Ni kwanini viongozi wengi wa Africa ni wagumu kujiuzulu?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,096
2,000
Wanajukwaa si lengo langu kumsema mtu, ama siandiki kwa kusukumwa na hisia flani flani. Tumelalamikia kwa muda mrefu utendaji wa mahakana ya kimataifa ya makosa ya jinai ya uhalifu wa kivita(ICC) bila kutizama nyenendo zetu.Tulishuhudia juzjuzi tu nchini marekani afisa mkuu wa ujasusi wa nchi hiyo aliachia ngazi baada ya kuandamwa na tuhuma za kozorota kwa mambo ya kiusala nchini humo,kadhalika na nchi zingine za Ulaya na Asia uwajibikaji kwao ni kitu muhim sana. Uchu wa madaraka umetujaa nyoyoni mwetu,viburi, sifa na ubinafsi usiokua na maana.Ivi kweli kama unajijua we unalalamikiwa na jamii unatafuta ushahidi gani uletewe ili ujiuzulu? Kama huwezi kwanini unaona aibu kuachia ngazi? Hata kama hutambui hata vitabu vya M.Mungu ambavyo ambavyo vinaelezea maisha ya manabii na mitume walivyoishi ktk tawala zao, basi itoshe hata kuonyesha heshima kwa familia yako wewe.Nataka kusema kwamba watuhumuwa wote wa ESCROW acc wasisubir muda wa ushahidi wajiuzulu mapema.
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225

Acha kuongopa na kupotosha Watu, mbona kuna wengi tu waliojizujru nchini mwetu? Kwa mfano Mwinyi (Raisi Mstaafu) alishawahi kujiuzuru kwa kashfa ya Wafungwa kufariki, Jembe Lowasa alijiuzuru wadhifa wa Uwaziri Mkuu cheo ambacho ni kikubwa sana ktk Nchi yetu kwenye utendaji ni namba 2 baada ya Raisi, Mawaziri wengi nchini mwetu wameshawahi kujiuzuru akiwemo Bibi Zakia Megji alijiuzuru Uwaziri wa fedha!
Mzee Mtei alijizuru Ugavana wa Benki Kuu n.k

sasa sijui ulimaanisha nini au ulikusudia kusema nini kwa maana kma ni kujizuru hatuna tofauti na nchi nyingi tu Duniani!
 
mululu

JF-Expert Member
Nov 7, 2014
742
500
matendo ya viongoz wa kiafrika pindi wakiwa madarakani ndio huwapa shda sana kujiuzulu, ufisadi, wizi kutowajibika na lugha za dharau kwa wananchi rejea muhongo, ndicho husababisha agome kujiuzulu coz anakua hajui nini yatakua malipo ya matendo yake! mtu anaona bora nikomae tu
 
MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,096
2,000
Acha kuongopa na kupotosha Watu, mbona kuna wengi tu waliojizujru nchini mwetu? Kwa mfano Mwinyi (Raisi Mstaafu) alishawahi kujiuzuru kwa kashfa ya Wafungwa kufariki, Jembe Lowasa alijiuzuru wadhifa wa Uwaziri Mkuu cheo ambacho ni kikubwa sana ktk Nchi yetu kwenye utendaji ni namba 2 baada ya Raisi, Mawaziri wengi nchini mwetu wameshawahi kujiuzuru akiwemo Bibi Zakia Megji alijiuzuru Uwaziri wa fedha!
Mzee Mtei alijizuru Ugavana wa Benki Kuu n.k

sasa sijui ulimaanisha nini au ulikusudia kusema nini kwa maana kma ni kujizuru hatuna tofauti na nchi nyingi tu Duniani!
Mkuu naona unakurupuka tu kujibu hoja, soma heading kwanza, kisha uusome uzi vizuri, tafakari na mwisho jibu hoja. Vinginevyo unasukumwa na hisia. Nilisema kuna watu husubiri waandamwe na wananchi kwanza ndo wawajibike na wengine hudai ushahidi hata kama mazingira yanajionesha waziwazi.Nikukumbushe kua hata kwa hili suala la ESCROW kuna watu wameombwa kiungwana tu wawajibike lakini wamegoma katakata.
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225
Mkuu naona unakurupuka tu kujibu hoja, soma heading kwanza, kisha uusome uzi vizuri, tafakari na mwisho jibu hoja. Vinginevyo unasukumwa na hisia. Nilisema kuna watu husubiri waandamwe na wananchi kwanza ndo wawajibike na wengine hudai ushahidi hata kama mazingira yanajionesha waziwazi.Nikukumbushe kua hata kwa hili suala la ESCROW kuna watu wameombwa kiungwana tu wawajibike lakini wamegoma katakata.

Wewe ndio unajichangaya, Nitajie Nchi ambayo kuna Kiongozi yoyote yule Mkubwa wa ngazi ya Waziri mkuu au hata Waziri tu huwa anaamua kujiuzuru bila ya kuandamwa na kushinikizwa!

Hayo unayoyaongelea wewe sijui ya Kiongozi wa CIA Marekani ndiyo ulioyasikia kwenye vyombo vya habari lkn kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia wewe huwezi kukijua, wote hao huwa kuna shinikizo aidha ktk kwenye vyama vyao ama wakubwa wao ili wajiuzuru, na hiyo ni kila Mahali Dunia nzima, kwa nini unafikiri ilichukua muda kwa Richadi Nixon (Raisi wa Marekani) kujiuzuru?

