Ni Mafisadi United dhidi ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Mafisadi United dhidi ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 14, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,772
  Trophy Points: 280
  Ni Mafisadi United dhidi ya nani?

  [​IMG]
  [​IMG]

  KWA wale 'vijana wa zamani' watetezi na waumini wa Marxism, watakumbuka kwamba huwezi kufanikisha mapinduzi au mabadiliko katika jamii (kama vile Maisha Bora kwa Kila Mtanzania) kama migongano iliyopo katika jamii haijakomaa vya kutosha; wenyewe wanaita kwa Kiingereza sharpening of contradictions.
  Ndugu zangu, kilichotokea na kusemwa wiki iliyopita, kwenye kikao cha Kamati ya Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wabunge wa chama hicho mjini Dodoma, Kinadhihirisha vitu viwili.
  Kwanza, kwamba kweli kuna ombwe la uongozi nchini, na pili kwamba migongano katika jamii inakaribia kukomaa ipaswavyo na hivyo kutoa fursa ya kufanya mabadiliko tunayoyahitaji. Ni matumaini yangu kwamba mwakani Watanzania watapiga kura kwa busara wakijua kwamba muda wa mabadiliko umewadia.
  Kuhusu ombwe la uongozi, si tu kwamba kuna ombwe la uongozi, lakini pia dunia yetu ya siasa imejaa viongozi ambao ni wasanii, wanafiki na wachumia tumbo.
  Mambo yanayoelezwa kusemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, kwenye kikao cha kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi cha kuchunguza uhasama miongoni mwa wabunge wa CCM na serikali yao, yanadhihirisha yote hayo.
  Kwa mujibu wa Sophia Simba, hakuna msafi CCM. Amewarushia madongo hata wabunge wa chama hicho wanaoonekana angalau kuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi mkubwa ulioshamiri nchini.

  Ni picha gani tunayoipata wabunge wa chama tawala wanaporushiana madongo badala ya kuwa kitu kimoja katika vita hiyo? Ni picha ya Taifa lenye ombwe la uongozi; kiasi kwamba hata wenye dhamana ya kuchukua hatua nao wanalalamika.
  Sofia Simba ameripotiwa kulalamika katika kikao hicho kwamba Mzee Malecela na mkewe Anne Kilango walichotewa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel Sh. milioni 200 ili wawahonge wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wapate kumchagua mzee huyo kuwa mgombea urais wa CCM.
  Kauli kama hiyo ikitoka kwa Waziri ambaye TAKUKURU na Idara ya Usalama Usalama viko chini yake, inaibua maswali mengi. Swali kubwa ni kwamba ni kwa nini yeye kama Waziri hakuchua hatua zozote za kuwashitaki watu hao wawili kama asna uhakika wa jambo hilo?
  Kwa nini naye alalamike kama mwanachi wa kawaida ; ilhali yeye ndiye Waziri anayepaswa kutenda? Kama alichukua hatua na akakwamishwa, kwa nini hakujiuzulu?
  Vyovyote vile, kilichotokea Dodoma ni uthibitisho mwingine tena kwamba Taifa linayumba. Lakini hiyo si mara ya kwanza kwa taifa kuogelea katika mawimbi makali. Tulishuhudia hivyo wakati wa Mwalimu Julius Nyerere, lakini hali haikuachiwa kuwa mbaya kiasi hicho - ilidhibitiwa.
  Lakini leo, hatuoni dalili za hali hii kudhibitiwa isipokuwa kuendelea kuwa mbaya zaidi. Tangu Rais Kikwete ashike hatamu za uongozi, ni kitu kimoja tu kilicholigawa taifa na kinachoendelea kuligawa taifa – ufisadi, ufisadi, na ufisadi zaidi!
  Juhudi zote za Rais Kikwete za kujaribu kuwaunganisha Watanzania na kusonga mbele kwa pamoja kujiletea maendeleo, zinafifishwa na kitu kimoja tu – Ufisadi.
  Na hiyo ni kwa sababu yeye mwenyewe amekuwa akicheza usanii katika kulishughulikia tatizo hili. Nasema anacheza usanii kwa sababu huwezi kuimaliza culture of impunity kwa kuwafungulia kesi hawa na kuwaacha wale; huku ukisingizia kwamba “wengine ni wajanja na hawakamatiki’.
  Kikwete anasema kwamba kwenye ufisadi hana rafiki, lakini hajaonyesha kwa vitendo kama kweli ni muumini hasa hasa wa hicho anachokisema.
  Si siri kwamba baadhi ya watuhumiwa wakubwa wa ufisadi ambao, kwa hakika, ndiyo chanzo cha taifa kwa miaka takriban minne sasa linazungumzia ufisadi tu, ni hao wanaoaminika kuwa ni marafiki zake (angalau hajapata kuwakana hadharani).

