Ni kwanini wanaume wanakufa mapema kuliko wanawake?

kityentyee

Member
Mar 9, 2021
72
338
Amani iwe nanyi bandugu,, natumai muwazima wa afya. Bila kupepesa macho wala kuzunguka zunguka napenda kuwaletea kwenu swali fikirishi hili,,,,,

Hivi ni kwanini wanaume kwa asilimia kubwa wengi hufa mapema or hutangulia kufa kuliko wanawake? Najiuliza swali hili sana kwa kutumia experience zangu tu katika maisha yetu haya ya nyumbani TZ na hata nje ya Tz.

Utakuta kuna familia nyingi sana zina wajane ,,,wanawake wengi sana wamefiwa waume zao,,,hata vifo vingi ukifuatilia ni vijana wa kiume na wanaume wengi tu wanakufa sana hii sijui ni kwa sababu gani.

Ukijaribu kufuatilia mifano mingi ya watu maarufu duniani waliokufa na kuacha wake zao utagundua kuna kaukweli fulani kanakuja akilini kuhusu hiki ninachokisema.

SAJUKI~wastara,,,,,,JK NYERERE ~mama maria,,,,JPM~mama Janneth,,,,,,BW MKAPA~ mama Anna mkapa,,,,MANDELA,,,,MUGABE,,,,Na hivi juzi juzi uingereza wamefiwa na mume wa malkia Elizabeth,,,,na wengine weeengi mnaweza kuongezea na nyinyi bandugu.

Naweza kuwa nipo shallow sana kuelezea hiki nilichokiandika ila tu hiki kitu kinafikirisha sana katika hali ya kawaida mtagundua tu kwamba asilimia kubwa wanaume wengi wanawahi kufa kuliko wanawake,,,,na kuwaacha wanawake wakiwa bado wanadunda tu.

Niombe radhi kwenu kama kuna pahala ntakua nimeteleza katika uandishi wangu ila tu naomba mchango na mawazo yenu bandugu.
 
1.Shughuli zetu za kiutaftaji nyingi znachosha miili yetu
2.Asili yetu kua wazito kuchek na kuomba ushaur na tiba za kidaktar kulinganisha na kinamama
3.Hatusemi tunaishi nayo tunapata stress na sonona
 
Mawazo +majukumu mazito
kwenye suala la kucheki afya niwazito sana wabishi
Changanya na wivu uliopitiliza
Michepuko lukuki inayochanganya akili zenu
Siku za kuishi hapo lazima zipungue
 
Wanaume wanakufa wengi kwa sababu zifuatazo ,

1. Kuna wanao oa mwanamke kamzidi umri mrefu kwa mfano binti ana miaka 21 mume wake ana 32 hii ni kutokana na mfumo wa kupata kipato unamlazimu mwanaume kujipanga kwa muda mrefu ili awe na makazi na kazi endapo akikosa ajira au hata akiwa na ajira.
Kwa wanawake wanaolewa na walio wazidi umri kwa sababu wanakuta hali ya maisha mwanaume katengeneza kwahio inamlazimu aolewe ili maisha yaende.

Kutokana na utofauti wa umri hivyo wakifikisha 51 - 62 mwanaume anawahi kuchomoka au kufariki " difference in age".
Hii inatokea sana. Wengine hata humu wamo wameoa na kuolewa na difference ya miaka 20.

2. Kuoa kwa kutumia pesa au uwezo wanaume wengi wanaoa wanawake wasiokua wa kwao ila shida zinazowakumba wanawake walitumia kigezo za kuwachukua na kuishi nao " hivyo ndoa inakua ndoano mwanamke anabadilika hakujali hakusikilizi kwa sababu hakuna upendo hivyo mwanaume anazongwa na mawazo kwa sababu ya kukosa ushirikiano na mwenza wake

Mwisho wake ni kufariki kwa kuchoka visa na maneno.

3. Kuoa wanawake wengi wanaume wanakufa kwa sababu ya kua na wanawake wengi au wake wengi ambao hupelekea kumpa majukumu mengi na visa, ukiachana na kulogwa ila ada, kodi , ujenzi na mambo kwenda mlama yamechangia kifoo na kuwaacha wake zao.

4. Afya kuzolota kwa sababu ya ulaji usio na afya kuna watu wana amini Pombe na nyama ndio chakula kizuri pekee, matumizi ya sukari na chumvi kwa wingi na kusahau mboga za majani na vya kula vya asili kama asali, mihogo, viazi na matunda hivyo kupelekea kushindwa kula mzigo na kuishia kufa au kufa kutokana na sababu za kifamilia kwa mshituko wa moyo au lolote lile.

Hizo sababu nne zinaweza zikafanywa na mtu mmoja na asife mapema inategemea na mentality yake na uwezo wa mwili wake kuna wamasai, wakulya na wasukuma na makanila mengine huko ndani ndani wanafanya haya mambo na maisha yanaenda ila kuna vijana na wazee wa mijini ndio wanaanguka hovyo.

Mwisho age difference pamoja na wake wengi ikiendana na kaya zisizo na baba nilifanyia research ya socio-economic- profile ya wilaya ndani ya mkoa wa dodoma.

Nawasilisha.
 
Research gani inaonyesha wanaume wanakufa mapema? kwa kiwango gani?
Katika kutafakari kwangu mie naona hata wanawake wengi tu wanakufa.... tena wanaanzia umri mdogo... wanatoa mimba, wanazaa kwa shida, wanaugua, wanajiua, wananyanyasika zaidi ya wanaume. Wanaume wanazaliwa wachache zaidi ya wanawake ndio maana wakifa tu pengo linaonekana. Wanawake wanazaliwa weeengi munoooooooo .... hata wakifa lile pengo halionekani.

Jaribu kuchunguza mwanamke anapokufa tu... hapo hapo nafasi yake inachukuliwa na mwanamke mwingine na hutaona mwanamume amebaki mjane... ni wachache sana! kwa hiyo pengo la kifo cha mwanamke huzibwa fasterrrr!!!! Kazi inakuja akifa mwanamume..... hakuna wa kuziba pengo... mjane anabaki anashangaa tu hakuna hata wa kumsogeza!.....
 
Sababu mojawapo kubwa ni hii. Tunapoteza terabytes nyingi mno jamani kha !!!
IMG_20210421_191820_989.jpg
 
Uchawi upo wanaume
Siku hizi wanawake nao wanajiongeza kwa waganga manake hamtulii kwenye ndoa zenu
Sasa unakuta mchepuko anakuroga anakulisha kila aina ya madawa kwenye vyakula,wife nae anakutengeneza kwenye misosi unalishwa udambwi kama wote
Hivi unategemea hizo organ zako zitaweza kufika miaka hata 70?
Sumu nyingi mwilini zinaingia through madawa haya
Changanya na mawazo ya kusaka kipato hapo ndo basi kabisa
Mkiamua kutulia kwenye ndoa zenu,kula vizuri,fanya mazoezi,pata muda wa kupumzika na kufanya toba kwa Mungu nna hakika hizi rate zitapungua mno
Wababa oyeee
 
Sababu kuu na ya msingi
Ni wanaume hatuna ubavu mmoja coz God aliuchukua akamtengeneza mwanamke.
 
1. Mawazo
Hiyo ni sababu ambayo mwanamke anaweza akimaliza kupitia kulia(machozi),kukupiga kwa namna yoyote, n.k
Lakini mwanaume yeye yanaishia moyoni, na hata hivyo inapelekea kufa mapema
 
Back
Top Bottom