Ni makosa kuituhumu VIP Engineering

Ni makosa kuituhumu VIP Engineering

SERGIO

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
348
Reaction score
147
Kampuni ya VIP Engineerinf inatuhumiwa kimakosa kwamba imefanya vitendo vya uvunjifu wa sheria kuhusiana na Akaunti ya Escrow. VIP si mshirika katika mkataba wa Akaunti ya Escrow ya Tegeta na haikuwa na jukumu lolote like katika uanzishwaji wake au katika ulipwaji wa fedha kutoka katika akaunti hiyo, wala VIP sio mwanahisa tena wa kampuni ya IPTL. VIP ililipwa fedha na mnunuzi wa hisa zake na kwa hakika itakuwa ni kumuonea VIP kumtaka kujua fedha alizolipwa na mnunuzi zilitoka wapi. Isitoshe malipo yenyewe aliyoyapata VIP yalitokana na kushupaa hadi kwenda mahakamani na kupatiwa amri iliyowezesha kulipwa.
 
Ukweli ni kwamba VIP ililipwa kwa msingi wa Mkataba wa Uuzaji wa Hisa uliotangazwa na kuridhiwa kwa amri ya Mahakama ya Septemba 5, 2013; na kufuatiwa na amri ya mahakama ya Januari 17, 2014 iliyotolewa katika shauri la wazi; na baada ya kuwa imefanya malipo ya shilingi za Tanzania bilioni 38 { sawa na dola za Marekani Milioni 23.6} katika Mamlaka ya Mapato Tanzania {TRA} kwa ajili ya kugharimia malipo tote ya kodi ya VIP. Kwa ujumla VIP ilipokea fedha kwa mauzo ya hisa zake iliyokuwa imeruhusiwa kuziuza; mauziano hayo na malipo yalifanyika kwa uwazi mkubwa na kwa ruhusa ya mahakama na VIP si tu kwamba imeahidi kulipa kwa ukamilifu kodi zozote zile bali tayari ilikwisha kukabidhi TRA shilingi Bilioni 38 kama kodi mbalimbali kutokana na mauzo hayo.
 
Wakati benki ya Standard Chartered inashinikiza kwamba fedha za akaunti ya Escrow ni halali yake, haiyumkiniki pesa hizo zikawa ni zile zile ambazo PAC inadai kwa makosa kwamba ni za Serikali. si sahihi hata kidogo. Aidha, PAC haikusema wazi fedha hizo za Escrow ni mali ya umma kwa misingi gani. Ni vizuri PAC ikasema wazi kikokotoo kilichotumika kufikia uamuzi huo kwamba fedha za akaunti ya Escrow ni za umma. Yaani tuambiwe wazi Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini walikuwa wakimlipa nani hizo fedha na kwa shughuli gani?
 
Ni kazi kubwa na ngumu kuwasiliana na mtu ambaye anaamini anajua kila kitu na ana msimamo kuhusu suala mnalotaka kuwasiliana naye. Aidha, ni vigumu kuwasiliana na kujadiliana na mtu ambaye hana shida na ukweli kwani anao msimamo unaotokana na yale anayoamini yeye. Suala la hoja halipo tena badala yake kuna suala la imani. VIP inaamini kwamba ni muhimu kuchunguza na kutoa taarifa huru kuhusu IPTL. Taarifa ambayo haitakuwa na mashinikizo ya kisiasa wala kiuchumi na kijamii. Kwa sababu VIP inaamini kwamba tuhuma zilizogeuzwa hatimaye kuwa eti ni ushahidi kamili wa kuweza kufikia mahali pa kuwahukumu watu na hata kutaka kufungwa kwao na kufilisiwa zimekengeuka na zinahitaji kuangaliwa kwa jicho kavu bila ya mawenge.
 
Leo sina hasira kwa hiyo situkani...only today ila hawa Majambazi wanatakiwa kufukuzwa even nchini...watafute nchi hisani wakaishi huko!
 
Ni vyema kutambua kwamba haitusaidii kama taifa kuhemuka na kunyoosheana vidole. Kwa mini tusifanye uchunguzi wa kina I'll kujua mambo kadhaa kama vile Mechmar ni nani na VIP in nano? Mini uhusiano wao na nani anayo nafasi gani katika suala hill la umeme na mgogoro wa haya malipo?
 
Mwanzo wakati tunajenga hoja hapa kuhusu tuhuma dhidi ya VIP zilikuwa za kisiasa mno wengi walihisi baadhi yetu siyo wazalendo lakini penye ukweli tuongee ukweli na siasa tuwaachie wanasiasa,tumesoma hivyo tunatakiwa kuchambua mambo kwa analysis zenye facts na si mihemuko
 
.... Mbona Unajitekenya Halafu Unacheka Mwenyewe?
 
Back
Top Bottom