  Hao ndiyo wanaomfanya aendelee kucheza usanii katila kila fursa anayoipata ya kulimaliza tatizo hili once and for all. Alipata fursa kwenye mkutano ule wa kihistoria wa CCM uliofanyika Butiama, lakini alishindwa kuitumia.
  Alipata fursa nyingine kwenye mkutano wa karibuni wa NEC uliofanyika Dodoma, lakini pia hakuitumia, na badala yake mkutano ukageuka kuwa wa kumsulubu Spika Sitta kwa sababu tu ya kuwa upande wa wabunge wanaopinga ufisadi.
  Usanii unaochezwa wa kuahirisha tatizo linalosumbua taifa la culture of impunity (wa kuwabeba mafisadi badala ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria), ndiyo unaolifanya Taifa lisishughulikie mambo mengine ya msingi na libaki linazozana katika jambo moja tu – ufisadi.
  Kwa mfano, kuunda kamati maalumu inayoongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kushughulikia chuki iliyotanda miongoni mwa wabunge wa CCM, ni sawa tu na kufagia uchafu na kisha kuuficha chini ya zulia. Nasema hivyo, kwa sababu tatizo ni kubwa na haliishii tu kwenye wabunge wa CCM. Hili ni tatizo la Taifa zima linalohitaji ufumbuzi wa kitaifa na si wa ki-chama.
  Lakini yeye Rais Kikwete anaamini eti Mzee Mwinyi akikutana kwa faragha na wabunge wa CCM na akawapa fursa kuzungumza na kutoa madukuduko yao, tatizo litakwisha!
  Wamekutana Dodoma wiki iliyopita, je tatizo limekwisha? Sana sana limeongezeka kwa sababu chuki sasa zimezidi kujikita ndani ya mioyo ya baadhi ya wabunge wa CCM, baada ya kurushiwa makonde ya chini ya mkanda kwenye kikao hicho cha siri cha Dodoma.
  Sijui Mzee Malecela ni mtu mwenye hulka ya namna gani, lakini naweza kujenga picha kichwani mwake alivyokuwa akijisikia wakati yeye na mkewe Anne Kilango wakirushiwa makonde ya chini ya mkanda na Waziri wa Serikali, Sophia Simba.
  Sijui vilevile Sophia Simba ni mtu mwenye hulka ya namna gani, lakini pia nahisi aliumia sana wakati Mzee Malecela alipojibu mapigo nje ya kikao hicho kwa kusema kwamba Sophia Simba anaumwa (ni kichaa) na anastahili kupelekwa hospitali ya vichaa (Mirembe)!
  Hapo ndipo CCM ilipotufikisha. Na sidhani na siamini kama kamati hiyo ya Mwinyi au hata Rais Kikwete mwenyewe anaweza kuyaponya kabisa majeraha ya kina Mzee Malecela, kina Sitta na wengine; hata kama baadaye tutakuja kuambiwa mambo ni shwari ndani ya CCM.
  Nimetoa mifano ya Malecela, Sitta, Anna Kilango na Sophia Simba tu, lakini ukweli ni kwamba wako wengi, wakiwemo hata baadhi ya watuhumiwa wenyewe wa ufisadi. Majeraha yao hayatapona si leo au kesho. Chuki ndani ya mioyo yao haitaisha; hata kama watapiga picha za pamoja na wale waliokuwa mahasimu wao kisiasa (au kibiashara?)
