumkosea haki huyo mtoto asiyekuwa na hatia? kufanikiwa kwenye maisha hakuhitaji kukata tamaa, endelea kukomalia haki zako lakini sio kwa kuua kizazi cha badae, wape wanafunzi haki zao, wewe komaa na waajiri na serikali yako.
Jaribu kubuni fursa za maendeleo ili upanue kipato chako badala ya kutegemea mshahara tu. Unachokifanya kwa sasa ni kujikusanyia laana kwa kushindwa kutimiza ipasavyo wajibu wako kwa viumbe wasio na hatia (WANAFUNZI). Kila laheri.