Uanzishwaji wa TRA mchakato ulianza kipindi cha Raisi Mwinyi kama moja ya masharti ya Structural Adjustment Policy ambayo serikali ya Tanzania ilishauriwa na The Breton Woods Institutions (IMF & WB) kwamba kuwe na chombo kimoja kilichoanzishwa kisheria, na huru (Autonomous) ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia ukusanywaji wa mapata yote nchini.
Mambo mengi ya kuzifanya taasisi zilikuwepo kipindi cha Raisi Mwinyi kuwa ni za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya soko huria yalifanywa chini ya Mzee Mkapa: Vyombo vingi vilikuwepo japo aidha vilikuwa chini ya Wizara fulani na siyo huru kama ilivyo leo. Japo lazima tukubali kwamba Mzee Mkapa ana sehemu yake kusukuma hili kufanyika ili aweze kuendana na mahitaji ya Uchumi wa soko huria ambao yeye aliauamini sana.
Ukiangalia vizuri kipindi hiki ndiyo yalifanyika mabadiliko makubwa sana kwenye sheria za nchi ambayo yalibadilisha muundo wa taasisi mbalimbali za kitaifa na kuzipanga upya. Sheria nyingi sana zilikuwa Revised na taasisi nyingi zikawekwa kisheria.
Nipo ndugu yangu.Upo?
Since Mtei aliwahi kuwa waziri wa fedha
Possibility ni kuwa wazo lake kama kweli lake
Lilikuwepo Tu hapo wizarani likifanyiwa kazi na
Review miaka kibao..na ndo maana naona sio Sahihi kusema Mkapa alianzisha TRA
Sheria hii ilipitishwa mwaka 1995 kipindi cha utawala wa Mzee Mwinyi. Sheria zote kabla ya kupelekwa bungeni huanzia Wizara husika ambao wao hufanya jitihada za kuwatafuta wadau mbalimbali wa ndani au nje ya nchi ili waweze kutengeneza rasimu ya muswada ambao utaenda kusomwa mara ya kwanza kabisa bungeni. Katika hili watu wa Wizara hupewa hata ruhusa ya kwenda kufanya Benchmark kutoka nchi jirani ambayo imefanikiwa kwenye hili.Role ya Kikwete ilikuwaje kama waziri wa Fedha chini ya Mwinyi?
Manake amewahi kunukuliwa pia kuhusika na uundwaji wa TRA
Sheria hii ilipitishwa mwaka 1995 kipindi cha utawala wa Mzee Mwinyi. Sheria zote kabla ya kupelekwa bungeni huanzia Wizara husika ambao wao hufanya jitihada za kuwatafuta wadau mbalimbali wa ndani au nje ya nchi ili waweze kutengeneza rasimu ya muswada ambao utaenda kusomwa mara ya kwanza kabisa bungeni. Katika hili watu wa Wizara hupewa hata ruhusa ya kwenda kufanya Benchmark kutoka nchi jirani ambayo imefanikiwa kwenye hili.
Jakaya kama Waziri ndiye aliyesaidia kufanya haya hadi tukapata sheria mwaka 1995, lakini Mzee Mkapa alihakikisha taasisi inaanza kufanya kazi mwaka 1996 kwa kuifanya taasisi isiwepo tu kwenye makaratasi kama mashirika mengi ya serikali yalivyo. Hivyo nadhani kusema Mzee Mkapa ndiyo anatakiwa kupewa pongezi peke yake nakataa kabisa maana hili jambo lilikuwepo serikalini muda sana likishughulikiwa.
Hivi kwa mfano hii Stiglers gorge ikikamilika credits zinaenda kwa nani? Mwalimu, Ruksa, BWM, JK ama JPM? Mimi kwa mawazo yangu ni JPM....hata kuhamia Dodoma, clearly credits zaidi zinaenda kwa JPM, sivyo?Since Mtei aliwahi kuwa waziri wa fedha
Possibility ni kuwa wazo lake kama kweli lake
Lilikuwepo Tu hapo wizarani likifanyiwa kazi na
Review miaka kibao..na ndo maana naona sio Sahihi kusema Mkapa alianzisha TRA
Hivi kwa mfano hii Stiglers gorge ikikamilika credits zinaenda kwa nani? Mwalimu, Ruksa, BWM, JK ama JPM? Mimi kwa mawazo yangu ni JPM....hata kuhamia Dodoma, clearly credits zaidi zinaenda kwa JPM, sivyo?
Factually tuseme hivi:Shida sio credits
Ni namna ya kuandika ukweli.
Tutasema JPM alianzisha stiglers gorge?
Au alikamilisha?..
Sidhani sahihi kusema Mkapa alianzisha TRA
Labda tuseme Mkapa alikamilisha uanzishwaji wa TRA..
Sometimes history huwa hazina ukweli aslimia 100% hivyo sishangai kwa wanaosema hivyo hata sasa wapo watu wanasema Magufuli ameanzisha Mahakama ya mafisadiNi vizuri kukawepo na ukweli zinapoandikwa historia za Viongozi wetu na historia ya nchi yetu Kwa ujumla..
Nimesikia mara kadhaa watu wakisema Rais Magufuli kajenga daraja la Kigambon na nabaki na maswali mengi..
Sasa hili la Mkapa kuunda TRA pia linanitatiza sana ..kivipi?
Nimemsikia mara kadhaa Rais mstaafu Kikwete akisema aliunda TRA alipokuwa waziri wa fedha wakati Rais ni Mwinyi..
Na alisema alienda Uganda nafikiri kupata uzoefu wao WA URA..na wapo waliokuwa wanamshauri vinginenevyo..
Ifahamike wakati Rais Mwinyi anamteua Kikwete kuwa waziri wa Fedha hata uchaguzi wa ndani wa CCM wa mgombea ulikuwa bado na hakuna aliekuwa anajua kama Mkapa au anyone atakuja kuwa Rais wa Tanzania miezi michache baadae...
Binafsi nafikiri kuna 'watu wanaostahili' credit za kuunda TRA lakini hawatajwi..
Hata Kikwete probably alikuta 'process' IPO tayari akafanya kuiongeza nguvu..
Na Mkapa alipokuwa Rais miezi michache later 'ikawa rasmi'...
Kusema Mkapa aliunda TRA sio sawa..
Na hata Kusema Kikwete aliunda TRA pia sio Sahihi..labda tuseme Mwinyi? Au
'wataaalam wetu wa wizara ya Fedha'
Ambao hawatajwi na kuacha wanasiasa kubeba credits ambazo sio zao?..
Ni Sawa na kusema Mkapa alianzisha DSE
Au UTT wakati nimewahi msikia Mtaalam mbobezi na first CEO wa DSE na first CEO wa UTT akisema alikuwa anaenda waeleza
Viongozi kuhusu UTT hawaelewi kitu..wanamshangaa..hata DSE walikuwa wanasema nchi bado haipo tayari...
Sijui Yuko wapi Hamis Kibola Leo hii na kama kuna mtu hata anamtaja kama
'The brain behind DSE na UTT....
Swali linabaki pale pale je Mkapa ndo aliunda TRA?
Factually tuseme hivi:
1. Wazo na sheria ya kuunda TRA lilipitishwa chini ya Rais Mwinyi (kutunga sheria)
2. Kuunda TRA na kuanza kufanya kazi kulifanywa chini ya Rais Mkapa (kutekeleza sheria)
Fair?
Kwahio Credit should go to Mabeberu ?TRA, URA na KRA yote yalianzishwa pamoja 1995 kwa msaada toka Benki ya dunia, ikiwa ni fedha ya msaada toka kwa mabeberu.
Yeah ni kwel hata neno serikali ukilichanganua ni pana lakin kunyoosha maelezo huwa wengine wanasema serikali ya Magufuli lakini japokuwa haipaswi kuwa hivyoMkuu nadhani hua wanapewa credit wanasiasa kuondoa mlolongo mrefu wa walioshiriki kitu kufanyika au kutokea. We mwenyewe unaona ulivozunguka sana kumpata muanzilishi wa TRA.
Kuunda, kuanzisha, ....nafikiri tunachanganya hapo. Sheria peke yake haifanyi kitu au jambo litokee....ni mpaka mtu atende. Kuunda TRA maana yake nini? Kwangu mimi ni kule kuteua Bodi ya TRA pamoja na Commissioner General kama sheria inavyotaka. Haya mawili alifanya Mkapa, sio Mwinyi. Angeweza kuacha kufanya, kama ambavyo Mamlaka kadhaa ambazo zimetungiwa sheria lakini bado hazijaundwa mpaka leo....nimetoa mfano wa Mamlaka ya kushughulikia Madawa ya Kulevya.....again, "imeundwa" chini ya Rais Magufuli ingawa sheria yake ilipitishwa chini ya JK.TRA ilishaundwa kisheria na Mzee Mwinyi,
Mkapa alitekeleza sheria tu iliyokwishaweka mifumo yote ya TRA iweje.
Kwa kweli siyo sahihi kumpa Mkapa credit za kuunda TRA
Mkapa ana credits za Mifumo kama vile, NHIF, TACAIDS, TANROADS, TVT (Siku hizi TBC1), Uwanja wa Mpira wa Taifa, Kuvuta Maji kutoka mwanza hadi Shinyanga, TASAF, PSRP, TCU, LOANSBOARD, REPOA na mengine mengi mazuri
Hayo ndo aliyaanzisha yeye, kwa michakato aliyoifanya yeye akiwa Kiongozi, Lakini siyo TRA, TRA alikuta ishaundwa kisheria tayari na mzee Mwinyi, yeye alitekeleza tu sheria.