Ni mamlaka ipi ina amri na dereva na leseni yake?

Ni mamlaka ipi ina amri na dereva na leseni yake?

Mtu_Mzima

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Posts
1,174
Reaction score
1,150
Ukifuatilia mkanganyiko uliopo sasa kwenye fani ya udereva haswa mafunzo na usimamizi wa leseni unabaki unajiuliza maswali mengi sana. Mfano.

1. Kwa sasa mamlaka inayotoa leseni ( issuing authority) ni Tanzania Revenue Authority- TRA. Lakini anayependekeza madaraja ni Polisi ( vehicles inspector). Trafiki barabarani wanaamini leseni wametoa wao. Wanazichukua, wanazifungia nk. HII SI KUDHARAU MAMLAKA WALIOTOA LESENI? KWANINI WASIANDIKWE POLISI KAMA NDIO MAMLAKA WANAOTOA LESENI?

2. HIKI NI KITUKO. Mamlaka zilizopewa kazi ya kufunza madereva ( NIT NA VETA ) wanawafunza madereva wanawapa vyeti vyao. Unapeleka polisi unapangiwa madaraja. UNAPOENDA KUJISAJILI LATRA NAO WANAKUPA MTIHANI. Hii sio kudharau mamlaka iliyokupasisha ? Kwanini taasisi za serikali zinadharauliana mbele yetu? Unapodharau cheti cha mwezio ndo mnatupa ujumbe gani?

3. Kwanini isiundwe mamlaka moja itakayosimamia maswala ya Leseni za udereva na sheria za usalama barabarani ? Ikawa ni sheria ya usafirishaji?

4. Leseni za sasa zote vifutwe. Kuwe na kipindi cha mpito. Kuwe na makundi 5 ya leseni za udereva na zote zitofautishwe kwa rangi zake.
A. Leseni ya udereva wa magari madogo, na abiria wasiozidi 12, pikipiki, bajaji nk.
B. Leseni za udereva wa mabasi na malori ( mabasi ni malori ya abiria)
C. Leseni za udereva wa mitambo ya aina zote.
D. Leseni za vyombo vyepesi vya majini ..boats, mitumbwi nk
E. Leseni za boats, feries, meli nk.

Kuwe na database na kuwe na mafunzo maalum kwenye vyuo vilivyosajiliwa na hiyo mamlaka na mitihani yake isimamiwe centrally. Maana hata sasa mitihani vya VETA na NIT inatofautiana na bado wote wanapata daraja C .

