Ni kweli dhahabu ina tabia ya kupotea kimazingara?

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Watu husema kuwa dhahabu mara nyingi hupotea kimazingara. Yaani unaweza kuiweka tu ikapotea. Wanahusisha na mambo ya majini nadhani.

Wengine huenda mbali na kusema ukinunua dhahabu unatakiwa kuiweka kwenye maji usiku kucha na kisha asubuhi unywe yale maji ili isipotee.

Kuna ukweli wowote katika hili?
 
ata mimi nilisikiaga kitu kama hicho....then nakumbuka kuna mtu alishawahi kunionya kutokuingia kwenye vyanzo vya maji ukiwa na dhahabu...iwe pete ama cheni ni lazima mwisho itakutoka pasipokutegemea
 
Inawezekana ikawa kweli mana hata shemeji yenu cheni yake ilipotea katka mazngra ya kutatanisha sana
 
Nakumbuka Pete ya ndoa ya wyf ilipotea katika mzingira tata mpk Leo hatukuiona
Bila kuvuliwa? No lazima kuvuliwa.

Pete ya ndoa huvuliwa wakati gani? Unapotaka uonekane single.

Kwanini uonekane single? Ili nichepuke.

Huwezi kuchepukia ofisini, ulikua wapi? Lodge.

Kwahiyo pete itakua wapi? Lodge.

THIS IS FICTION
 
ata mimi nilisikiaga kitu kama hicho....then nakumbuka kuna mtu alishawahi kunionya kutokuingia kwenye vyanzo vya maji ukiwa na dhahabu...iwe pete ama cheni ni lazima mwisho itakutoka pasipokutegemea
Inawezekana ni kwa sababu uchimbaji hufanywa kwa kutumia uchawi na makafara (inasemekana lakini)
 
Hizo ni imani tu sawa na zile za zamani eti albino huwa hawafi wanapoteaga tu
 
Bila kuvuliwa? No lazima kuvuliwa.

Pete ya ndoa huvuliwa wakati gani? Unapotaka uonekane single.

Kwanini uonekane single? Ili nichepuke.

Huwezi kuchepukia ofisini, ulikua wapi? Lodge.

Kwahiyo pete itakua wapi? Lodge.

THIS IS FICTION
Haikuwa kama hivyo unavyofikiri coz nakumbuka tukio zima ilivyokuwa jaribu kufanya research kwa wakina mama walioolewa Pete zao nyingi huwa zinapotea katika mazingira tata japo hata hii yako inaweza kuwa sababu na kwanza wanaume ndio wanaongoza Kwa kuvua Pete ili waonekane single
 
Back
Top Bottom