Ni lazima CCM ing'oke 2015! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni lazima CCM ing'oke 2015!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by andrews, Mar 28, 2012.

 1. a

  andrews JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  katika viongozi wakuu wa tanzania imeonyesha wazi ni nyerere na mwinyi waliokuwa waadilifu tu.nyerere na mawaziri wake 90% walikuwa wanatumikia taifa. Hapa hakuna mjadala,vijiji vya ujamaa elimu kwa wote, matibabu kwa wote nyerere aliwaweka watoto wake kwenye shule za watanzania,walilala kwenye magodoro,na kuliwa na mbu kula maharage kama wengine,wakiwemo watoto wa kawawa,aboud jumbe, sokoine msuya hapa hakuna ubishi.

  Ukimuona mzee Mwinyi hakuwa na makuu hakuwa mdini,wala mkabila hakuwadharau maskini.mawaziri wake wakuu wote walikuwa waadilifu na si mafisadi angalia mzee msuya,mzee wariyoba walitumikia taifa kwa moyo mmoja.

  Umoja wetu, mshikamano ulikuwa madhubuti pamoja na utendaji wa mawaziri wao wote asilimia kubwa hawakuwa mabinafsi.

  Akaingia fisadi MKAPA huyu ni kiongozi aliyekuwa mbabe kwa kujifanya anakusanya kodi na kuwa na salio serikalini, lakini lengo kubwa ilikuwa ni kuzichota zoote kwa kisingizio nilizikusanya mimi, msomi huyu kauza majengo yote ya watumishi wa serikali,walipeana kusudi wasimuhoji akitoka madarakani na mpaka leo hajaulizwa. WAZIRI mkuu wake alijilimbikizia ardhi utafikiri anamiliki mifugo yote nchini,huyu nae angekuwa muadilifu angezuia kabisa kuuza nyumba alizoacha mjerumani kwa ajiri ya serikari,MKAPA na genge lake la wahuni waliuziana rasilimali zote waliokuwa madarakani akawafungua macho mapapa wana mtandao. Hapa serikali yake haikuwa na uadilifu hata kidogo ilikuwa ya majizi yote.

  SMILLING BOY alipoingia huyu akaahidi kwa macho na masikio yangu tutazirudisha nyumba za serikari mpaka kesho, tutarekebisha mikataba mibovu ya madini.matokeo yake vinazidi kujengwa viwanja vya ndege kwenye machimbo yote hakuna uhakiki wa hili.

  Watanzania wote wamechoka na serikari yao na hata watumishi wite hawaitaki serikali isiyokuwa na kiongozi(eti kuna kiongozi tanzania?)tunashuhudia majengo ya kifahari kama ya spika ili apitishe agenda zao bungeni bila kujali wapiga kura.Kuna wakati makaburu waliapa kuwa mweusi hataongoza nchi ile mpaka wazungu wote wameisha 1985 MANDELA akawa raisi, walimfunga na kuuwa wengine kusudi kuuwa umoja wa weusi.

  USA mweusi akawa rais kuna wabaguzi waliombeza Martin Luther King kuwa ana wazimu lakini Obama leo rais.

  WOGA waliokuwa nao ccm ni kuhojiwa kwa ufedhuri ufisadi unyama walio nao kwa raia wao. Sheria wanazoziweka kukandamiza upinzani zitawasurubu wao wenyewe.NYERERE alisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.siku hadi tunashuhudia bendera na wabunge waupinzani ukiongezeka kwa kasi na vijana ambao kwa ccm ni taifa la kesho kwa vyama nya upinzani ni ngao ya leo hakuna tena umoja wa vijana kuna vibaraka wa mafisadi.

  Tutakachoshuhudia 2015 ni anguko ambalo hawatategemea sababu wajinga na mbumbu waliokuwa wakiwapa kanga,kofia pilau wamechoka, wanalala gizani wakati wabunge wao wana majereta,wanafia muhimbili wakati wake zao wanaenda ulaya kufanyiwa massage. Enough is Enough. Wakati wa kuendesha mashangingi wakati taifa ni maskini safari za rais kama John walker semina warsha kongamano na upuuzi vifikie mwisho.

