SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,280
Hii tabia ya mabinti zangu inanikera sana.Nina haraka ya kwenda shambani,naingia kwenye gari naliwasha tayari kuelekea shambani, lakini oohhhh! dashboard inawasha taa kunieleza kwamba mafuta yako chini sana, hayatanifikisha shambani. Namwita binti akaniletee mafuta kituo cha karibu, na namkabidhi galoni na fedha akimbie mara moja. Eti anaanza kutafuta ndoo ya maji akaoge kabla ya kwenda.Nyongo inanipanda navumilia. Anamaliza kuoga (baada kama ya nusu saa hivi) anajivuuta kwenda kuvaa. Anaibuka toka chumbani akinukia marashi akisema: 'Niko tayari, galoni na hela viko wapi? Ninao mabinti watatu na wote wana tabia hii. Wanaonaje? Kituo cha petrol ni disko? Au hawataki kutumwa? Nauliza: Wasichana wote wako hivi au wa kwangu wana matatizo?