Kwa nini kikwete anahubiri ukabila kwa maneno wakati yeye anatengeneza taifa lka ukabila kwa vitendo?..............kikwete amajenga ukabila nchini kwa kujenga shule za kata ambazo zinabagua na watz wanashindwa kuchanganyana km ilivyo kuwa siku zetu na zake.............kikwete angemjua vipi lowasa km angesoma shule za kata............kikwete hafai kuwa rais kwani anajenga taifa lenye misingi ya udini na ukabila.
Mheshimiwa Jile 79;
Pole kwa kuandika kwa uchungu mkuu!
Ukweli ni kuwa UFISADI uliolelewa na kukomaa ndani ya CCM ndio umezaa na kuendekeza ukabila na udini. Kabla ya hapo taifa lilikuwa moja bila utata wowote. Na Rais Jk Kikwete ...amatajwa kwenye list of shame... ya Maifisadi.
Ukisoma gazeti la rai mwema la oktoba 27-novemba 2, 2010. Kichwa cha habari:
Dr Slaa afunga kazi.
...kuwashugulikia vigogo 11 wa list of of shame.
..... Aahidi kuwamaliza ndani ya miezi sita.
Limewataja baadhi ya Mafisadi wa kuu kuwa ni:
1. Rais Jakaya Kikwete.
2. Rais Mstaafu Benjamin W Mkapa.
3. Dr Daudi Balali
4. Andrew Chenge
5. Basil Mramba
6. Gray Mgonja
7. Nazir Karamagi
8. Nimrodi Mkono
9. Rostam Aziz
10. Eduward Lowassa
11......nk...nk....
Tufanye uchambuzi Yakinifu.
1. Hawa watu ni wadini moja? HAPANA ...Wanajali, kuzingatia na kuzozana dhidi ya dini ya kila mmoja wao? HAPANA ... Wameunganishwa na ufisadi , kuulinda na kujilinda na kuutetea kwa gharama zozote.
2. Ni wakibila moja? HAPANA ... Wanajali kabila la kila mmoja wao? kulizingatia na kuzozana? au kuuna kwa ajili ya tofauti za kikabila ..? HAPANA. Wameunganishwa kufisadi taifa...wataulinda ufisadi na kuutetea ..hadi kifo kiwateganishe.
3. Wana rangi ya aina moja kwenye ngozi zao? HAPANA ..wanajali hilo katika kufikia malengo yao? HAPANA ... Wameungana kwa kazi moaja tu, kulifisadi taifa na kujilinda wao na familia zao hata wengine wakimwaga damu wao haiwahusu.
4. Wanatoka kanda moja? HAPANA... Hawajali kanda za wapi katoka nani ...Chamsingi wafanikishe adhma yao ya kufisadi na kujilinda hata kutumia nguvu za dola na hata ikiwezekani toka nje ya nchi..Kudumisha umoja na nguvu ya kundi ndio msamiati mkuu.
UJINGA WA WANANCHI WETU:
1. Wanafikiri fisadi wa Kikristo anajali ukristo kuliko ufisadi na kundilake. Wanafikiri atawasaidia na kuwalinda Wakristo na kuuacha wanachama wenzake.. hata kama sio wakristo. Si kweli Fisadi wa Kikristo hatawasaida wakristo wala waislam. Fisadi wa kiristo wala hakubaliki na wakristo wa kweli.
2. Wanafikiri fisadi wa Kiisalam atawajali waislamu na kuwaacha wakristo mafisadi wenzake kwenye list of shame. Kufikiri hivyo ni ujinga na kupotoka. Hawatambui kuwa kiukweli fisadi hana dini zaidi ya ufisadi wenyewe. Hatawasaidia waislam wala wakristo..labda tu kama ni jia ya kuwanyonya na kuwatumia. Fisadi wa kiislam wala hakubaliki na Waislam wa kweli.
3. Wanafikiri eti, Fisadi wa Kihindi, ataacha na kuwakana mafisadi waafrika ili kuwatetea wahindi wasio mafisadi. Fisadi hajali ngozi ya mtu, anatizama kama uko kundini tu, kama haupo ... atakumaliz atu!
UTAMBUZI:
Utu wa Mtu; sio dini. Utu hauna dini.
Utu sio Ukabila. Utu hauna kabila.
Utu sio rangi ya ngozi. Utu hauna rangi...ni utu tu!
Utu sio ukanda. Utu hauna ukanda!
Utu sio Jinsia. Utu hauna jinsia.
LAKINI: UTU SIO UFISADI.
FISADI AMEKANA UASILI WAKE. AMEUVAA UNYAMA:
Hivyo basi FISADI Hawezi kuwa wa msaada kwa dini yeyote, kabila lolote, mkoa wowote, jinsia yeyote.. Si wakuaminiwa hata kidogo mahali popote!
UKWELI:
Kabla taifa hili kupekwechwa kwa ufisadi wa kiwango cha juu kabisa...
Watanzania tulikuwa tunaishi Bila kujali tofauti ya makabila yetu,
Watanzania tumekuwa tunaishi bila kujali tofauti ya Dini zetu,
Leo Mafisadi wanatuchanganya hadi tunaanza kuona kuwa tatizo ni dini na ukabila...Hapana si kweli na hatukubali jambo hilo. Huo ni upuuzi!
TUWAONYESHE NGUVU YA PAMOJA KUWA SISI: NI WAMOJA KATIKA UTU WETU, KAMA WAO WALIVYO WAMOJA KATIKA UFISADI WAO.
UMOJA WA UTU WETU NDIO UTANZANIA.
NA UTANZANIA SIO UKABILA, SIO UDINI, SIO UKANDA, SIO UFISADI: NI UUNGU NDANI YA MTU NA NDIO MAANA TUNAIMBA MUNGU IBARIKI TANZANIA ... !!!
Fuatilia na soma kwa kina gonga hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...sio-mkristu-sio-kabila-lingine-ni-fisadi.html