Ni maandamano

Ni maandamano

Hata kule North Korea tunakoambia nchi inaendeshwa kwa mkono wa chuma, maandamano yanaruhusiwa japo ni ya kumpongeza Kim Il Un na serikali yake.

Mwenye data naomba anifahamishe ni nchi gani katika sayari hii yenye sheria kama hii ya kuzuia maandamano!!. Ama kweli Tanzania ni AJABU JINGINE LA 9 LA DUNIA.
 
Taifa linakoelekea ni kuzimu sasa, kama watanzania watafikia hatua ya kutunga sheria zinazozuia watanzania wengine kufikisha hisia zao sehemu husika. Dawa ya tatizo kama migomo inayotokea nchini sio kuzuia watu kugoma physically bali ni kusuluhisha visababishi vya migomo, Yanapotumika mabavu ya kuwazuia waandamanaji ambao huandamana tena bila nia ya kufanya fujo bali ni kuwasilisha majonzi yaliyoko mioyoni mwao juu ya hali ya uongozi na maisha yao ni kuwalazimisha kutafuta njia nyingine ya kuweza kufikisha hisia hizo. Angalia nchi jirani walikojaribu kuzuia wananchi kueleza hisia zao kisiasa leo kuna vikundi vingi msituni vinavyosababisha nchi kuwa na vita kila mara. Hata hao M23 tunaowasikia wanahangaikia usawa wa madaraka na mali zinazoporwa katika nchi yao lakini leo wanaonekana ni waasi na kweli wanasababisha kutoweka kwa amani na leo dunia yote macho yako huko.

Naamini kabisa viongozi wetu wengi walioko katika chama tawala wanajua chimbuko la Timu ya mpira ya Yanga. Hivyo pamoja na mkoloni kuzuia mikusanyiko tena enzi hizo njia za mawasiliano zikiwa duni watanzania waliweza kutumia Njia kama za timu za mipira kuweza kukutana na kuongelea yanayowahusu. Sembuse leo na teknolojia zote hizi mbona wanatafuta kuwaita watanzania majina mabaya na ambao hawakustahili.

Mabadiliko ya raia kwa sasa ni sawa na maji katika mpira (Bomba) unapoyazuia yasipite basi usitarajie kingine zaidi ya mpira kupasuka. Tumeshuhudia nchi fulani alijiua kijana wa chuo kikuu aliyejishughulisha na kazi ya uchinga lakini kwa ujumbe aliouacha leo uongozi uliokuwepo madarakani imekuwa ni historia katika nchi hiyo.

Rejea Machafuko ya waislamu Mbagala Baada ya kutaka kuwazuia kwa mabavu madhara kila mtu aliyaona, Huko mtwara na lindi baada ya kutumia nguvu majibu yameonekana, Hata pale tu walipomzuia manyau nyau kufanya kazi yake huko TAG tulishuhudia kituo cha polisi kuchomwa moto.

Ni ushauri wangu, si hekima kulea na kukuza makosa na kuwaacha wahalifu lakini badala yake sheria zichukue mkondo wake PIA viongozi wetu wasome alama za nyakati na kumaliza migogoro ni kushughulikia vyanzo vya migogoro na sio kuwazima wenye migogoro kuzungumza na kusikilizwa juu ya migogoro yao tena kwa yule ambao wao wanahisi ndio msababisha migogoro na huenda ndiye anayeweza kutatua migogoro. Hii itapunguza matatizo na kulifanya taifa letu lizidi kusonga mbele likiwa na amani na utulivu.
 
Lengo la nchimbi ni kuwakomoa waislamu na si vinginevyo, waislamu kwa umoja wao wanaweza kuyasimamia maandamano, maana wakiamua wanaweanza andamana katikati ya jiji. Mfumo kristo huo, si kingine!
 
217174_457878434296521_129317152_n.jpg



,,,.jpg Hali si shwari
 
Back
Top Bottom