Ni maandamano

Ni maandamano

GK-Shayo

Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
18
Reaction score
2
Maandamano:

Mapendekezo ya serikali kutaka kuleta sheria ya kuzuia maandamano kutaligharimu taifa kama sio leo ni kesho au kama sio kesho ni keshokutwa. Maandamano ni namna ya watu kuelezea hisia zao zinaweza kuwa furaha au huzuni, mathalani ikiwa ni hisia za huzuni, chuki na hasira zinapozuiwa zinakua hivyo upo wakati unafika ambapo njia nyingine za hatari hutumika na wananchi kuelezea hayo kwa viongozi wao. Hayo yakitumika gharama yake kwa taifa ni kubwa sana, nadhani ni wakati muafaka serikali itafute suluhu ya matatizo ya wananchi wake na sio kwenda kufanya kichaka cha kujifichia sheria wanazoweza kuzitunga!

Nashauri serikali ipime na ione inafanya hayo kwa faida ya nani kama ni kisiasa au ni kuwakomoa wananchi? Na je wamepima madhara ya baadae kwa Taifa letu?

 
Maandamano ni kupotezeana muda tu, na wakati mwingine huleta madhara yasiyo ya lazima.
 
Maandamano ni njia nzuri ya kukusanya fedha za M4C.
 
Maandamano ni uhuru wa watu au kundi la watu kueleza hisia zao kwa watu au kundi la watu wengine. Ni haki ya mtu au watu kutoa maoni yao. Kuzuia maandamano ni kuvunja haki ya msingi ya watu au kundi la watu katika kueleza hisia zao, iwe ni kuunga mkono au kupinga jambo fulani. Kuzuia maandamano ni sawa na kuzuia maji ya mto kwa viganja vya mkono. Maji lazima yatafute njia nyingine ya kupita. Sielewi kama serikali inajua kuwa watu wakizuiliwa kueleza hisia zao kwa maandamano watatafuta njia nyingine ya kufikisha hisia zao, na njia hiyo yaweza kuwa mbaya zaidi kuliko ile ya maandamano. Wakati huu ni wakati wa Kizazi cha digital, sisi wazee wa wakati wa kizazi cha analogia tusipokubali mabadiliko, tutaishia kuzua balaa.
 
Sikuwahi kuwaza kama hata wabunge wetu na mawaziri hawaijui katiba katiba kiasi hiki maana ni mtu asiyeijua katiba tu ndo anayeweza kutamka ----- huu wa kutunga sheria ya kuzuia maandamano.
 
Sasa serikali inataka watanzania wote wawe na maamuzi kama ya wakazi wa NEWALA kwamba mkiwa na hasira mzimalizie kwenye mali za viongozi. Unapomuona mtu amezidiwa na hasira ni vyema umuache alie sana machozi yakiisha na hasira zimepungua, lakini ukimzuia kulia njia nyingine yoyote mbadala atakayochagua kupunguza hasira zake itakuwa na madhala makubwa sana.
 
Sidhani kama wanaweza kutunga sheria ya kuzuia maandamano bila kuwa specific, labda walete sheria ya kupinga maandamano yanayoandaliwa na Vyama vya upinzani dhidi ya Serikali vinginevyo itakuwa ngumu maana kuna maandamano ya aina kibao kama vile maandamano ya kupongeza jambo, maandamano ya kusheherekea uhuru n.k
 
sikuwahi kuwaza kama hata wabunge wetu na mawaziri hawaijui katiba katiba kiasi hiki maana ni mtu asiyeijua katiba tu ndo anayeweza kutamka ----- huu wa kutunga sheria ya kuzuia maandamano.

nani alikuja na hilo wazo?kuna haja kubwa ya kumfahamu huyu mtu.kuzuia maandamano???duuh.TUTAFUTE CV YAKE.
 
Sidhani kama wanaweza kutunga sheria ya kuzuia maandamano bila kuwa specific, labda walete sheria ya kupinga maandamano yanayoandaliwa na Vyama vya upinzani dhidi ya Serikali vinginevyo itakuwa ngumu maana kuna maandamano ya aina kibao kama vile maandamano ya kupongeza jambo, maandamano ya kusheherekea uhuru n.k

Unajua ndugu yangu hii amri au mswaada unaodhaniwa uletwe kuwa sheria na serikali kuhusu maandamano utakuwa umelenga hasa SIASA sababu walioleta hiyo kadhia nao ni wanasiasa..na MLENGWA mkuu ni VYAMA vya siasa hasa hasa vile vinavyoonyesha threat kwa Chama Chetu plus WANAHARAKATI ambao wanaikosoa Serikali SIKIVU..vinginevyo kusingekuwa na upuuzi wa kufikiria kukataza maandamano...

Nawasilisha
 
Maandamano ni kupotezeana muda tu, na wakati mwingine huleta madhara yasiyo ya lazima.

Kwani kuna anaeweza kumlazimisha mtu akaandamane? Tusizuie freedom of expression pale ambapo mtu hana namna nyingine
 
nani alikuja na hilo wazo?kuna haja kubwa ya kumfahamu huyu mtu.kuzuia maandamano???duuh.TUTAFUTE CV YAKE.

Kama ni Nchimbi au Mtu mwingine ( japo tetesi zinasema ni wazo La Nchimbi mwenyewe ) akamatwe sasa hivi , kuzuia Maandamano ni uchochezi na wala hakuna mwenye uwezo huo , Tutaandamana kupinga muswada huo !
 
Kama ni Nchimbi au Mtu mwingine ( japo tetesi zinasema ni wazo La Nchimbi mwenyewe ) akamatwe sasa hivi , kuzuia Maandamano ni uchochezi na wala hakuna mwenye uwezo huo , Tutaandamana kupinga muswada huo !



Anae ona maandamano ni kupoteza muda aendelee na shughuli zake. Sisi tutaandamana kufikisha ujumbe tutakaoona unatakiwa kupelekwa lakini hakuna namna ya kuufikisha, hapo tutaandamana. Watanzania wako tayari kuandamana huyo anae taka kuleta sheria ya kupinga maandamano ajichunguze yeye na familia yake kama zimo zote huko kichwani.
 
Kwa nini tukajadili Uongo???! Serikali imependeza kuwa inaangalia uwezekano wa kupendeleza kwamba maandamano yawe na utaratibu mzuri!!!! Sijui Kama hiyo Ina maana kupiga marufuku maandamano. Na ieleweke Bunge ndilo linalotunga sheria.
 
ccm inaogopa kivuli chake hukimbia huku na kule wakijua kivuli wamekiacha mbali watulie wasubri 2015 si mbali.
 
Maandamano ni njia nzuri ya kukusanya fedha za M4C.

946736_496190513767878_1919287762_n.jpg
 
Back
Top Bottom