Ni maajabu au? Mwanamke kupata MP wakati ana mimba ya miezi 4??

SAWEBOY

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
241
173
Wapendwa Wana Jf,

Nina Mke wangu ambae ana mtoto wa miezi 8. Mke wangu huyu baada ya kupata huyu mtoto alini-surprise pale aliponiambia ana mimba. Nilipomuhoji imekuaje ashike mimba hali mtoto ni mdogo aliniambia hata yeye ameshangaa coz hakupanga ila ni bahati mbaya.

Nikawa namashaka kuwa mimba sio yangu.....akalia nakusema ni yangu. Nikasema ok poa aiche na wala asitoe lakini amwachishe mtoto kunyonya. Nikaandaa utaratibu mzuri wa kumhudumia mtoto. Miezi 2 baadae nikabaini kuwa ana mahusiano na mwanamme wa nje, nikamhoji akakataa. Nikamwambia ukweli utajulikana baada ya mtoto kuzaliwa kama ni wangu au hapana. Akataka kwenda kutoa mimba nikamkatalia.

Wiki Iliyopita nilisafiri kwenda arusha kwa dahrura...siku ya jumamosi, nimerudi home J4 usiku bila taarifa.......nimeshinda J5 tu , Alhamisi usiku huyu mwanamke ananiambia mvua imeanza kunyesha toka mchana. Mhmh sikumuelewa, na sikuamini asemacho.

FIKRA ZANGU:
1. Nahisi amemeza madawa ya kutoa mimba ili kufuta ushahidi wa kuwa mimba ni ya jamaa.
2. Sina knowledge kuwa mwanamke anaweza pata siku zake huku angaliana mimba hata ya miezi minne(4).
3. Naona mtoto wangu atakuwa hajatendewa haki kama ikiwa kweli ametoa hiyo mimba na mtoto
ameachishwa kunyonya akiwa na miezi 7 tu.

OMBI:

Naomba ushauri wenu juu ya doubt zangu hapo juu wapendwa wangu.

Asanteni sana na kazi njema.
 
SawBoy,
Kwanza pole sana kwa mkasa. Ingawa unaona tatizo ni mimba na mtoto anayenyonya nina wasi wasi kuwa tatizo ni kubwa kuliko unavyodhani. Tufanye nadharia tu kuwa alishika mimba isiyo yako, hapo utaona kuwa alikusaliti kindoa na kuwa na mahusiano na mtu ambaye hakutumia kinga!!mh

Pili, suala la kupanga uzazi ni la wazazi wawili na wewe kumuachia aliangalie peke yake ni kosa. Ulipaswa kumsadia kujua ni wapi na lini muepeuke ili kumpa mtoto nafasi ya kunyonya na kukua.

Tatu, kunyonyesha peke yake haijawa kinga ya mimba. Zipo nadharia 'literature' zinazoonyesha kuwa uwezekano wa kushika mimba unapungua wakati wa kumyonyesha, hii haina maana kuwa uwezekano haupo.

Nne, katika mazingira fulani mwanamke anaweza kupata hedhi akiwa na mimba. Hedhi hiyo inaweza kuwa ni ndogo na si full masika. Hiyo isichukuliwe kama ni kawaida ingawa huwa inatokea 'spots'.
Ikitokea ni vema kumuona daktari kwani kuna kitu hakipo sawa.

Tano, kama amefanya jaribio la kutoa hiyo mimba ya miezi minne, ukweli ni kuwa ni kubwa ya kutosha na katika mazingira ya kawaida kungekuwa na kasheshe lililoambatana na hilo.
Lakini pia inaweza kuwa ametua mzigo kwa njia 'mbadala' na kinachobaki na unachokiona si masika ya kawaida bali yatokanayo na vurugu zilizotendeka.

Ushauri: nendeni hospitali mkapate majibu ya tatizo.
Kwa wakati huu jifikirie wewe na mtoto aliyepo kwanza. Katika nyakati hizi mashaka si jambo la bahati nasibu tena.
 
Ndoa nyingine ni ngumu sana hasa pale mwanamke anapokuwa na bwana nje!!! Si kawaida sana!! Yaani ninavyoona akina mama busy na watoto wao wadogo inakuwaje wengine wana nafasi ya vidumu nje? Huyu mke atakuwa lishakubuhu kabla hujamuoa. Pole sana mkuu.
 
Daah,
Mko wachache sana wenye roho kama yako...
Alaf inaonekana unamwoga uyo mkeo...Preliminary iyo Mimba ishapigwa chini coz tunajua How miscarriage hurts..
Baada ya kusikia izo taarifa umechukua hatua gani ?? Kama mimba imetoka lazima akasafishwe ..je amekushirikisha ??
Vijana washatia makono kapu lako,amka

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hilo la kupata period wakati ana ujauzito wala sio geni manake hutokea kwa baadhi ya watu ila mimba huwa haitoki bali inapungua tu na kuna jinsi anaweza shauriwa na wataalamu ili kuzuia mimba isitoke kabisa! Kwa suala la mkeo inabidi muende hospitali kucheki kama mimba iko kweli au ameitoa.........kama haipo ujue ushawahiwa kaka!
 
