KERO TANROADS, kwanini mnaruhusu watu kujenga kwenye hifadhi ya barabara? Mnaweka amri ya Katazo baada ya wiki ujenzi unaendelea

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna utaratibu wa TANROADS kuruhusu ujenzi wa majengo kwenye hifadhi ya barabara. Kuna ujenzi pia unaendelea kwenye hifadhi ya barabara za TARURA.

Wanachofanya nikuweka Katazo kwa lengo la wewe kufika ofisini kwao, ukifika unaongea nao kwa capital letter then wanakuambia kaendelee.

Watanzania wengi hasa wasio na upeo mkubwa wamekuwa wakiendelea na ujenzi bila kujua kwamba ipo siku watavunijiwa. Siku hao hao mamlaka za barabara zikija kuvunja tunaanza kulia kwa mawaziri sijui nimetumia pensheni yangu sijui nitaishije...kumbe ulitoa kitu kidogo upate kibali.

Nichukue fursa hii kuwataka wenye barabara wapitie majiji makubwa kuona vibanda na nyumba za biashara zinazojengwa kwenye hifadhi ya barabara.

Naongea kwa niaba ya wananchi waliowengi wanaotoa fedha waruhusiwe kujenga kwenye barabara.....you are wasting your capital

======
MREJESHO:

TANROADS wamejibu kuwa hawajawahi kuruhusu ujenzi kwenye maeneo ambao walishaweka zuio la ujenzi, wasema wananchi wawe makini ili wasijepata hasara ya kuvunjiwa kwa kujenga karibu na barabara.

Zaidi, soma: TANROADS: Hatujawahi kutoa ruhusa kwa watu kujenga kwenye hifadhi ya Barabara
 
Back
Top Bottom