  GADAF aliondoka,mubarak aliondoka viongozi waliokuwa na mabafu ya dhahabu. Zambia, Senegal, wameweza bila kumwaga damu,Ivory Coast waliamua,KENYA wamebadili katiba. Sasa Tanzania tunataka kiongozi kama akina NYERERE, SALEEM, MWINYI, WARIOBA, KAWAWA, MSUYA NA SOKOINE NA SI MKAPA, SUMAYE, KIKWETE NA PINDA.

  Tunataka wazalendo na si wanafiki na mafisadi.

  INSHALAH
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  washangaa sana viongozi wa CCM wanashindwa kuongoza nchi hii wakati kilakitu kimewekwa wazi hakuna taabu kabisa una lala ukiamka unatembelea JF Basi unajua cha kufanya hiki ni kisima cha fikra watu wanafikiri kwa kina na wanajua nini kifanyike leo kesho na baada ya kesho,thanx Comrade japo next time zingatia kanuni za uandishi wa insha kidogo
   
 3. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nchi ilishauzwa long time
   
 4. a

  andrews JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ridhiwan kikwete furahia matunda ya baba yako leo hii utahukumiwa kama wato wa mabutu,amin gadaf,za mwizi arobaini hivi wama pale ikulu nanai analipa umeme na misafara ya salma kikwete na aliwaambia nchi inaongozwa na mke na mume
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  too far to say now.
   
 6. s

  sangija Senior Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  polepole ipo siku kitaeleweka tu!!! na lazima tuwe sisi wala tusimtegemee mtu kutoka nje aje atusaidie!! pamoja tunaweza sana ni maamuzi tu.Inauma sana!!
   
 7. a

  andrews JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtu kama shayo huyo tulikuwa tunailaani wote ccm kumbe yeye ni njaa inamsumbua chuo kikuu alichokuwa anafundisha ndicho chuo kinachoongoza kwa kuwa na matikeo hafifu ni dr wa nini huyo is too late shayo
  huambulii chochote ccm
   
 8. a

  andrews JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Utafiti unaonyesha viongozi wengi wa ccm ni waathika ndio maana hawajali vijana wala watanzania ndio maana maamuzu yao hayaingii akilini kuna haja ya kupima afya za wagombea wote wa ubunge na watumishi wa serikari is soo sad
   
 9. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 792
  Trophy Points: 280
  Nimejikuta nikitokwa na machozi baada ya kumaliza kusoma uzi huu, kura yako na yangu ndizo zitakazo ikomboa tanzania.
   
 10. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  TRA wamepewa risiti ya kuuzwa Tanzania. Au nani ana risiti ili tuwe na uhakika kwamba TZ imeuzwa.
   
 11. J

  JacksonMichael JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu fuatilia taarifa baada ya kuuwawa Gadafi, nchi imegawanyika vipande vipande, soma RT.COM zaidi ya 50 leo hii wamekufa kwenye vita vya kikabila, waliovamia wanajichukulia mafuta kama hawana akili nzuri, wazungu sasa wanalinda mafuta tu na sehemu za kuyatolea. hakuna central command any more. watu wamekata tamaa sasa libya ambayo watu walinufaika sana kipindi cha gadafi. Hakuna chombo chochote cha magharibi kinareport kuhusu libya anymore kwa kuwa walichokifuata (OIL) wamekipata.
   
 12. Typhoid

  Typhoid JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  So what next?
   
 13. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Kama CCM itaendelea kuwa madarakani 2015 nahaidi kuandaa mpango wa kuingia msituni kuipigania nchi yangu na damu yangu itahesabiwa haki pale ntakapokufa,nimechoka mpaka maini yamechoka,nahisi cna vision katika nchi ya hivi,ukila unashangaa wenzako wanalala njaa,wengine wanapelekwa ulaya wengine wanafia majumbani kwa kukosa panadol,wengine wanawasha ebimuri kupata moto na nyumba zao zinawaka mioto wengine wana umeme ili tu watoto wacheze gemu,hawalali usiku kucha wakikwepa matone ya mvua kwenye mabanda yao wengine wanalala kwenye mabangalo mfano wa kasri na mapiramid ya farao,umesoma cha ajabu unataabika zaidi ya mbeba taka pale kariakoo...what's bright life my comrades?

