Ni kweli Tanroads inapangisha maeneo ya hifadhi ya barabara?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,409
13,260
Hivi karibuni Tanroads wamevunja majengo ya biashara na makazi yaliyokuwa katika hifadhi ya barabara maeneo ya Mbezi mwishio karibia na kituo cha daladala. Lakini hivi majuzi wamepita watu waliojitambulisha kuwa ni wafanyakazi wa Tanroads wakiwa na vizibao vyenje kuakisi mwanga na vitambulisho wakidai kuwa Tanroads imeamua kuwa kuanzia sasa haitavunja maeneo ya biashara ambayo haiyahitaji kwa wakati huo na badala yake wafanya biashara katika maeneo hayo watalazimika kulipia kodi kwa kulipia dola 2 kwa kila square metre au mita mraba.

Baada ya hapo wakaanza kupima maeneo na kama kawaida shughuli hiyo ikaanza kuvutia rushwa ambapo baadhi ya wafanyabiashara waliwahonga wapimaji ili watoe ukubwa mdogo wa maeneo yao ili kodi iwe ndogo. Hiyo ilikuwa ni mavuno kwa wapimaji ambapo walikuwa wanachukua kati ya laki 2 hadi 5 kulingana na eneo na ukubwa wa biashara

Kikubwa ambacho watu hawaelewi je ni kweli utaratibu huo upo na kama ulitangazwa au haukutangazwa kwani watu wanapigwa sana. Maana watu wamepigika lakini bado wanajihoji je ni kweli Tanroads wameamua kupangisha maeneo ya hifadhi ya barabara kwa muda na je ni nchi nzima au ni Dsm tu?
 
Tanroads watakupangisha Leo....kesho manispaa watakuja na Bill yao....I hope the line of demarcation on the open space and road reserve has been made clear now
 
Back
Top Bottom