Kwa kifupiii mfumo ufumuliweeee
 
Mamlaka yenye amri ya leseni na dereva ni zile zinazosimamia sheria za usalama barabarani.
NB. Mahakama hutafsiri sheria.
Ukifuatilia mkanganyiko uliopo sasa kwenye fani ya udereva haswa mafunzo na usimamizi wa leseni unabaki unajiuliza maswali mengi sana. Mfano.
Ni kweli na tunapata tabu 7bu hata ukienda vyuo vya udereva hatupatiwi uwelewa wa kutosha kuhusu hilo, na hupelekea kuwachukia Polisi tukajiona tunajua na tukawadharau, na ndipo wanapotunyoosha kwa kuona polisi tunawadharau.
1. Kwa sasa mamlaka inayotoa leseni ( issuing authority) ni Tanzania Revenue Authority-
TRA hutoa leseni ila siyo ya udereva.
TRA hukusanya mapato ya leseni ya udereva kutoka kwa dereva husika na kutoa kadi inayoonyesha mwisho wa kodi hiyo na sio mwisho wa leseni ya udereva. Sheria haikulazimishi ku rinyuu bali inakutaka usiendeshe chombo cha moto 7bu hujalipa kodi. Ndio maana TRA wanachokifanya kwa dereva alie kwepa kulipa kodi. Mfano, Leseni iliisha 10/01/2020 derva akarinyuu 02/01/2023 ili iishie 01/01/2027. TRA watatoa muda uliokwepa kodi hiyo na kukupa kadi hii, KUTOKA 02/02023 na KUISHA 01/01/2025.
TRA. Lakini anayependekeza madaraja ni Polisi ( vehicles inspector).
Kiufupi, Polisi/v.inspector hapendekezi bali ndiye anayethibitisha wewe unapaswa kuwa na daraja lipi kwa draiving yako au usiwe na leseni kabisa. (Hapa hutoelewa vizuri ila kifupi Polisi/V.INSP ndie anayetoa leseni) Kama unayo leseni na hukupita kwa V.INSP, ambaye ni Polisi akakuthibitisha kuwa wewe unafaa kua na leseni au la, jua ulipata leseni bila utaratibu wa kisheria.
Trafiki barabarani wanaamini leseni wametoa wao.
Wapo sahihi kwa wanacho kiamini. Ndio maana nikakwambia kiufupi leseni anayetoa ni Polisi. Hapa wa Tz wengi tunachanganya mafaili Trafiki sio mtu, bali ni sheria ya usalama barabarani. TNZANIA ROAD TRAFC ACT. Polisi pia sio mtu bali ni taasisi/idara ya kijeshi. Ndani ya polisi kuna vitengo mbali² kama FFU, STPU, CID, INTELIGENS, TASC FORCE, ANT-ROBBARY, D&H SECTION, GD, nk, hala kitengo mama ni GD, General Duties, hawa huvaa sare za Khaki ambazo huvaa V.INSPECTOR kwa huu huvaa koti la bluu/khaki na havai nguo nyeupe kwa 7bu ya kuchafuka ktk ukaguzi wa magari anapilala mvunguni mwa gari analolikagua.
Polisi yeyete aliyepangiwa kusimamia sheria barabarani siku hiyo na viongozi wake, bila kujali sare ya rangi gani, huyo ni Polisi na anatekeleza majukumu yake ya kisheria. S. 95 Tz Trafc act. Sisi tumekariri alievaa sare nyeupe ni Trafiki, sio hivyo, yole ni polisi anaesimamia sheria za usalama barabarani, crown ktk kofia zao huwa na vishikizo/vifungo na majina ktk mashati yao ndio vile vlile, havibadiliki maana anahamisha kutoka shati mojwa kwenda jengine anapofanya usafi.
Wanazichukua, wanazifungia nk.
Wakichukua leseni basi kuna shida kwa dereva inayopelekea siendesha gari kwa muda huo na kubaki polosi kama kielelezo endapo amepewa muda wa kufika kituoni kwa taratibu za kisheria.
Polisi hafungii leseni, ila akikupeleka mahakamani ndio leseni hufungiwa kwa mujibu wa kosa lako, na endapo polisi akikukazia kuthibitisha uhalali wa leseni yako hapo ndipo Vehicle Inspecter aliekupatia/aliekuthibitisha kuwa na leseni atatakiwa aje kuthibitisha mahakamani, aje yeye ama iletwe PF alioijaza wakati ukiwa naye ktk tray, sasa kama leseni uliletewa nyumbani PF haikujazwa na wewe pia unafungwa kwa kosa la kughushi nyaraka za serekali (kufoji)
HII SI KUDHARAU MAMLAKA WALIOTOA LESENI? KWANINI WASIANDIKWE POLISI KAMA NDIO MAMLAKA WANAOTOA LESENI?
Hawadharau. V.Insp ni askari Polisi.
Kuna tofauti kati ya leseni ya udereva na cheti cha udereva. Ndio maana Polisi hadai cheti.
TRA unaenda na fomu ya Polisi PF ndio ukilipa 70,000/= utapewa kadi ila wakiwa hawana kadi utatumia ile copy ya PF na risiti za malipo ya kodi ya leseni kutoka TRA bila shida yeyote.
2. HIKI NI KITUKO. Mamlaka zilizopewa kazi ya kufunza madereva ( NIT NA VETA ) wanawafunza madereva wanawapa vyeti vyao. Unapeleka polisi unapangiwa madaraja.
Mamlaka ya kufunza madereva ni nyingi sana, Vyuo vipo vingi sana mikoani kila kona, na hutoa vyeti vya udereva. Ila havijapewa mamlaka ya kutoa leseni ya udereva. NIT ni cha serekali, hivyo pale pale chuoni wale walimu baadhi yao ni ma V.INSP ambaye ni Polisi, ndio maana unapata leseni na cheti bila usumbufu 7bu walikufundisha polisi wenyewe. VETA pia huwa wanakuanao.
UNAPOENDA KUJISAJILI LATRA NAO WANAKUPA MTIHANI. Hii sio kudharau mamlaka iliyokupasisha ? Kwanini taasisi za serikali zinadharauliana mbele yetu? Unapodharau cheti cha mwezio ndo mnatupa ujumbe gani?
Hawadharau bali wanajiridhisha maana kuna vyuo havijasajiliwa kutoa baadhi ya madaraja.
3. Kwanini isiundwe mamlaka moja itakayosimamia maswala ya Leseni za udereva na sheria za usalama barabarani ? Ikawa ni sheria ya usafirishaji?
Polisi ndio yenye jukumu hilo, hatuna uelewa tu wakutosha ndio maana tunajichanganya kwa hawa jamaa na kuona tunawadharau.
4. Leseni za sasa zote vifutwe. Kuwe na kipindi cha mpito. Kuwe na makundi 5 ya leseni za udereva na zote zitofautishwe kwa rangi zake.
A. Leseni ya udereva wa magari madogo, na abiria wasiozidi 12, pikipiki, bajaji nk.
B. Leseni za udereva wa mabasi na malori ( mabasi ni malori ya abiria)
C. Leseni za udereva wa mitambo ya aina zote.
D. Leseni za vyombo vyepesi vya majini ..boats, mitumbwi nk
E. Leseni za boats, feries, meli nk.
Hii ni lawama kwa serekali na Polisi. Kama uhakiki tu wa daraja la leseni na cheti cha udereva imeleta shida watu hawana vyeti, zikifutwa zote itakuaje?
Kuwe na database na kuwe na mafunzo maalum kwenye vyuo vilivyosajiliwa na hiyo mamlaka na mitihani yake isimamiwe centrally. Maana hata sasa mitihani vya VETA na NIT inatofautiana na bado wote wanapata daraja C .
Mtihani ukifanana huo sio mtihani tena, ni masahihisho.
Kinacho angaliwa ktk mitihani ni uwelewa na sio ukariri. Mfano:- Dar-Mwanza sio sawa na Dar-Mbeya ingawa wote mtapita Dodoma.
Kwa kifupiii mfumo ufumuliweeee
Mfumo hauna shida, shida ni wanaotakiwa kuuelewa mfumo.

