Ni lini serikali itapanga vituo vya kazi kwa walimu wa sayansi na hisabati?

Twalyaninkomi

JF-Expert Member
Oct 31, 2016
265
259
Ni takribani zaidi ya mwezi sasa tangu serikali kupitia wizara ya elimu ilipotoa muongozo mpya wa kutoa ajira, ambapo walimu wahitajika ni wa sayansi na hisabati waliotakiwa kutuma vyeti vyao kwaajiri ya uhakiki na kupangwa vituo vya kazi rasmi! hata hivyo zoezi hili lilifanyika na kumalizika kwa muda wa siku tatu tu.

Licha ya shule zote nchi kufunguliwa tarehe 9 january, lakini mpaka sasa hakujatangazwa ajira hizo kwa walimu hawa wa sayansi na hisabati wenye umuhimu mkubwa hasa katika kipindi hiki nchi ikielekea katika uchumi wa viwanda, pia kulingana na uhaba katika shule zetu za kata hasa za vijijini!

Ni lini serkali itatoa majina ya vituo vya kazi kwa walimu wa sayansi?
 
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu!

Kwaiyo umejiona wewe wa sayansi na hisabati ndio unaumuhim zaidi ya mwalimu wa sanaa?

Kwa hii serkali mnatakiwa muungane pamoja mpiganie haki yenu, kwani serkali haina mpango wowote wa kuajiri! Hayo matamko sijui wanaajiei wanasayansi ni siasa tu wanasukuma muda
 
Alisema Engineer Manyanya kuwa kazi ya wizara yake sio kuajiri walimu, ila ni kuhakiki tu vyeti vya hao Walimu na kisha kupeleka majina yao kwenye ofisi ya Rais utumishi wa uma ndio yenye jukumu la kuajiri na tayari wameshafanya hivyo labda tusubiri Kairuki atatangaza lini
 
walimu wa sanaa wamepoa sana na wamekata tamaa kabisa, ngumu kuwarudisha kwenye morali
 
Alisema Engineer Manyanya kuwa kazi ya wizara yake sio kuajiri walimu, ila ni kuhakiki tu vyeti vya hao Walimu na kisha kupeleka majina yao kwenye ofisi ya Rais utumishi wa uma ndio yenye jukumu la kuajiri na tayari wameshafanya hivyo labda tusubiri Kairuki atatangaza lini
hapo penye lini ndio shida! na muda unakimbia sana
 
Ajira zitolewe kwa wote!
Kwani nyie wa sayansi mtafundisha lugha?
Walimu wa sanaa bado wanahitaji na wanaumuhim mkubwa
 
Ni takribani zaidi ya mwezi sasa tangu serikali kupitia wizara ya elimu ilipotoa muongozo mpya wa kutoa ajira, ambapo walimu wahitajika ni wa sayansi na hisabati waliotakiwa kutuma vyeti vyao kwaajiri ya uhakiki na kupangwa vituo vya kazi rasmi! hata hivyo zoezi hili lilifanyika na kumalizika kwa muda wa siku tatu tu.

Licha ya shule zote nchi kufunguliwa tarehe 9 january, lakini mpaka sasa hakujatangazwa ajira hizo kwa walimu hawa wa sayansi na hisabati wenye umuhimu mkubwa hasa katika kipindi hiki nchi ikielekea katika uchumi wa viwanda, pia kulingana na uhaba katika shule zetu za kata hasa za vijijini!

Ni lini serkali itatoa majina ya vituo vya kazi kwa walimu wa sayansi?
Muwe na subira kuhusu ajira zenu Mara taratibu zkikamilika zitatolewa
 
Bora ya nyie mnasubiri kupangiwa wenzenu hakuna kabisa na hawajui wala hata waziri mwenye dhamana haongelei
 
Back
Top Bottom