  Kwa haya wakuu sina jinsi zaidi ya kuitoa nafsi,ni bora ukafa kwa kudai usawa hata Mungu atakubali kufa kwako kuliko kuishi katika adha kiasi hiki huku umekondeana kama mbwa wa wawindaji

  I must die and I will die!
   
 14. K

  Koffie JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 403
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bora ufe wajinga wapungue duniani
   
 15. OJ7 Da Hustler

  OJ7 Da Hustler New Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nmeshkwa na simanzi sana baada ya kusoma kilio hiki cha mtanzania ambaye amechoka na uongozi mbovu wa watu waliofoji vyeti vyao vya elimu ili wawanyonye watz mil 41.............jaman sisi kama watz,japo hawa mafisadi wamekosa uzalendo basi tujitahidi kuwa wazalendo na wenye mshikamano ndio tutaweza kuleta mabadiliko!!!!! Jamani we have to know that"Winners are people who have taken meaningful actions,not just thought about the things they want to do"kwa hiyo sisi tupigane kiume mpaka waondoke hawa mafisadi wakubwa...............................................
   
 16. K

  Koffie JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 403
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bro acheni kuingizana mkenge,, hakuna wa kupigana hapa, Ni walewale wa kyubwabwaja kwenye mtandao tu. Nendeni field mkaone moto uko vipi. Tundelee na umbea humu.
   
 17. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kazi bado ni kubwa mbele kwa Tanzania upinzani kuchukua nchi.

  Chama cha magamba wana mbinu mbaya mno - kwanza kuua yeyote anayewakosoa au kuwapinga.

  Ushahidi unayo, sina haja ya kusema zaidi, Kolimba, Kombe, Sokoine, Nyerere

  Pia Kununua wanachama wa upinzani na kuwafanya vibaraka wa kuvuruga vyama.

  tayari NCCR, Sasa CUF.

  Watanzania tumebaki na CDM ambayo ni Tumaini letu.

  Hata hivyo CDM haiko Salama, kuna chocko choko zinaanzishwa.

  Nawaomba Mbowe na Slaa (Viongozi wakuu) Muwe imara
   
 18. a

  andrews JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ikibidi damu kumwagika ni afadhari lakini tupambane ccm iondoke
  watoto wa mitaani wanaongezeka,ni matunda ya uongozi mbovu wa ccm,
  shule za kata bomu zote,mahospitalini hakuna dawa wenyewe na familia zao wanatibiwa ulay na india.makampuni ya kigeni yananyanyasa wazawa sababu wakubwa wameshapata 10%zao.mikataba mibovu yote ya ujenzi wa barabara zisizo na viwango viongozi wote kimya,uteuzi wa viongozi kutokana na ukanda (ukabila)na agenda za usiri za udini. Ccm inachangia kwa kiasi kikubwa kujenga udini wazi wazi na hii ni laana kwa mkapa na kikwete sababu tukija chinjana kizazi chote kitawahusisha na hilo.hivi ccm kusimama na kutumia bakwata kule igunga wanaona imani? Ccm kutumia makanisa arumeru ni sahihi tunasema ni heri tumwage damu kidogo wengi wakomboke kuliko utawala wa ccm unaotuuwa kila kukicha.viongozi wote wasiopenda kujirekebisha umma ndio unawatoa.mnahonga mabrigedia lakini washika bunduki ndugu zao wanakufa kila siku sabau yenu,polisi wa mitaani wana njaa mpaka utafikiri wana ukimwi ni matunda ya ccm.
  Sasa tuchapane kama kenya tuheshimiane.pamoja na kuchinjana rwanda kagame kafanikiwa kufuta ukabila na marafiki zake wa karibu mafisadi kawasweka ndani na hiyo ndiyo haki sawa kwa wote.
  Nguvu ya umma itawaodoa kweupe.
   
 19. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Hata wewe utakufa tu na ujinga wako pambaf kabisa wewe.
   
 20. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Ningekuwa na uwezo kama msajili wa vyama vya siasa ningeshaifuta CCM muda mrefu.CCM inanikera sana watanzania hatukutakiwa tuwe masikini kama tulivyo watanzania wengi tumepigika ili hali watu wachache wanaogelea kwenye utajiri na wamepata pesa kwa njia haramu.
   
Loading...