Ni kweli Makonda ana ' mapungufu ' yake ila kwa hili la ' Kuzushiwa ' kwa kinachomsibu sasa Ruge tunamuonea sana!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,921
Siku zote nitasimama katika ukweli na katikati bila kuwa ' Mnafiki ' au Kumuonea fulani na hivyo ndivyo nitakavyokuwa siku zote. Kwa masikitiko makubwa kabisa nimekuwa nikifuatilia sehemu mbalimbali hasa Mitandoni humu na kujikuta sasa naanza kupata wasiwasi juu ya muelekeo wa Watanzania wengi.

Yaani Watanzania badala ya kuwekeza nguvu zetu nyingi katika Kumuombea Afya Njema Ndugu yetu ( Mtani wangu ) Ruge Mutahaba kutokana na matatizo yake ya ' Figo ' ambayo yanamsumbua kwa Kipindi kirefu tu sasa wengi wetu tumeanza kuhamisha Goli na kuanza ' Kumsingizia ' Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda kwamba amemlisha ' Sumu ' inayomuua taratibu kwakuwa tu inasemekana wana ' Uadui ' japo Mimi GENTAMYCINE naamini kuwa umeshaisha na Wawili hawa wapo vizuri tu.

Najua leo GENTAMYCINE nitawaudhi wale ambao ' wanamchukia ' Mkuu wa Mkoa Makonda kwa sababu zao mbalimbali ila mtanisamehe tu kwakuwa huwa napenda ' Haki ' na ' Usawa ' baina ya Wawili unaochagizwa na ukweli pamoja na uhalisia wa jambo husika.

Nimeona mahala kuna Mtu mmoja ( anayeaminika sana na Watanzania wenye mrengo wa Kushoto ) akisema kwamba hata Bosi Ruge Mutahaba nae pia anaamini na ana uhakika wa 100% kuwa Ugonjwa wake huo unatokana na kuwekewa ' Sumu ' inayomuua taratibu na huyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda.

Kama ni kweli Mtani wangu Ruge Mutahaba maneno haya ameyasema Yeye basi nitaanza Kumpunguzia ' marks ' zangu za ' Umakini ' ambazo nimemuwekea tokea nianze Kumfahamu kwakuwa ni Mtu mmoja ambaye namkubali sana na hasa kutokana na uwezo wake mkubwa mno wa Ubunifu, Uthubutu na Utendaji Kazi wake. Ila mpaka sasa siamini kama kweli Ruge amesema haya maneno ambayo huyo ' Mtanzania Mghaibuni ' anayaeneza.

Kwa sababu za Kimaadili na hasa kwa taarifa za Afya ya Mtu huwa si desturi nzuri kwa Mtu kuanza ama Kuuzungumzia au hata Kuutaja Ugonjwa wa Mtu lakini hapa niseme tu ya kwamba tatizo hilo la Figo la Ruge Mutahaba halijaanza leo na tena kwa taarifa ambazo nimepewa ni kwamba kumbe hili tatizo la Figo limekuwa likimsumbua Ruge hata kabla Makonda hawaja ama Mkuu wa Wilaya au hivi Mkuu wa Mkoa na nimesikitika na bado naendelea kusikitika kuona sasa anahusishwa nalo.

Hata kama tunamchukia ila tujitahidi muda mwingine kutokuwa ' Wazushi ' mwishowe tukajikuta tunajichumia bure dhambi kwa Mwenyezi Mungu. Muda mwingine tufanye mambo kwa kumuogopa Mola / Allah. Najua kuwa Makonda kuna muda anakera na kuudhi na hata Mimi GENTAMYCINE huwa ' ananishangaza ' na nimekuwa nikimsema mno hapa Jamvini JF lakini kwa hili tunalomuhusisha nalo nina uhakika wa 100% kwamba wengi wetu tunaomsingizia na kumuhisha nalo tunajichumia bure dhambi na ipo siku zitakuja Kututesa.

Tumseme Mtu kwa haki na siyo kwa Kumsingizia ama Kumzushia kwani siyo jambo zuri na halina Tija wala Afya Kwetu.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda endelea na Kazi zako za Kiutendaji ila Mimi kama GENTAMYCINE nakuomba kama itakuwa chini ya uwezo wako na najua unaweza na una Mamlaka kama Mkuu wetu wa Mkoa hebu livalie njua upesi sakata la akina Maua Sama, Soudy Brown na Shaffih Dauda ili basi waweze kuachiwa hata kwa dhamana. Sitaki pia kuamini kwamba unahusika kwa wao kuwepo ndani huko waliko sasa ila nakuomba tu ' wapiganie ' ili wawe huru na naamini watajirekebisha na maisha yataendelea.

Nitashukuru sana kama Ombi langu hili utalifanyia Kazi na najua hutoniangusha GENTAMYCINE katika hili. Akhsante.

Nawasilisha.
 
Huyu mtoto anapenda sana umbea; sasa hayo yanatuhusu nini? Inakusaidiaje kupambana na matatizo yaliyokulemea
 
Mkuu Makonda Huyu Sio Wakumuwekea Dhamana, lolote linawezekana

' Sometimes ' tunamsingizia na kumuonea sana kwakuwa tu tayari yumo ' Mioyoni ' mwetu kwa Chuki kama siyo Husuda. Hata Mtu wa karibu kabisa na Ruge amenielezea kuwa Bosi Ruge hilo tatizo amekuwa nalo kwa muda mrefu na kwamba amekuwa akisafiri mara kwa mara nchi za nje kwa matatibabu yake ila kwa sasa wanaona kama vile Dawa zinaanza ' Kukataa ' japo wanaomtibu wanajitahidi huku wengine wakizidisha ' maombi ' yao.

Kwa hili nitamtetea Makonda hadi mnune na mninunie. Tuache Kuzushazusha tu kwasababu ya Chuki zetu zilizopitiliza. Tunamuonea mno katika hili na ikiwezekana wale wote ambao nanyi mmeamini na kudhani kuwa ni kweli basi muda bado mnao wa ' Kutubu ' kwa Mungu / Allah na bado mtasamehewa tu ' dhambi ' zenu.
 
Kwa Bashite aka mzee wa kujipendekeza kwakweli lolote linawezekana!.

Namuogopa sana Mwenyezi Mungu / Allah hivyo sipendi kabisa ama ' Kumzushia ' au ' Kumsingizia ' Binadamu mwenzangu kwa lolote lile. Kwa hili tunamuonea na tunamsingizia sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. Tumuogopeni Mola!
 
sijaona sehemu yoyote yenye ushaidi wa maana naona tu 'nimeambiwa na mtu wa karibu' kwani kuambiwa na mtu wa karibu ndo inafanya kuwa kweli

mara ugonjwa ni siri, hapo hapo unasema anaumwa figo tangu zamani (siri iko wapi)

mara nasimamia kweli na haki, asa kweli gani ikiwa yote niya kuambiwa na wala huna ushaidi wa hayo ya kuambiwa kama ni kweli ama laah.

Kifupi hakuna cha maana ulicho andika
 
Siku zote nitasimama katika ukweli na katikati bila kuwa ' Mnafiki ' au Kumuonea fulani na hivyo ndivyo nitakavyokuwa siku zote. Kwa masikitiko makubwa kabisa nimekuwa nikifuatilia sehemu mbalimbali hasa Mitandoni humu na kujikuta sasa naanza kupata wasiwasi juu ya muelekeo wa Watanzania wengi.

Yaani Watanzania badala ya kuwekeza nguvu zetu nyingi katika Kumuombea Afya Njema Ndugu yetu ( Mtani wangu ) Ruge Mutahaba kutokana na matatizo yake ya ' Figo ' ambayo yanamsumbua kwa Kipindi kirefu tu sasa wengi wetu tumeanza kuhamisha Goli na kuanza ' Kumsingizia ' Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda kwamba amemlisha ' Sumu ' inayomuua taratibu kwakuwa tu inasemekana wana ' Uadui ' japo Mimi GENTAMYCINE naamini kuwa umeshaisha na Wawili hawa wapo vizuri tu.

Najua leo GENTAMYCINE nitawaudhi wale ambao ' wanamchukia ' Mkuu wa Mkoa Makonda kwa sababu zao mbalimbali ila mtanisamehe tu kwakuwa huwa napenda ' Haki ' na ' Usawa ' baina ya Wawili unaochagizwa na ukweli pamoja na uhalisia wa jambo husika.

Nimeona mahala kuna Mtu mmoja ( anayeaminika sana na Watanzania wenye mrengo wa Kushoto ) akisema kwamba hata Bosi Ruge Mutahaba nae pia anaamini na ana uhakika wa 100% kuwa Ugonjwa wake huo unatokana na kuwekewa ' Sumu ' inayomuua taratibu na huyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda.

Kama ni kweli Mtani wangu Ruge Mutahaba maneno haya ameyasema Yeye basi nitaanza Kumpunguzia ' marks ' zangu za ' Umakini ' ambazo nimemuwekea tokea nianze Kumfahamu kwakuwa ni Mtu mmoja ambaye namkubali sana na hasa kutokana na uwezo wake mkubwa mno wa Ubunifu, Uthubutu na Utendaji Kazi wake. Ila mpaka sasa siamini kama kweli Ruge amesema haya maneno ambayo huyo ' Mtanzania Mghaibuni ' anayaeneza.

