Ni kweli CCM wamekosa pesa za kuandaa mkutano mkuu?

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,642
6,269
Wakati akikanusha habari zilizo enea kuwa mwenyekiti hataki kukabidhi kiti ole sendeka alidai kuwa kikao cha kk kiliendelea vizuri na mwezi June kitakuwepo kikao, ingawa tarehe haijulikani na sababu ya kutopanga tarehe ni kutokua na pesa na zikipatikana watatangaza tarehe.

Swali ni kweli CCM haina pesa wakati inamiliki raslimali nyingi kuliko hata baadhi ya taasisi nchini?
Inamiliki majengo kila mkoa viwanja vya mpira kila mkoa frem za maduka kila mkoa inapata kodi kila mkoa alafu wanadai wanatafuta pesa za mkutano.

CCM mpeni Rais uenyekiti wake msiogope kutumbuliwa kwa kuwa mliyataka wenyewe na msimuhujumu kupitia wafanyabiashara ili ashindwe.
 
CCM ni Imara sana kama kimevuka salama 2015 usitegemee kitayumba 2016. Ccm chini ya Dr. Pombe itakuwa moto wa kuotea mbali hayo mengine ni michakato ya kisiasa tuna muda huu Mwenyekit wetu Jakaya yupo Kenya kumuwakilisha Rais Magufuli kwny Mazishi ya Mama Kibaki. Mnaotabiri mpasuko ni sawa na kutabiri Jua kuchomoza Magharibi!
 
Kwa nini wazee wa chama wanamuamini sana Magufuli wakati partners wengi wa chama hawamuamini??

Maamuzi mengi ya JK yakipelekwa kwa wazee wa Chama yanatenguliwa kumfeva JPM, Swali ni JK si miongoni mwa mzee wa chama??

Nani yuko nyuma ya JK ndani ya chama, maana hata Kinana anaonekana kutofautiana sana na JK.
 
Ukawa sasa wanakuja kivingine kuzusha tu,mkutano mkuu ni june,2016,tarehe itapangwa na kamati kuu ambayo hukutana mara moja kila mwezi mna haraka gani ccm inafanya mambo kwa kalenda.
Sio kama chadema mara ya mwisho kamati kuu iliitishwa kumpokea mashinji mpaka leo kimya kila mtu kambale
 
Kwa nini wazee wa chama wanamuamini sana Magufuli wakati partners wengi wanamuamini??

Maamuzi mengi ya JK yakipelekwa kwa wazee wa Chama yanatenguliwa kumfeva JPM, Swali ni JK si miongoni mwa mzee wa chama??

Nani yuko nyuma ya JK ndani ya chama, maana hata Kinana anaonekana kutofautiana sana na JK
Leta ushahidi
 
Hahaha! Endeleeni kunitengenezea direct questions! Dr. Jakaya akihutubia Singida Feb Mwaka huu alishatuaga wana ccm wenzake akatuambia June anaondoka na ataondoka Inshallah kwa heshma kubwa ya kutokomeza Mtandao wake uliotaka kurithishwa chama na nchi!
 
Jk kila mwenye mapenzi mema na Chama anatamani akikabidhi tu chama ajikalie pembeni.

Kakivuruga sana chama hilo liko wazi.

Ni vema kama mko karibu naye kumshauri kuwa zama zake zimeisha akae pembeni aruhusu mwingine achukue chama.
 
Fedha ni kisingizio tu, Wanaogopa kumpa Ngosha rungu la pili kwani hili moja tu alilo nalo anapiga mbaya sasa ukimpa la pili si ataua kabisa
Bora yako umeona hili, wengi hawalioni.

Kuanzia kwezi ujao kutakuwa na mtifuano mkubwa sana pale Lumumba, yawezekana ile rangi ya kijani ikawa nyekundu soon.

Magufuli hataweza kuvumilia kuishi na ule uvundo ndani ya chama akiwa kama mwenyekiti, bahati nzuri sana wahafidhina wa chama wengi tu wanamuunga mkono.
 
