Ni Lini Utatulia?

Ni Lini Utatulia?

Radium

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2022
Posts
490
Reaction score
871
Wakati muafaka wa kutulia katika mahusiano(Ndoa) ilikuwa ni pale ambapo mwanaume ameshaweka akiba ya kutosha au anamsingi mzuri wa uchumi kama kazi nzuri au biashara yakueleweka.
Mambo ya mahaba yakapamba moto ikawa kwamba ili muweze kuwa na mahusiano imara basi wawili nyinyi muwe mnapendana vibaya mno
Itoshe kusema kwamba hizi criteria zote sasa zimeshapitwa na wakati.

#Hivi ni vigezo muhimu kwa sasa vitakavyoashiria kuwa sasa unaweza kuwa na mahusiano imara na yakaweza kuwa ya kudumu.

#1.Achana na ukamilifu.

Wakati wa kukituliza ni pale utakapo kubali kuwa mwenzako yuko deeply imperfect. Ana mamia ya kasoro na madhaifu. Anakera kwa kila hali hawezi vitu kibao na hakaribii kabisa kufania kuwa yeye ndie Mungu amekupangia. Tukiangalia upande wa saikolojia yake tutakuta ni muozo wenye fetish na phobia na trauma ambazo hazivumiliki kiasi kwamba ni vigumu sana kuishi nao.
Ila mwisho ni lazima tugeneralize kwamba kila mmoja hivyo ndo alivyo. Punde tu utakapo ingia ndani ya hicho kiumbe kichangamfu na kipole kwa pamoja ambacho kinaukonga moyo wako ni lazima ukutane na ubovu usiovumilika.
So chakufanya ishi na huo upande wa furaha na huo wa kasoro uvumilie tu maana kama ni kubadilisha basi utaimaliza dunia usiijue rangi ya kile unachokitaka.

WE'RE FUNDAMENTALLY FLAWED SPECIE

#2.Kubali kuwa hautaeleweka kwa kila kitu.

Tunavyojua ni kuwa upendo ni kueleweka na kukubalika kwa kila sehemu ambayo ipo ndani akili zetu, sehemu tunazozifanya kuwa siri na matamanio ambayo tunatamani mwenzetu azielewe na kuzifeed.
Kuwa tayari kutulia ndani ni kukubali kuwa haitojalosha tunaeleweka kwa kiasi gani menzi wetu hawatoweza kamwe kuziba kila hitaji la nafsi zetu.

Pia haitojalisha tutatafuta kwa kiasi gani hatotokea wa kuturidhisha kwa kila nyanja ya matamanio yetu.
Hakuna mwanadamu anayeweza kumuelewa na hivyo kuweza kubond kwa 100% na binadamu mwingine.

#3.Jitambue kuwa una wendawazimu ndani yako.

Ni rahisi kujiterm kama mtu ambaye umrahisi kuwasiliana naye kutengeneza ukaribu na msikivu.
Ila ni wakati wa kuoa/kuolewa sasa unapojitambua ni kwa kiasi gani wewe ni garasa.
Unahasira za karibu.
Mgumu kusikia ushauri.
Mtu wa majuto.
Mbishi na kwa wakati tofauti mwenye dharau.

Umekua mkubwa vya kutosha kutulia ndani utakapo shikwa na aibu ukijifikiria kuwa wewe ni nani na tabia zako kisha ukawa tayari kabisa kijishusha na kutaka radhi kwa mwenzako pale utakapoonyesha ugarasa na uhovyo wako.

#4. Acha kukomalia upendwe, Anza wewe kupenda.

Tunasema ni rahisi kuwa na mtu unayejua anakupenda kuliko kuwa na yule unayejua unampenda.
Ila tunajisahau mno kwa kutafuta kupendwa na kuuchunguza upendo wa wenza wetu kwetu zaidi ya sisi kuonyesha upendo wetu kwao.

Upo tayari kuingia kwenye ndoa isiyo utapeli au gereza pale utakapo kuwa tayari kuushika usukani wa shughuli ambayo hatujaizoea, shughuli ya kumuonesha upendo mwenza wako bila kudai kuoneshwa upendo.

Wewe si wakulaumiwa kwa hali hii kwa sababu bila hatia ujuzi wa kupokea mapenzi bila ya kuonesha mapenzi tuliupata kutoka kwa wazazi wetu.
Tukiwa watoto kazi yetu ilikuwa moja ti, KUWEPO basi.! Mengine yoote walifanya wazazi umekula? Uansikia joto au baridi, unataka kuangalia chaneli gani mpaka ikawa tunalia tukiwa tunataka halafu wao waotee ninini kinatusumbua. Hayo yote sisi hatukujali ni kiasi gani wameuma ndimi zao ili wasitutolee chafu. Tuliwachosha kiasi cha kuona uvivu mpaka kuvua viatu ili wapumzike.
Hiki ndo chanzo kikubwa unapomsikia mtu mzima akisema anataka upendo anachomaanisha ni kuwa anataka kupendwa na sio kupendana achilia mbali kupenda.

Hili kiasili ni janga. Kudumisha uhusiano inabidi kila mmoja aweke mbaili dhima ya mtoto na aicheze nafasi ya mzazi.

#5Jiandae kwa utawala.
Tatizo jengine ni kuwa tunaona kama mahusiano ni suala la mahaba na hisia hisia pekee ila kinachofanyika ndoani ni kama kuendesha kijibiashara fulani. Wawili nyie itabidi msafishe ,mpike mlipe bills ,mpange bajeti na muitrack, mlee na mfanye vikao kwa mazungumzo ya kina kuonyana na kupongezana....ila hakuna kusimamishana kazi kwasababu kampuni kibali chake ni nyinyi wawili.
Pia ujiandae kuwa hakuna miongoni mwa shughuli za kiutawala itakayokuwa ya kufurahisha over time. Ila ni shughuli za muhimu mno katika kuutunza uhusiano na ndio msingi tegemevu wa kampuni yenu.

#6. Jiandae kujifunza.
Kuna imani kuwa kupendwa kunamaanisha kukubalika kwa jinsi tulivyo na hivyo hakuna mtu kutaka ubadilike kwa namna yeyote. Lakini jua tu ni lazima atakutaka ubadilike na unajua ana haki ya kufanya hivyo. Kwa sababu kwa kiasi kikubwa umkosefu mwenye mapungufu na unahitaji kula bapa la pasi ili unyooke.
Unaweza kama anakuvamia na ana uchu wa kukuendesha ubadilike tofauti na alivyo kukuta lakini upo tayari kutulia utakapokuwa tayari kukosolewa na kutajiwa kabisa sehemu ambazo u,kikwazo. Kwahiyo muone mwenzako kama mwalimu na wewe kama mwanafunzi and vise versa.
Ila kusiwe na upande unaotumia hasira.
Mahusiano yawe ni elimu ya kuwafanya watu wawili muwe wat bora zaidi ya kabla ya kuwa mke na mume. Na yasiwe eti ni kupendana kwa jinsi ulivyo mkuta mtu basi uridhike na matendo yake tu.

*Kwa idea hizi na akili kubwa kutumika tunaweza kurudi kwenye dunia ya zamani ambapo ndoa ilikuwa ni jambo la uhakika wa mwangaza la kudumu na lenye future ambayo iko realistic ndani yake.
 
Ujumbe mujarabu kwa tunaohangaika kutafuta pakutulia, changamoto ni kwamba unapata mtu unawaza "hapa sasa nitulie" kumbe nae anawaza "hapa sasa nijichetue" tafrani tu
 
Ujumbe mujarabu kwa tunaohangaika kutafuta pakutulia, changamoto ni kwamba unapata mtu unawaza "hapa sasa nitulie" kumbe nae anawaza "hapa sasa nijichetue" tafrani tu
Hawezi kusema akajichetue baada ya kuolewa mkuu. Kwani atakosa nini
 
Back
Top Bottom