Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,311
- 38,448
kwa kweli kinachoendelea huko Pemba kwa kuonekana kuranda randa kwa magari ya deraya na maroli yaliyosheheni Askari Polisi na wanajeshi bila shaka hari ya kwenye visiwani hivyo imevuka mipaka ya kudhibitiwa kwa nguvu ya Polisi wa kawaida.
Lakini Askari hao hasa wa jeshi la wananchi na vifaru vyao wanaoonekana huko Pemba ni lazima kwanza waruhusiwe na Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi kuwa mitaani baada ya yeye kujiridhisha kwamba ulinzi wa kawaida kwa kutumia Askari Polisi umeshindikana. Jee magufuli kama Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania aliwahi mahala popote kuwaambia watanzania kwamba sehemu moja ya nchi yao usalama wake ni tete na unahitaji jeshi la wananchi kuingia?
Ni lazima tuwe na Katiba inayoweka mipaka kwa wanasiasa kuyatumia majeshi yetu kwa manufaa yao ya kisiasa. Ni haki kweli kuwa na vifaru kwenye mitaa ya nchi yako kama vile kuna vita dhidi ya raia unaowaongoza?