Duh!! ki-ukweli hii haijakaa vizuri kabisa. Nakushauri mwende nae hospitali kwa vipimo zaidi ili kubaini kilichotokea then fanya uamuzi ambao ni sahihi kwa future ya familia yako.
 
We kijana kweli hazikutoshi kwanza vipi unaishi na mwanamke ambaye humuamini?

Pili wako wanawake wanakuwa napata period na huku bado wana mimba, inategemea inawezekana mimba imeotea nje ya mfuko wa uzazi, na kuna mambo mengi tu wako wengine wanapata period mpaa wanazaa kila mwanamke na uzazi wake.
 
Nawashukuruni sana wapendwa wangu kwa michango yenu, tupo pamoja and I am reading your comments between the lines....so thank you so much for your comments.
 
kweli ishini na wake zenu kwa akili...........................................lol:shetani::shetani::shetani:
 
Hebu nenda hospitali usiandikie mate..mengine yatafuata au kama vipi urudi tena jamvini!
 
Mungu tunusuru na hizi dhambi jamani!hizi ndoa sasa hivi zina nini?huyo binti mbona sjui nimweke kundi gani?mtoto wa miezi 8 yet unaenda kugawa kipochi manyoya nje na kubeba mimba nyingine?!
 
Una hakika gani kama huyo anayenyonya ni mtoto wako mpaka uwe unahamaki kakoseshwa haki yake ya kunyonya miaka 2?
 
Wewe ulijua mkeo ana mtoto mchanga lakini bado ukawa unakula mavitus ulitegemea nini? kama ungekuwa hutaki apate mimba ungekwepa kabla hujatafuna, ungekwenda na tarehe zao kuingia mwezini (mawinguni) kama unahofu kuwa mkeo anakwenda nje hizo ni hisia potofu unao ushahidi? kama unao ushahidi basi inaonyesha hajaanza leo hata huyo mtoto wa kwanza pia ana walakini amua moja jione kama mkeo ni mwaminifu haendi nje, mpaka pale utakapokuwa na ushahidi kamili, kama bado unamashaka kuna D. N. A itakupa majibu

Wapendwa Wana Jf,

Nina Mke wangu ambae ana mtoto wa miezi 8. Mke wangu huyu baada ya kupata huyu mtoto alini-surprise pale aliponiambia ana mimba. Nilipomuhoji imekuaje ashike mimba hali mtoto ni mdogo aliniambia hata yeye ameshangaa coz hakupanga ila ni bahati mbaya.

Nikawa namashaka kuwa mimba sio yangu.....akalia nakusema ni yangu. Nikasema ok poa aiche na wala asitoe lakini amwachishe mtoto kunyonya. Nikaandaa utaratibu mzuri wa kumhudumia mtoto. Miezi 2 baadae nikabaini kuwa ana mahusiano na mwanamme wa nje, nikamhoji akakataa. Nikamwambia ukweli utajulikana baada ya mtoto kuzaliwa kama ni wangu au hapana. Akataka kwenda kutoa mimba nikamkatalia.

Wiki Iliyopita nilisafiri kwenda arusha kwa dahrura...siku ya jumamosi, nimerudi home J4 usiku bila taarifa.......nimeshinda J5 tu , Alhamisi usiku huyu mwanamke ananiambia mvua imeanza kunyesha toka mchana. Mhmh sikumuelewa, na sikuamini asemacho.

FIKRA ZANGU:
1. Nahisi amemeza madawa ya kutoa mimba ili kufuta ushahidi wa kuwa mimba ni ya jamaa.
2. Sina knowledge kuwa mwanamke anaweza pata siku zake huku angaliana mimba hata ya miezi minne(4).
3. Naona mtoto wangu atakuwa hajatendewa haki kama ikiwa kweli ametoa hiyo mimba na mtoto
ameachishwa kunyonya akiwa na miezi 7 tu.

OMBI:

Naomba ushauri wenu juu ya doubt zangu hapo juu wapendwa wangu.

Asanteni sana na kazi njema.
 
Mkuu huyo binti atakuwa ashatoa mimba hiyo, kwa nijuavyo mtu mwenye mimba ya miezi minne hupata spots tu za damu na sio mafuriko ya muda mrefu.
Hata huko hospitalini huwa tunaambiwa ukiona damu inatoka na umjamzito ni dalili hatari ya mimba kutishia kutoka au ishatoka.
Mpeleke hospitali upate majibu kamili haraka sana iwezekanavyo, na kama ametoa hiyo mimba huyo hafai kuwa mke (sio kwamba muachane ila hafai sababu atakuletea mtoto mwingine wa nje na kutoa cz ashazoea hiyo tabia).
 
Pole ndugu

usifikirie vibaya kabla hujahakikisha

huwa kuna kitu wanaita force bleeding.

Huwa ionaweza kutokea kwa mama mjamzito ila huwa haina harufu kama bleeding ya kawaida

mpeleke hospitali ili kama ni msaada ukaupate huko,

usimhukumu mkeo kwa mambo yanayohitaji utaalamu ambao wewe huna
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom