Ni kwamba tigo A. K. A Yas wanakunywa MB'S?

Ni kwamba tigo A. K. A Yas wanakunywa MB'S?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,243
Reaction score
1,989
Na imani mnaendelea poa.

Jana nilikuwa kijijini ndani ndani na kwa bahati mbaya katika hicho Kijiji mtandao wa HALOTEL, VODACOM kasi ya internet ipo chini sana.

Sasa nikapata ushauri kwa Wadau kwamba mtandao wa Yas upo vizuri hapo kijijini niujaribu, Okay nikafanya nilivyoshauriwa na alamdulillah mtandao wa ulifanya vyema sana.

Kipengele kinakuja kwenye ulaji wa MB'S Mama yangu ni balaa, Yani kusoma tu bila ku-play chochote dakika 20 unaambiwa huna salio la kutosha. Enewei niliweka bundle la jero.

Hapa nawapenda Halotel bundle la 350 unamaliza nayo siku ikiwa unasoma tu.

Nimeshatumia mitandao mingi ila halotel ni kiboko japo kuna baadhi ya sehemu mtandao wao ni jau.
 
Internet ya Yas ni kama Jini kausha Damu. Na isitoshe wamepandisha na bando kabisa
 
Sio peke yao
Mimi nipo na Airtel aiseee 10Gb within no time
 
Ushaambiwa Tigo sasa ni yas.... Ni mwendo wa kumeza bando tu
 
Back
Top Bottom