KUHUSU MADA HII INA MAMBO MENGI SANA HADI VIFUNGU VYA SHERIA, UKIONA WACHANGIAJI NI WACHACHE UJUE ULICHO KIWEKA MKUU NI VIGUMU SANA MTU KUKUCHAMBULIA HADI UELEWE KWA UNDANI, HAPO KUNA VINGI NIMEVIACHA ILI KUFUPISHA. Ahsante.
 
Ukifuatilia mkanganyiko uliopo sasa kwenye fani ya udereva haswa mafunzo na usimamizi wa leseni unabaki unajiuliza maswali mengi sana. Mfano.

1. Kwa sasa mamlaka inayotoa leseni ( issuing authority) ni Tanzania Revenue Authority- TRA. Lakini anayependekeza madaraja ni Polisi ( vehicles inspector). Trafiki barabarani wanaamini leseni wametoa wao. Wanazichukua, wanazifungia nk. HII SI KUDHARAU MAMLAKA WALIOTOA LESENI? KWANINI WASIANDIKWE POLISI KAMA NDIO MAMLAKA WANAOTOA LESENI?

2. HIKI NI KITUKO. Mamlaka zilizopewa kazi ya kufunza madereva ( NIT NA VETA ) wanawafunza madereva wanawapa vyeti vyao. Unapeleka polisi unapangiwa madaraja. UNAPOENDA KUJISAJILI LATRA NAO WANAKUPA MTIHANI. Hii sio kudharau mamlaka iliyokupasisha ? Kwanini taasisi za serikali zinadharauliana mbele yetu? Unapodharau cheti cha mwezio ndo mnatupa ujumbe gani?

3. Kwanini isiundwe mamlaka moja itakayosimamia maswala ya Leseni za udereva na sheria za usalama barabarani ? Ikawa ni sheria ya usafirishaji?

4. Leseni za sasa zote vifutwe. Kuwe na kipindi cha mpito. Kuwe na makundi 5 ya leseni za udereva na zote zitofautishwe kwa rangi zake.
A. Leseni ya udereva wa magari madogo, na abiria wasiozidi 12, pikipiki, bajaji nk.
B. Leseni za udereva wa mabasi na malori ( mabasi ni malori ya abiria)
C. Leseni za udereva wa mitambo ya aina zote.
D. Leseni za vyombo vyepesi vya majini ..boats, mitumbwi nk
E. Leseni za boats, feries, meli nk.

Kuwe na database na kuwe na mafunzo maalum kwenye vyuo vilivyosajiliwa na hiyo mamlaka na mitihani yake isimamiwe centrally. Maana hata sasa mitihani vya VETA na NIT inatofautiana na bado wote wanapata daraja C .

Kwa kifupiii mfumo ufumuliweeee
Hilo nalo mkalitizame
 
Back
Top Bottom