Ni kwa nini Israel ina jeshi la kisasa zaidi kwa teknolojia duniani

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Ni kwa nini Israel ina jeshi la kisasa zaidi kwa teknolojia duniani

Israel.jpg

Israel ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa mauzo ya silaha duniani, ikiwa inauza silaha zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 6.5 kwa mwaka.

MWAKA 1950, miaka miwili tu baada ya taifa la Israel kuanzishwa, ujumbe wa kibiashara wa nchi hiyo ulifunga safari kwenda bara la Amerika Kusini.

Nchi hiyo ilikuwa inahitaji wenza kibiashara. Tofauti na adui zake wa Kiarabu, Israel haikuwa na maliasili kuendesha uchumi wake. Haikuwa na mafuta wala madini. Haikuwa na chochote.

Ujumbe huo ulikuwa na mikutano kadhaa lakini ulikutana zaidi na vicheko. Waisraeli walikuwa wanajaribu kuuza machungwa, taa zinazotumia mafuta na meno ya bandia. Kwa mataifa kama Argentina, ambayo inapanda machungwa yake na imeunganishwa katika gridi ya umeme, bidhaa hizo hazikuwa na maana yoyote.

Ni vigumu kufikiria aina ya bidhaa ambazo nchi hiyo ilikuwa inasafirisha nje miaka 67 iliyopita. Leo, Israel imeendelea kiteknolojia na ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa mauzo ya silaha nje ya mipaka yake ikiwa inakadiriwa kuuza silaha zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 6.5 kwa mwaka.

Tangu mwaka 1985, kwa mfano, Israel imekuwa inaongoza kwa mauzo ya ndege zisizotumia rubani, yaani drones ambazo zinachukua kiasi cha asilimia 60 ya soko lote duniani, ikiizidi hata Marekani, ambayo soko lake ni asilimia 25 tu. Wateja wake wapo kila mahali – Urusi, Korea Kusini, Australia, Ufaransa, Ujerumani na Brazil.

Mwaka 2010, kwa mfano, wanachama watano wa NATO walikuwa wanatumia ndege zisizoongozwa na rubani huko Afghanistan. Haya yote yamewezekana vipi? Ni kwa namna gani nchi hiyo, ambayo haina hata umri wa miaka 70, imegeuka na kuwa mbabe ikiwa na jeshi lenye teknolojia ya kisasa zaidi duniani ambalo mapinduzi ya namna vita vinavyopiganwa leo?

Jibu, ni majumuisho ya tabia kadhaa za kitaifa ambazo zipo Israel pekee.

Kwanza, pamoja na udogo wa eneo la nchi hiyo, kiasi cha asilimia 4.5 ya pato la mwaka hutumiwa katika utafiti na mipango. Katika kiasi hicho, asilimia 30 hupelekwa kwenye bidhaa zenye asili ya kijeshi. Kwa kulinganisha, ni asilimia 2 tu ya fedha kwa ajili ya utafiti na maendeleo nchini Ujerumani na asilimia 17 tu ya fedha hizo nchini Marekani hutumika kwa ajili ya utafiti wa masuala yanayohusiana na jeshi.

Pia utamaduni wa uvumbuzi na ubunifu nchini humo. Waisrael hawana kawaida ya kuogopa kushindwa ukilinganisha na watu wa mataifa mengine. Wanapata hili kutokana na mafunzo ya kijeshi ya lazima kwa kila raia. Wakiwa katika umri mdogo, kushiriki katika operesheni za hatari.

Wakati kijana wa miaka 19 akishiriki katika operesheni hatari za kijeshi, wale wa nchi za magharibi wanakuwa salama mabwenini katika vyuo wanavyosoma.

Mwisho, nchi hiyo imekuwa katika mkao wa kivita tangu ilipoanzishwa, ikipigana vita karibu kila baada ya miaka michache. Ukweli huu, wa kuzungukwa na adui, unafanya ubongo ufanye kazi zaidi. Inawalazimu kuwa wabunifu na kutafuta njia nzuri na silaha ili kuweza kuishi.

Hii ni habari ya Israel….

