Wanajukwaa si lengo langu kumsema mtu, ama siandiki kwa kusukumwa na hisia flani flani. Tumelalamikia kwa muda mrefu utendaji wa mahakana ya kimataifa ya makosa ya jinai ya uhalifu wa kivita(ICC) bila kutizama nyenendo zetu.Tulishuhudia juzjuzi tu nchini marekani afisa mkuu wa ujasusi wa nchi hiyo aliachia ngazi baada ya kuandamwa na tuhuma za kozorota kwa mambo ya kiusala nchini humo,kadhalika na nchi zingine za Ulaya na Asia uwajibikaji kwao ni kitu muhim sana. Uchu wa madaraka umetujaa nyoyoni mwetu,viburi, sifa na ubinafsi usiokua na maana.Ivi kweli kama unajijua we unalalamikiwa na jamii unatafuta ushahidi gani uletewe ili ujiuzulu? Kama huwezi kwanini unaona aibu kuachia ngazi? Hata kama hutambui hata vitabu vya M.Mungu ambavyo ambavyo vinaelezea maisha ya manabii na mitume walivyoishi ktk tawala zao, basi itoshe hata kuonyesha heshima kwa familia yako wewe.Nataka kusema kwamba watuhumuwa wote wa ESCROW acc wasisubir muda wa ushahidi wajiuzulu mapema.
Acha kuongopa na kupotosha Watu, mbona kuna wengi tu waliojizujru nchini mwetu? Kwa mfano Mwinyi (Raisi Mstaafu) alishawahi kujiuzuru kwa kashfa ya Wafungwa kufariki, Jembe Lowasa alijiuzuru wadhifa wa Uwaziri Mkuu cheo ambacho ni kikubwa sana ktk Nchi yetu kwenye utendaji ni namba 2 baada ya Raisi, Mawaziri wengi nchini mwetu wameshawahi kujiuzuru akiwemo Bibi Zakia Megji alijiuzuru Uwaziri wa fedha!
Mzee Mtei alijizuru Ugavana wa Benki Kuu n.k
sasa sijui ulimaanisha nini au ulikusudia kusema nini kwa maana kma ni kujizuru hatuna tofauti na nchi nyingi tu Duniani!
Mkuu naona unakurupuka tu kujibu hoja, soma heading kwanza, kisha uusome uzi vizuri, tafakari na mwisho jibu hoja. Vinginevyo unasukumwa na hisia. Nilisema kuna watu husubiri waandamwe na wananchi kwanza ndo wawajibike na wengine hudai ushahidi hata kama mazingira yanajionesha waziwazi.Nikukumbushe kua hata kwa hili suala la ESCROW kuna watu wameombwa kiungwana tu wawajibike lakini wamegoma katakata.
Wewe ndio unajichangaya, Nitajie Nchi ambayo kuna Kiongozi yoyote yule Mkubwa wa ngazi ya Waziri mkuu au hata Waziri tu huwa anaamua kujiuzuru bila ya kuandamwa na kushinikizwa!
Hayo unayoyaongelea wewe sijui ya Kiongozi wa CIA Marekani ndiyo ulioyasikia kwenye vyombo vya habari lkn kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia wewe huwezi kukijua, wote hao huwa kuna shinikizo aidha ktk kwenye vyama vyao ama wakubwa wao ili wajiuzuru, na hiyo ni kila Mahali Dunia nzima, kwa nini unafikiri ilichukua muda kwa Richadi Nixon (Raisi wa Marekani) kujiuzuru?
Ukisikia vyombo vya Habari vinatangaza Kiongozi fulani amejiuzuru ujue nilazima kuna shinikzo tena kubwa tu, hivyo hata hapa kwetu ni hivyo hivyo hakuna Mtu anayejiuzuru kwa hiyari yake, hakuna kitu kama hicho Dunia Hii!
Nia haikua kubishana!Ila utambue sisi waafrika ndio tuna tabia ya kugomea hata kama mtu anashinikizwa,Na hii ni kwa sababu ya kulewa madaraka.Wenzetu hua hawana hayo,mtu akishajua kakosea basi anawajibika.
Mkuu!!!!
HIV hii no tetesi???
tafakari