Ni kwanini baadhi ya wanasiasa wanapotosha kazi za mawakili?

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,185
7,491
Nimeshawishika kuanzisha uzi huu kutokana na tamko la mwana jf huyu;-
Hivi kwa mfano akishindwa hiyo kesi, si nae atatupwa rumande mana katetea wahalifu

Pombe si chai...
Jamani ni hivi; mtu anapotuhumiwa kwa jambo fulani haimaanishi kuwa ni muhalifu mpaka mahakama itakapothibitisha. Yaani kwa mfano wewe hapo unaweza kutuhumiwa kumbaka simba, hautahesabiwa kuwa ni muhalifu mpaka mahakama ithibitishe.

Zaidi ya hapo, ni mara ngapi tumesikia kesi za kubambikiziwa na ushahidi wa kubumbwa?

Pia ifahamike kuwa mawakili wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kama ambayo watuhumiwa hushitakiwa kwa mujibu wa sheria na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria. Kwa mantiki hiyo, hata kama mtuhumiwa anakuwa na kosa kweli, bado ana haki zake kisheria.

Mwisho:
Kama tunaamini utawala wa kisheria ni mzuri, basi tufuateni sheria bila kujali inamnufaisha nani. Sio mtu/upande ukiona unanufaika na sheria unatetea ufuataji wa sheria ila ukiona mwingine ananufaika na sheria hizo hizo unapinga ufuataji wa sheria. Hiyo haifai.

Hebu fikiria "scenario" kama hii kwa mfano.
Unaamka asubuhi, unafungua mlango wa nyumba yako, mbele yako unaona fuko lenye damu, kwa mshangao unaamua kulifungua kwa kutumia vijiti, ndani yake unaona kichwa cha twiga, unashikwa na mshangao zaidi kwamba ni nini kinatokea, wakati unaendelea kushangaa, wanatokea askari, wanakuambia wamepata taarifa kuwa una nyara za serikali, wanakukamata na kukufungulia kesi ya jinai, unaambiwa huna haki ya kuwa na wakili wala kujitetea maana umekamatwa na ushahidi mkononi, Unahukumiwa kifungo cha maisha. Je! haki itakuwa imetendeka? kama haijatendeka, tufanyeje ili iweze kutendeka?

Itakuwa ni vyema kama wanasiasa wataheshimu kazi za mawakili na mahakama kwa ujumla.
 
Moja ya haki ya msingi ya binadamu ni "kusikilizwa".Hata hao wanaopinga wanasikilizwa pia. Ni vyema tukaheshimu misingi hii ambayo ni kipimo cha ustaarabu na hekima ambayo inatambulika kimataifa na wanazuoni wote.Tuache mihemuko ya kijinga.
 
Moja ya haki ya msingi ya binadamu ni "kusikilizwa".Hata hao wanaopinga wanasikilizwa pia. Ni vyema tukaheshimu misingi hii ambayo ni kipimo cha ustaarabu na hekima ambayo inatambulika kimataifa na wanazuoni wote.Tuache mihemuko ya kijinga.
Yaani sijui watanzania tumekuwa je! yaani inasikitisha sana.
 
Scenario yako ni mfu, mwenendo wa kesi za jinai mahakamani hayaendeshwi hivyo kama ulivyoelezea.
 
Scenario yako ni mfu, mwenendo wa kesi za jinai mahakamani hayaendeshwi hivyo kama ulivyoelezea.
haiendeshwi hivyo ila kuna watanzania wenzetu watatamani iwe inaendeshwa hivyo kwa wale wasiowapenda.Ndi maana nasema kama tunaamini juu ya utawala wa kisheria, basi tusiwe na double standards.
 
Back
Top Bottom