Ni mambo yapi kimsingi UKAWA wanakubaliana na Rais Magufuli?

Fortilo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
5,025
15,656
Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) umekuwa kimya tangu na baada ya uchaguzi wa oct 2015 na hata baada ya kuapishwa kwa Rais wa jamuhuri, mengine tunayosikia ni personal opinions za wana UKAWA na bado hatujapata maoni yao kwa ujumla, ili pengine wale tunaowasapoti tujue muelekeo wa upinzani wao kwa serikali hii ni upi..

Personally nakubaliana na mambo kadhaa anayofanya Rais Magufuli hasa vita dhidi ya wazembe na mafisadi japo sikubaliani moja kwa moja na njia zinazotumika lakini angalau kuna kazi inafanyika
Bado kuna mambo kama kusimamia kodi, kuimarisha utumish wa umma, kusimamia sheria na kuwajali wananchi wa kipato cha chini..

Pamoja na yote hayo ningependa kujua ni yapi hayo ambayo UKAWA kwa ujumla wao wanakubaliana na Mh.Magufuli bila kujali itikadi ya vyama vyetu ili pengine ajisahihishe pale inapoonekana dhaihiri kuwa anakosea

Ni hayo tu,
Wasalaam.
 
Mimi namsubiri apewe Chama kwanza ndiyo nitakoment ila ni mapema Sana kumuamini mtu wa ccm kwa sasa, maana mambo Mengi aliyofanya yanahitaji muda kujua kafanya kwa dhamira au ni kutafuta kick za kisiasa, maana majipu yamesimamishwa kazi tunasubiri uchunguzi ukamilike kwanza na hatua watakazo chukuliwa
 
1. Kujaribu kurudisha nidhamu iliyo kuwa imepotea/potezwa na walio pita
2.kuondoa ama kupunguza ule u "unajua mimi ni nani?" kwa wale walio kuwa na nafasi zao serikalini
3....... kadri siku zitakapo songa nitaongeza
 
Back
Top Bottom