Kwan lazima magu awe mwenyekiti wa chama? Kwa taratibu za kichama kiongoz mkuu wa chama unakuta amepitia uongoz kuanzia ngazi za chini mpaka kufikia kuwa mwenyekit wa chama taifa sasa sijui kama magu alipitia njia hizo zote za kukijua chama vyema
 
Oho,mie nataka akabiziwe rungu awa gonge gonge wale c.c.m vilaza kama jingalao,barbarosa,wakudadvua,mzee mwanakiji na wote wale twits!akitoka hapo atumbue majipu ya escrow,epa,egma et al
 
Fedha ni kisingizio tu, Wanaogopa kumpa Ngosha rungu la pili kwani hili moja tu alilo nalo anapiga mbaya sasa ukimpa la pili si ataua kabisa
Hahahaaa mkuu ...jamaa hawana namna...inawabidi wafe na tai shingoni...kifupi wanajutia kumfahamu ngosha
 
Hahahaaa mkuu ...jamaa hawana namna...inawabidi wafe na tai shingoni...kifupi wanajutia kumfahamu ngosha

Na kibaya zaidi wale wahindi mafisadi waliokua wakichangia chama hivi sasa wameweka mpira kwapani hawataki tena mechi lazma ukame upite hapo lumumba ngosha yeye yuko bize na wananchi
 
Miaka yote ccm walikuwa wanapewa na wauza sukari na mafuta! This time hakuna wa kuwapa hizo 2Bil! Sasa unadhani nani atawapa hizo pesa? Serikali? Thubutu!! Sasa chama kimevuliw nguo! JPM anataka wanachama wachangie chama sio chama ndio kiwape pesa wanachama haiwezekani!! Sasa watapata wapi? Unadhani SSB atawapa pesa na kuaibishwa huku?? Haiwezekani!! Nani atatoa pesa yake? Itarudi vipi? Labda Kitwanga pekeyake ndio atakuwa uhakika kurudi pesa yake si SSB wala MO!!
 
Hahaha! Endeleeni kunitengenezea direct questions! Dr. Jakaya akihutubia Singida Feb Mwaka huu alishatuaga wana ccm wenzake akatuambia June anaondoka na ataondoka Inshallah kwa heshma kubwa ya kutokomeza Mtandao wake uliotaka kurithishwa chama na nchi!
Muafaka wa ile Bil 73 za ESCROW vipi?
 
Na kibaya zaidi wale wahindi mafisadi waliokua wakichangia chama hivi sasa wameweka mpira kwapani hawataki tena mechi lazma ukame upite hapo lumumba ngosha yeye yuko bize na wananchi
kilichobaki ni kujitoa ufahamu ili uteuliwe UDC ...atayeongoza kwa kujitoa ufahamu mitandaoni ndo anapewa hicho cheo .. duuh hali ni tete sana Lumumba
 
CCM ni imara leo kuliko jana,acheni kujisumbua bure na CCM,mlimchukuwa Edward Lowassa fisadi mkuu mkajinasibu kukivuruga chama na kwamba nusu ya wana CCM watahama kufuata lakini kilichotokea..mnakijua.Nawashauli huo muda mnautumia kujadili CCM mngeutumia kujadili ya vyama vyenu ..CCM ni levle nyingine hamuiwezi kama unataka kujua hilo waulize Ngoyai na kingunge.
 
Muafaka wa ile Bil 73 za ESCROW vipi?

Kikwete kawafunga Mramba na Yona ma best wa Mzee Mkapa mpaka Mkapa alienda Mahakamani kuwatetea lakini hiyo haikuathiri mahusiano yao!
Mengine hatuwezi kuandika humu yataibua mjadala mwingine ila mnapaswa kujua tu mbali ya Maigizo ya kisiasa kati ya Magu na Jk ni watu wenye bond kubwa sana iliyowaunganisha!
 
Back
Top Bottom