vyanzo:-
- umasikini (wa mali na akili):
kama wewe ni kijana wa kiume uliyebahatika kuwa na maisha ya wastani (umesoma kiwango cha chuo kikuu, unapata mahitaji yako muhimu ya kijamii, unakipato cha kukuwezesha, e.t.c) mara nyingi unakuwa unategemewa na ndugu zako (wa-kiume/kike), na utegemezi ni wa mahitaji muhimu ya kijamii! Kwa mantiki hiyo basi unapopata mwenza (mchumba - mke) msaada wako kwa ndugu hupungua kwa ghafla na kwa kiwango kikubwa (sawa?) na mapokeo ni kwamba huyo mwenza ndiyo chanzo cha upungufu huo (sawa?), kwa hiyo dada zako wataanza kuonyesha vituko (wivu) kwa mwenza wako
- udhaifu wa kiasilia:
kila binadamu umwoneo binadamu mwenzake wa jinsia tofauti WIVU! Maana yake ni kwamba, Dada yako anakuonea WIVU (sio wa kushirikiana kimwili)unapoanza mahusiano na binadamu mwenye jinsia kama yake!
- u-afrika:
kama unaishi bila ndugu zako (without extended family) hakuna atakayeonea wivu mwenza wako!
KWA HIYO
- hakuna mwenye TATIZO!
wakati naolewa nilikuwa napatana sana na mawifi zangu kuliko maelezo,kukaa kidogo tulianza kutokuelewana/chuki zsizo na sababu..... walidhani mimi ndio chanzo cha wao kukosa matumizi yale waliokuwa wakiyapata kabla, kumbe ni majukumu yamekuwa mengi kwa kaka yao tofauti na kipindi alichokuwa single, lawama zote ni kwangu, tena zile za kiswahili"nimemteka kaka yao".....mama mkwe ndio kabisaaaaa...haaa ndoa hizi jamani.
Nyamayao,
Vipi shemeji zako (kaka wa mumeo) nao pia hampatani? Kuna mchangiaji amehusisha tatizo hili na umasikini. Lakini hata hivyo napata hisia kwamba tatizo hili lipo kwa wanawake zaidi kuliko wanaume (i.e. mashemeji). Hili linanipa shaka hasa kama umasikini inaweza kuwa chanzo cha tatizo hili. Tena tatizo hili lipo hata kwa mawifi ambao wana uwezo na hawamtegemei kaka yao kiuchumi.
waaambie kwenye biblia mume atamwaacha baba na mamake na kuambatana na mkewe hakuna sehemu walioonyesha atambatana na wifie!!!lingine ambalo tunakuwa nalo ni kwamba wanaumewengi awatambui umuhimu wa wake,,wewe umeoa anakuja dadko mara kwa mara naomba chumvi,naomba sukari,,kuona aitoshi ukigongana nae ati anakupiga busu ,saa mke akiangalia busu nalopigwa mumewe alitofautiani kabisa na lake pale kanisani au msikitini unafikiri kitaeleweka,,hivyo na sie wanaume tujue gap iliop[o kati mke ,dada,wazazi,,mfano mmoja mi baada ya kuoa dadazangu wengine awakumpenda mwenziwangu wakachukua jukumu la kupiga usiku wa manane ati anakuuliza uko juu ya kiuno then usiku mwema!!mmh mkewangu akasema awana muda mwingine ukiona logic,nikaamua kumwaga live beef-chicken mpaka leo ....n i dont mind
Tatizo ni njaa
I concur with u 100%, mimi ni shuhuda/muhanga/muathirika wa yote uliyonena.Nawaunga mkono watoaji mada hasa wa kwanza.Ndoa nyingi zinavurugwa na Mama wa mwanaume na watoto wao wa kike.Tatizo hasa linaanza kwa hawa vizabinazabina (dada wa mwanaume) kuanza pekeche,umbeya, unafiki na majungu dhidi ya wifi yao!! Taabu na bahati mbaya kwa baadhi ya akina mama wakwe inakuja pale anapoungana na hawa wapuuzi ktk fitina hizo.Hapo wamesahau kwamba hata wao (mama wakwe) wangeweza kukutwa na matatizo hayo ktk ndoa zao vipi wangeweza kuwatunza hao wafitini(binti zao) na hata huyo wa kiume mwenye mke wanayempiga vita? Dawa ni kuwapiga marufuku kuja unapoishi na kila mtu akae kwake,mpaka akili ziwakae sawa!![/B]