Kwa sababu za Kimaadili na hasa kwa taarifa za Afya ya Mtu huwa si desturi nzuri kwa Mtu kuanza ama Kuuzungumzia au hata Kuutaja Ugonjwa wa Mtu lakini hapa niseme tu ya kwamba tatizo hilo la Figo la Ruge Mutahaba halijaanza leo na tena kwa taarifa ambazo nimepewa ni kwamba kumbe hili tatizo la Figo limekuwa likimsumbua Ruge hata kabla Makonda hawaja ama Mkuu wa Wilaya au hivi Mkuu wa Mkoa na nimesikitika na bado naendelea kusikitika kuona sasa anahusishwa nalo.

Hata kama tunamchukia ila tujitahidi muda mwingine kutokuwa ' Wazushi ' mwishowe tukajikuta tunajichumia bure dhambi kwa Mwenyezi Mungu. Muda mwingine tufanye mambo kwa kumuogopa Mola / Allah. Najua kuwa Makonda kuna muda anakera na kuudhi na hata Mimi GENTAMYCINE huwa ' ananishangaza ' na nimekuwa nikimsema mno hapa Jamvini JF lakini kwa hili tunalomuhusisha nalo nina uhakika wa 100% kwamba wengi wetu tunaomsingizia na kumuhisha nalo tunajichumia bure dhambi na ipo siku zitakuja Kututesa.

Tumseme Mtu kwa haki na siyo kwa Kumsingizia ama Kumzushia kwani siyo jambo zuri na halina Tija wala Afya Kwetu.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda endelea na Kazi zako za Kiutendaji ila Mimi kama GENTAMYCINE nakuomba kama itakuwa chini ya uwezo wako na najua unaweza na una Mamlaka kama Mkuu wetu wa Mkoa hebu livalie njua upesi sakata la akina Maua Sama, Soudy Brown na Shaffih Dauda ili basi waweze kuachiwa hata kwa dhamana. Sitaki pia kuamini kwamba unahusika kwa wao kuwepo ndani huko waliko sasa ila nakuomba tu ' wapiganie ' ili wawe huru na naamini watajirekebisha na maisha yataendelea.

Nitashukuru sana kama Ombi langu hili utalifanyia Kazi na najua hutoniangusha GENTAMYCINE katika hili. Akhsante.

Nawasilisha.
Leo hujaongea mambo ya 'dally kimoko' au ndio 'figo'?
 
Nilisikia makonda hapig mswak

Na viatu vyake vinanuka

Hayo waliyaongea shilawadu

Dooh chek sasa yanayowapata
Hawa shilawadu walikataa kurusha kipindi alichokiandaa Makonda kilichomhusu Gwajima, na Makonda alipokifuata kipindi chake clouds wakasema amewavamia na kuwapiga vibaya, wakaungana na Gwajima na watanzania wote kumkejeli Makonda, wakawa kila kipindi chao kikifika ni kumkashifu Makonda mara hapigi mswaki ananuka mdomo, mara ananuka miguu, wakawa hasa ka-Soudy brown kanamtumia Mange taarifa za siri kuhusu Makonda etc.

Makonda mpaka sasa anaamini kuwa yeye kuchukiwa na watz kwa kiasi kikubwa kumechangiwa na clouds maana hakuna kashfa iliyomuharibia Makonda kama ya kuvamia clouds FM. Ilisimamisha taifa ikagharimu uwaziri wa Nape kama si JPM kutumia kiburi chake cha ukoo Makonda angetumbuliwa.

Kutokana na hayo hapo juu leo hii mtu akiniambia Makonda anahusika na kuumwa kwa Ruge, kukamatwa kwa Soudy Brown, kukamatwa kwa Shaffii Dauda na Mc Luvanda wote wa clouds FM siwezi kumbishia kwa sababu za kimazingira kama nilivyoeleza hapo juu
 
sijaona sehemu yoyote yenye ushaidi wa maana naona tu 'nimeambiwa na mtu wa karibu' kwani kuambiwa na mtu wa karibu ndo inafanya kuwa kweli

mara ugonjwa ni siri, hapo hapo unasema anaumwa figo tangu zamani (siri iko wapi)

mara nasimamia kweli na haki, asa kweli gani ikiwa yote niya kuambiwa na wala huna ushaidi wa hayo ya kuambiwa kama ni kweli ama laah.

Kifupi hakuna cha maana ulicho andika

Ningeshangaa sana kama ' Matahaira ' na waliotungiwa Mimba zao ' Chooni ' wasingejitokeza. Huu Uzi GENTAMYCINE ningeuandika kwa Kumsema / Kumnanga Mkuu wa Mkoa Makonda wala msingekuja na ' such comments ' na tena mngemshambulia mno tu, ila kwakuwa mna chuki nae kubwa hivyo hamtaki awe anatendewa haki hata katika mengine ambayo kiukweli hastahili na hahusiki nayo.

Kwa hili nitamtetea Makonda hadi tutakesha hapa.
 
Back
Top Bottom