  Kwa hakika, baada ya wabunge wa CCM kuanza kupigana makonde ya chini ya mkanda, sitashangaa huko mbele katika kikao kingine zikawa ngumi kamili za watu kutoana damu.
  Na damu hiyo ya kwanza (rejea filamu ya Rambo “First Blood”), ndiyo itafungua milango kwa damu nyingine kumwagika na hivyo taifa kuingia katika ile awamu ambayo sote, kwa muda mrefu, tumekuwa tukiihofia kutokea – awamu ya machafuko!
  Ndugu zangu, hapo ndipo culture of impunity ilipotufikisha. Laiti Rais Kikwete angekuwa anapambana na ufisadi mkubwa bila kuangalia huyu ni rafiki yangu au si rafiki yangu, huyu alichangia kwenye kampeni yangu au hakuchangia, Taifa lisingefikia hapo lilipofika.
  Naambiwa kwamba sasa watuhumiwa wa ufisadi wametangaza vita kamili, na wanakusudia kuanzisha himaya kubwa ya vyombo vya habari ili kudhibiti hisia za umma. Ninapozisikia habari hizo huwa najiuliza: Hivi timu hiyo ya Mafisadi United ni dhidi ya nani?
  Ni mjinga tu ndiye asiyejua kwamba vita hiyo ni dhidi ya Watanzania masikini ambao wengi wao huishi vijijini. Kama tusingekuwa na culture of impunity, mabilioni ya pesa za umma yasingeibwa kila mwaka na mafisadi, na badala yake yangetumika kupunguza mateso ya wanavijiji wetu na wanetu.
  Kwa hiyo kama mafisadi wametangaza vita kuu, basi ni vita dhidi ya asilimia 85 ya Watanzania masikini ambao ndiyo waathirika wakubwa wa ufisadi.
  Asiyeelewa hilo, nampa changamoto ya kulitafuta gazeti la Mwananchi la Novemba 5, 2009 na kuiangalia picha ya ukurasa wa kwanza inayowaonyesha wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Mgulusi, Kata ya Mazimbo, Manispaa ya Morogoro, wakiwa wanafanya mitihani yao huku wamekalia ndoo za plastiki darasani!
  Fikiria: Badala ya viti, wanetu wanakalia ndoo za plastiki darasani, na hiyo ni Kilomita chache tu kutoka Dar es Salaam. Hivi mabilioni ya pesa za EPA, Kagoda, Meremeta nk, yangewezesha kujengwa shule na hospitali ngapi nzuri na zilizokamilika?
  Lakini hilo halikuwezekana na halitawezekana chini ya culture of impunity ya serikali yetu hii ya chama tawala CCM. Watatoana roho kwenye vikao vyao, lakini bila kuitokomeza culture of impunity, hakuna kitakachobadilika!
  Na Richmond Je? Bunge limemaliza kikao chake wiki iliyopita bila kujadili utekelezaji wa Serikali wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu kashfa hiyo. Hakuna sababu za msingi zilizotolewa za Serikali kushindwa kuwasilisha ripoti hiyo kama ilivyotarajiwa.
  Wahusika wa kashfa hiyo na pia watawala wetu wanaweza kupumua wakidhani tatizo limekwisha! Lakini je, ni kweli tatizo la Richmond limekwisha au ni uchafu umefichwa tu chini ya zulia? Waingereza wanasema: What goes around comes around! Tafakari.
  Tafakari.
   
Loading...