Ni kweli mwanamke akielimika..........

Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
2,955
6,328
Ni kawaida kwa mwanamke mwenye elimu kubwa ya darasani kiasi cha kuajiriwa kukuta ni mwajiriwa au mjasiriamali. Sasa kwakuwa ni mtafutaji,anakuwa busy na kumweka h.g amlelee mtoto. H.g ni std 4 leaver,mtoto muda mwingi yuko na h.b,ambapo akili yake inatengenezwa kihvyo,

Je,jamii hiyo itaelimika kutokana na kuelimika kwa mwanamke huyo?
 
Hili ni janga la Taifa, binafsi ningefurahi wife angekuwa anabaki home! ila wanaweka wa siku hizi hasa wanaojiita wasomi matatizo matupu!
 
basi hakuna haja ya kuwasomesha watoto wa kike kama unatambua hiyo elimu itamfanya awe kiguu na njia kusaka pesa,hata hivyo kuna wanawake wengi vijijini wamejaa tele kwanini usichukue hao ili akuzalie na kukulelea watoto wako,kwa sababu sitaki kuamini kipindi unamtongoza huyo mwanamke hukujua kitakachofuata mbele,cha msingi ni kupanga muda wa kukaa na watoto wako kuwaelimisha yawapasayo kutenda hzo zingine ni blahblahblah tu.
 
Lakini mkuu,kijiji tunaendaga tu kusalimia kwa siku kadhaa!
 
basi hakuna haja ya kuwasomesha watoto wa kike kama unatambua hiyo elimu itamfanya awe kiguu na njia kusaka pesa,hata hivyo kuna wanawake wengi vijijini wamejaa tele kwanini usichukue hao ili akuzalie na kukulelea watoto wako,kwa sababu sitaki kuamini kipindi unamtongoza huyo mwanamke hukujua kitakachofuata mbele,cha msingi ni kupanga muda wa kukaa na watoto wako kuwaelimisha yawapasayo kutenda hzo zingine ni blahblahblah tu.
Vipi wale ambao madai ya kusoma yanaanza mara baada ya ndoa...?
 
Malezi ya mtoto ni miaka mingapi ?, na hata huyo mama akiwa ni mama wa nyumbani Je ni kweli kwamba atakaa nao watoto kwa miaka yote ?

Hivi unasomeshwa / kuelimika ili uondoe ujinga na kuongeza upeo au unasoma ili kuajiliwa na kukaa mbali na nyumbani ?, na Je kutokusoma / kuelimika ndio kukaa nyumbani ?, na watoto wakishakuwa wakubwa wife (ambae hana elimu atakaa nyumbani kumlea nani ?)

By the way hii tabia ya kuwasingia wasaidizi wa kazi kwa uchizi wa watoto wenu sio poa kabisa
 
Asnam ana jibu lake hapo!

nimeshamjibu,wanaume wanashindwa kuelewa kwamba karne hii sio zama za ujima,kulea watoto ni jukumu la baba na mama kwasababu kitandani mlishughulika wote kukata nyonga sasa kwanini linapokuja suala la malezi wamsukumia mama peke yake.
 
So tukibaki wajane baada ya waume kufariki watoto wageuke chokoraa kwa vile hatuhangaiki hatuna cha kuwapa? Nonsense.
Huyo hg std 4 leaver hawezi kulea? Mabibi zetu hawakusoma sisi tumefikaje hapa?
 
Thread closed lol. Mababu zetu hawakuenda shule ila watoto wao wametoka safi tu . Kuenda kazini haimaanishi utaacha kulea watoto wako. Malezi ni kazi ya wazazi wote wawili. Ni wajibu wetu kuchukua muda kusaidia watoto na homework pamoja na kulea wakati tupo home. Zaidi ya hapo watoto wapo shule wakati mimi nipo kazini kwahiyo haina haja ya Mimi kukaa nyumbani. Huyo housegirl ingawa hataweza kumsaidia mtoto na algebra, ana uwezo mkubwa wa kumfundisha mambo mengine kama kufua, kupika, kunyoosha nguo, kupiga viatu kiwi n.k

So tukibaki wajane baada ya waume kufariki watoto wageuke chokoraa kwa vile hatuhangaiki hatuna cha kuwapa? Nonsense.
Huyo hg std 4 leaver hawezi kulea? Mabibi zetu hawakusoma sisi tumefikaje hapa?
 
hivi mwanamke akipata elimu na kujitegemea nyie wanaume mnakuwa na kijicho sana.kazi ya kulea sii mwanamke peke yake ni woote kwa iyo u guys need to stop this stupid idea. We as girls in this generation hatutonyanyaswa kama walivokua mama zetu.mama zetu walipata tabu sio chengine ni kukosa elimu na kutoweza kututegemea. wanastahamili mingi na kukaaa kimya watoto hawajui lakini akikuhadithia a-z alonifanyia babayo utaenda mbio. Girls move one this is new generation.
 
tumekataa na tumechoka kuwa magoal keeper,cha msingi ni mama akitoka kazini ajitahidi kuwa karibu na mwanaye na afanye baadhi ya kazi za nyumbani siyo kila kitu afanye housegl!
 
