Ni kweli KTM imefungiwa na NEMC? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli KTM imefungiwa na NEMC?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Nov 15, 2008.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Wiki mbili zilizopita wakazi wa Mbagala walipata adha kubwa ya usafiri baada ya maji machafu kutoka kiwanda cha nguo cha KTM yalipoanza kupita juu ya barabara ya muda iliyowekwa na kampuni ya Kajima inayojenga Barabara ya Kilwa na madaraja mapya 2 Mto Kizinga. Hii ilitokana na mvua zilizokuwa zimenyesha siku hiyo tangu saa 11 (05:00) hadi saa 3 (09:00) asubuhi.

  Maji hayo yananuka sana na hata yanakausha majani sehemu yanayopita. Asubuhi sana ukipita utaona mvuke unatoka karibu na bomba linalotirirsha hayo maji, ambayo kwa sasa yamekuwa kama dimbwi kubwa sana.

  Licha ya kusikia kuwa NEMC wamekifungia kiwanda hicho hadi hapo kitakapotimiza masharti ya utunzaji wa mazingira na kujali afya za wakazi wa eneo hilo, ukipita usiku utasikia mwungurumo wa mashine na moshi unatoka sehemu za kutolea moshi. Sasa sijui ni kweli kimefungiwa au tulidanganywa tu ili tuamini hivyo?

  Naomba tulijadili hili na wale wenye contacts na wahusika serikalini au NEMC waweze kuwajulisha kitu gani kinasemwa kwenye vyombo vya habari na kitu gani kinafanyika.

  Hiki kiwanda kimejengwa katikati ya makazi ya watu (eneo la Kanisa katoliki, Mbagala Mission). Inasemekana huko kiwandani kuna makaburi ya wamisionari wa kwanza na msalaba na wakristo huwa wanaenda kufanya ibada za kuwakumbuka wafu wao humo kiwandani.

  Wale wenyeji wa Mbagala, kama mnapita sehemu za kiwanda usiku, jaribuni kuthibitisha haya ninayosema. Kama mtakuta siyo kweli, basi mniambie ili niondoe kauli yangu.
   
 2. BantuGirl

  BantuGirl Senior Member

  #2
  Nov 15, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe, kunakipindi walikifungia kisha baada ya muda kidogo wakaanza tena kazi cha ajabu mambo yakawa yale yale..... hakuna mabadiliko.... Cjui NEMC inafanya kazi gani... huwa inasubiri mpaka patokee jambo kubwa ndo wanaamka usingizini..... ukiangalia sasa hivi hata kambale waliokuwa pale washakufa zamani.. na cjui kama ule mvuke hauna madhara kwa wakazi wa eneo la pale, maana ukipita asubuhi mvuke wapalia kooni
   
Loading...