Ni kweli Serikali imeamua kuwa kimya na kuendelea kutuumiza

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,441
Habari wanabodi

Nimeendelea kutafakari ya spika na wabunge wake huku nikisikiliza ya PM na watu wake huku waziri wa fedha, tume ya ushindani, waziri wa biashara na Rais wako kimya.

Nikiwa natafakari hayo, naambiwa kesho nauli za mabasi na daladala zinaanza kutekelezwa.

Spika naye kichwa maji mnajili hakuna azimio

Rais kichwa maji anaendelea kutia kuni kwenye jungu lilitoswa mikono ya mwanaye

Waziri wa nishati bogus kabisa huku tukimsamehe waziri wa fedha kwani hajielewi eti anapost sensa.

Ni bora tukahairisha sensa na fedha za sensa zikafidia hizo tozo ambazo kimsingi hazitapungua kwani makisio ya bajeti sasa yanaenda kuongezeka kwa kuwa asilimia zinaongeza fedha kwa kuwa bei imepanda kwani tozo iliyo fixed ni hizo chache tu.

Kama sote tulivyoona mapendekezo ya ACT pamoja na ya wenzetu kwenye majukwaa mbalimbali lakini serikali imekuwa kiziwi.

Hivi sisi hela ya kuongeza kununua mafuta, unga, Michele, mafuta ,vifaa vya ujenzi, nk tunaitoa wapi maana hata access ya kukopa ni shughuli na tunaserikali yenye uwezo wa kutumia hifadhi ya dollar au kukopa.

Rais wa marekani jumapili kawaambia wamarekani kuwa ameshafanya kupunguza maumivu ya gharama za gesi na mafuta sasa ni zamu ya bunge.

Lkini kwetu bunge linamngojea serikali inataka nini na serikali inasikiliza wafanyabiashara wanataka nini.

Sasa hao watumishi mnaowatesa mnawaongeza za nini?

Magufuli aliwaambia napunguza inflation ili kwa mshahara mkidhi mahitaji kwa unafuu

Haya wewe ajuza unasemaje na serikali yako.

Naaumia but tulitegemea utatusikiliza kuliko huyo mchemba anayezikusanya kwa ajili ya uchaguzi 2030

Pole yenu na yetu
 
haya ni mavuno ya watanzania waliyoyapanda tangu enzi zile sasa ni wakati wa mavuno,tuwe watulivu tunapovuna tulichopanda,wakati mbengu hizi zikipandwa tulikuwa kimya tukijipa maneno ya faraja eti hapa kazi tu,kasi mpya ari mpya na maneno kedekede ,wacha ninywe uji wa ubuyu huku nikiangalia tu.
 
Mnaya upinzani mlitegemea nini? Mnachafua uchaguzi? Mungu katupa azabu ndiyo hii.
 
Mnaya upinzani mlitegemea nini? Mnachafua uchaguzi? Mungu katupa azabu ndiyo hii.

Upinzani uliishia 2015 baada ya hapo walikuwepo watengeneza mazingira kupitia siasa na wakakutana na yule Mlume wa Chato akawanyoosha haswa.
 
haya ni mavuno ya watanzania waliyoyapanda tangu enzi zile sasa ni wakati wa mavuno,tuwe watulivu tunapovuna tulichopanda,wakati mbengu hizi zikipandwa tulikuwa kimya tukijipa maneno ya faraja eti hapa kazi tu,kasi mpya ari mpya na maneno kedekede ,wacha ninywe uji wa ubuyu huku nikiangalia tu.............................
Hatukuyapanda nyerere alitufundisha kuisikiliza serikali badala ya serikali kusikiliza umma.
 
Back
Top Bottom