DellaPina
JF-Expert Member
- Jun 19, 2016
- 1,010
- 3,464
Swali hili ninajiuliza kuhusu hii club ya ureno inaitwa Benfica,1962 club hii ya Benfica ilishinda 5-3 dhidi ya Real Madrid ya uhispania.Kipindi hicho Real madrid ilikuwa na nyota wake wakali kama Puskas na Di stefano.Bella Gutmban ni jina geni ila kwa wapenzi wa miaka hiyo hasa wale wa Benfica wanalikumbuka alikuwa ndiye kocha wa club.Ni raia wa hungary mwenye asili ya uyahudi. Baada ya kushinda fainali akamuomba rais wa benfica aongezewe mshahara na mkataba,Rais wa Benfica akalikataa suala hilo.Bella Gutman akaamua kuiacha club lakini akawaambia viongozi kwa pamoja kuanzia leo mpaka miaka 100 Benfica haitashinda ligi ya mabingwa wa ulaya kwa sasa inajulikana Champion League.mwaka uliofuata Benfica ilifika fainali na AC Milan ya italia.Benfica ikafungwa na Milan.hapa chini nimekuorodheshea fainali ambazo Benfica amezipoteza toka Bella Gutman ayaseme maneno hayo,sasa sijui ni laana ya kweli au kwa sababu kama ni kweli inabidi benfica wasubiri ipite miaka 100 kiujumla mpaka mwaka 2062.
Fainali alizopoteza Benfica;
1962/1963 Benfica vs AC milan
1964/1965 Benfica vs Inter Milan
1967/1968 Benfica vs manchester U
1982/1983 Benfica vs Anderletch
1987/1988 Benfica vs PSV
1989/1990 Benfica vs Ac milan
2012/2013 Benfica vs Chelsea
2014/2015 Benfica vs Sevilla
Yaani maneno ya huyu jamaa alisema kuanzia leo hakuna timu yoyote ya ureno itashinda club bingwa ulaya mara mbili mfululizo na Benfica bila ya mimi mpaka ipite miaka 100 haitashinda club bingwa. wadau wa soka hili limekaaje labda leteni data za Benfica,kama kushinda kashinda ligi tu ya nyumbani ila kimataifa toka mzee aongee maneno hayo sijaiona benfica kabisa ikishinda europa league wala champion wakaombe radhi? Na jamaa mwenyewe keshafariki zamani japo 1990 kuna kiongozi alienda kuomba kaburini kwake benfica haikufanikiwa bado.