Ukisikia vyombo vya Habari vinatangaza Kiongozi fulani amejiuzuru ujue nilazima kuna shinikzo tena kubwa tu, hivyo hata hapa kwetu ni hivyo hivyo hakuna Mtu anayejiuzuru kwa hiyari yake, hakuna kitu kama hicho Dunia Hii!
 
Nia haikua kubishana!Ila utambue sisi waafrika ndio tuna tabia ya kugomea hata kama mtu anashinikizwa,Na hii ni kwa sababu ya kulewa madaraka.Wenzetu hua hawana hayo,mtu akishajua kakosea basi anawajibika.
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225
Nia haikua kubishana!Ila utambue sisi waafrika ndio tuna tabia ya kugomea hata kama mtu anashinikizwa,Na hii ni kwa sababu ya kulewa madaraka.Wenzetu hua hawana hayo,mtu akishajua kakosea basi anawajibika.
Siyo kweli hao unaowaita wenzetu huwa hawajizuru kwa Hiari hata siku moja huwa ni lazima kuna pressure ktk mahali, Hakuna mtu anayejiuzuru kwa hiari hata kwenye dini Maaskofu hao hao wazungu wanashikwa na kashfa ya ubakaji lkn mpaka watu waandamane na kumlazimisha Papa ndio wanajizuru na kukiri Makosa (nimetolea mfano wa Maaskofu sijaingiza udini)

Hayo ni yako lkn mimi nimejibu ulilouliza ya kwamba kwa nini Waafrika hatuna tabia ya kujiuzuru? Na jibu lake ni kwamba SIYO kweli kwa maana Viongozi wetu wengi tu tena wa ngazi za juu wameshajizuru kwa kuwajibika, labda kama ulimaanisha mambo mengine lkn hili la kuwajibika ni Dunia nzima iko hivyo hakuna asiyependa Madaraka na hivyo siyo swala la Uafrika au Uzungu bali ni Ubinadamu, kwa mfano kuna watu wanasema kwa nini Malikia Elizabeti wa Uingereza hajiuzuru na kumwachia mtoto wake ukichukulia yeye tayari ana Miaka zaidi ya 80? lkn hataki kufanya hivyo kwa maana hakuna cha kumsukuma kufanya hivyo, Mwenzake Malikia wa Uholanzi alijiuzuru na kumwachia mwanae madaraka baada ya kuona Muda umekwenda!

Brown73

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,065
2,000
Ukweli ni kwamba viongzi wengi wa kiafrika au nchi zanazo kua hawataki kuachia ngazi kabisa, kuna baadhi Yao walio achia ngazi lakini ni asilimia ndogo sana. Tatizo kubwa ni Uchu wa utajiri, ufisadi. Uwekwe kwenye neema halafu uondoke au uondolewe!! Kwa nchi zilizo endelea mtu akipatikana na kashfa mara 3 tu anaachia ngazi, Mfano Sweden kwenye chama cha social demecrat Håkan Juholt Aliachia ngazi baada ya mwaka mmoja tu kuchaguliwa kua mwenykiti wa chama hicho pale gazeti kuu la nchini Expressen kumfichua tuhuma za mkewe kutolipa au kutochangia kodi ya nyumba ambayo hiyo nyumba ilikodishiwa kwa Håkan pekee. lingine ilikua kutumia usafiri wa serikali kwa njia za binafsi na kukodi taxi.
Sasa je mwafrika au mtanzania anayetuhumiwa kwa ufisadi???
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Siyo rahisi kuacha ulaji kaka.Kumbuka watu wanauana kiteto, kashfa ya meno ya tembo hakuna mtu anayestuka kuona anahitaji kuwajibika.Hongera sana kwa wale wachache waliojengwa na busara na uwoga wa mungu.

Kuwajibika siyo lazima kiongozi akosee haya makosa ya wa chini yake kiongozi mwenye busara anatakiwabkujishusha na kujivua madaraka kabla ya kusukumwa na nguvu ya nje
 
a.k.a_Mimi

JF-Expert Member
Nov 12, 2014
292
250
Pamoja na miskendo mikubwa na ya ajabu ajabu, hawaoneshi uungwana na heshima kwa nchi kwa kujiuzuru, nchi za magharibi kakosa kadogo mtu anastep down bila hata kuambiwa kiustaarab......Juzi Kati Uingereza waziri kivuli katweet picha ina bendera ya ireland,westham na england ye mwenyewe kajivua gamba, Marekani mkuu wa ulinzi Chuck Hagel kajiondoa mwenyewe.......
 
Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,064
2,000
Mawee! Siku hizi mtu akiteuliwa kushika nafasi ya juu serikalini, tunasema AMEULA!

Siku hizi uteuzi sio utumishi bali ulaji, ndio maana baada ya uteuzi hufuata sherehe ya kupongezana.

Vv
 
Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,206
1,195
Mtu akishakula nyama ya mtu hawezi kuacha, vivyo hivyo CCm wameshaona uongozi ni ulaji, hawawezi kuachia ngazi kwa hiari mpaka afukuzwe. Napo atakaa benchi kidogo anapewa cheo kingine aendeleze wizi wake bora anaimba CCM ni nambari wani!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom