ABEL MAGEMBE LUGIMBA
Member
- May 22, 2016
- 63
- 59
NI LINI EDWARD LOWASSA AMETEULIWA NA KUTHIBITISHWA KUWA MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA?
Kwa siku za karibuni, Waziri Mkuu aliyeshinikizwa kujiuzulu kwa kashfa ya Richmond na aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA na Mwamvuli wa UKAWA, EDWARD LOWASA amekuwa anatambulishwa kama Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA. Sote tunafahamu kuwa aliyeteuliwa rasmi na kupitishwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ni Frederick Sumaye. Ni Sumaye ndiye tulitangaziwa na taarifa zake kusambazwa kwenye media ikiwemo social Media kuwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA.
Hata hivyo, hakuna ushahidi wa dhahiri shahiri wa kuthibitisha juu ya Lowasa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu. Je uamuzi huo umefanyika gizani na kimya kimya? Au kwa uamuzi wake tu wa kukinunua chama na kugombea Urais ndo unamfanya awe Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA? Je kuna ushahidi wowote juu ya Lowasa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA?.
Maswali haya yalipaswa kuulizwa na wana CHADEMA wenyewe ila kwa vile uwezo wao ni mdogo, hili hawajaliona na ndo maana wamekaa kimya.