Hili ni janga la Taifa, binafsi ningefurahi wife angekuwa anabaki home! ila wanaweka wa siku hizi hasa wanaojiita wasomi matatizo matupu!

Hivi wanaume wa hivi bado mna exist hadi zama hizi.....
yani mwanamke awe tu anakaa nyumbani hadi hela ya kiberiti uombwe!!!makubwa....
 
Ni kawaida kwa mwanamke mwenye elimu kubwa ya darasani kiasi cha kuajiriwa kukuta ni mwajiriwa au mjasiriamali. Sasa kwakuwa ni mtafutaji,anakuwa busy na kumweka h.g amlelee mtoto. H.g ni std 4 leaver,mtoto muda mwingi yuko na h.b,ambapo akili yake inatengenezwa kihvyo,

Je,jamii hiyo itaelimika kutokana na kuelimika kwa mwanamke huyo?

Swali ni kwamba, kumuelimisha mtoto/watoto kitu gani?
Na huyo mtoto/watoto wana umri gani?
Na huyo mtoto/watoto wana jinsia gani?
Na hao watoto wanaishi wapi?
Elim ya baba na mama?
Babu na bibi pande zote wapo wapi na wanashughuli gani?

Kwani wewe unafikiri kuelimisha mtoto/watoto ni jukumu la mwanamke tu peke yake?
Mwanamme pia anawajibu wa kuelimisha watoto, tena baba akielimisha watoto, watoto wanakua very strong kichwani. Mama jukumu lake kuwapa upendo watoto na kuwafundisha madogo madogo ikiwa baba ndio anatakiwa awafundishe watoto maisha kiujumla.

Nakupa mfano maisha ya kijijini,
Baba anaplan kumchukua mtoto wake wa kiume wa miaka 9 kwenda kuwinda, sababu kashaona umri nzuri wa kumfundisha kuwinda, kidume kinaelekea, na mtoto anaonesha anataka kujifunza kuwinda, kaanza kucheza michezo ya kuwinda winda.
Baba anaanza kumfundisha jinsi ya kutengeneza mshale, upinde nk. Na vyote muhim vya kuzingatia.
Mwezi baadae safari ya kuwinda imewadia, mtoto anafurahi sana kufatana na baba yake. Hayo mawindaji wanajarudia mara kwa mara, mtoto anajifunza msitu, wanyama porini, na miti.

Au pale baba anaplan kumchukua mtoto wake wa kiume wa miaka 9 akamfundishe kuvua samaki, anaanzia nyavu, mashua na vyote vya kuzingatia. Mtoto anaweza kujifunza kuogelea na kuokoa maisha yake na mwingine majini, anajifunza kudil na maji na wanyama wa majini.

Watoto wanatakiwa wajifunze jinsi ya kudil na mazingira, na vitu vya kitamaduni tamaduni,
kwa mfano uwimbaji, hadithi, uwindaji, uvuvi, uchungaji, uchezaji mpira, upigaji ngoma, kulima, kupanda juu ya miti, kutembea maporini vichakani, kucheza na wanyama, kucheza na maji, kuogelea, kutengeneza viatu, kulima bustani, kuuza vitu, kufua, usafi, kupika, kazi za nyumbani. Mzazi anaweza kutumia wiki mara moja kumfundisha, na mzazi unatakiwa umfundishe mtoto wako kile ulichojifunza wewe mwenyewe utotoni na unakifaham vizuri.

Lakini nyinyi baba wa siku hizi badala ya kutumia muda baada ya kazi na weekend kuwafundisha watoto wenu vitu muhim vya kimaisha, munaenda nyumba ndogo, mpirani na mambo yenu binafsi.

Na akina mama wao wakitoka kazini anaelekea saloon, na kuenda madukani, masokoni, kwa marafiki, na kujistarehesha binafsi.

Researching imegundua kuwa wazazi wote wawili wakifanya kazi, ni fundisho tosha kwa mtoto kufaham kuwa wazazi inabidi wafanye kazi ili waweze kuwalisha wao, watoto.

Lakini kama mzazi akitoka kazini anaishia mitaa na kurudi home kulala tu, duh hiyo ni kuaribu watoto
 
Hivi wanaume wa hivi bado mna exist hadi zama hizi.....
yani mwanamke awe tu anakaa nyumbani hadi hela ya kiberiti uombwe!!!makubwa....

Bado, na kila mwanaume anapenda hivo akirudi full service, sio oooh nimechoka, mara nitachelewa! Hata mm kama ningekuwa na uhakika wa kupata 10M/day ningekuwa nafanya kazi ya kusupervise tu (maximum of 2hrs a day muda mwingine nakula kuku na familia yangu)
 
Unasema tu wewe, hapo ukirudi mkeo akaomba hela ya saloon maneno yatakutoka...
mishipa itakusimama, jicho litakuwa jekundu aku ya nini yote hayo!!!!
 
Back
Top Bottom