Ulinzi wa mpaka kwa kutumia roboti

Guardium ni aina mpya ya silaha inayofahamika kama Unmanned Ground Vehicle au UGV. Haya ni magari yasiyo na dereva. Israel ni nchi ya kwanza duniani kutumia roboti za aina hii ikiwa na nia ya kuwaondoa wanajeshi katika ulinzi wa mpaka.

Tayari, magari ya Guardium yamewekwa katika mpaka wa Israel na Syria kaskazini mwa nchi hiyo na katika Ukanda wa Gaza kwa upande wa kusini.

Gari hilo linaweza kuendeshwa na askari ambaye yupo umbali wa maili kadhaa kutoka lilipo au likapewa amri mapema, juu ya maeneo yapi litakwenda kufanya doria, na kulifanya kuwa na uwezo wa kujitegemea kabisa.

Israel-1.jpg

Gari la Jeshi la Israel, yaani IDF, ambalo halina dereva, linalofahamika kama Guardium, likifanya doria katika mpaka wa Israel na Ukanda wa Gaza.

Kuongezeka kwa matumizi ya roboti katika jeshi la Israel ni sehemu ya mpango mkubwa wa kupunguza hatari kwa askari wake pale inapowezekana. Pia, askari wanahitaji kupumzika, wanahitaji chakula na maji. Kitu ambacho magari ya Guardium yanahitaji ni mafuta ya kutosha. Magari mengine yasiyo na dereva yanayotumiwa na jeshi la Israel ni pamoja na Segev.

Ikiwa inakabiliana na magaidi ambao hutumia mahandaki kuingia nchini humo kutoka maeneo kama Ukanda wa Gaza, Israel inategemea roboti zinazofanana na nyoka kuingia ardhini na kutafuta mahandaki hayo na pia makao makuu ya adui, kabla ya askari kuvamia eneo hilo.

Baharini pia haijabaki nyuma. Meli isiyoendeshwa na nahodha inayofahamika kama Protector inatumiwa na Israel katika kulinda bandari zake na kufanya doria katika pwani ndefu ya bahari ya Mediterania.

Mpango wa ulinzi dhidi ya makombora
Mwaka 2000, Jeshi la Israel lilipokea betri yake ya kwanza ya ulinzi wa makombora unaofahamika kama Arrow, na kuifanya nchi hiyo kuwa taifa la kwanza duniani kuwa na mfumo unaofanya kazi na ambao una uwezo wa kutungua kombora lolote kutoka kwa adui.

Wazo la kuundwa kwa Arrow lilizaliwa katikati ya miaka ya 1980 baada ya Rais Ronald Reagan kutangaza mpango wake wa vita ya angani na kuwataka washirika wake kushiriki katika kuunda mfumo ambao unaweza kuilinda nchi na makombora ya kinyuklia ya Urusi.

Hilo lilikuwa ni wazo la kimapinduzi. Kutokana na udogo wa emeo lake, mabomu yote katika Mashariki ya Kati – huko Syria, Iraki na Iran – yanaweza kufika sehemu yoyote nchini Israel na kusababisha hatari kubwa. Wanasayansi wa nchi hiyo wakasema kwamba mfumo wa ulinzi wa anga unaweza kuzuia hilo kutokea kwa kulitungua katika anga ya nchi jirani na kutoa ulinzi kwa taifa dogo la Israel.

Israel-2.jpg

Betri ya kombora la kujihami ya Arrow

Mpango huo ulikumbwa na changamoto kadhaa lakini baada ya vita ya kwanza ya Ghuba ya Uajemi ya mwaka 1991 wakati Saddam Hussein alipofyatua bou ya scud kuelekea nchini Israel na kuwalazimu mamiliani ya Waisrael katika mahandaki ulipata fedha kutoka kwa Marekani.

Huo ulikuwa ni mwanzo.

Leo Israel inamifumo kadhaa ya ulinzi wa makombora ukiwemo ule wa Sling ambao ni maalumu kwa ajili ya kutungua makombora ya masafa ya kati na pia ule wa Iron Dome, ambao ulitungua roketi na makombora mengi kutoka Ukanda wa Gaza katika miaka ya hivi karibuni.

Satelaiti ndogo za upelelezi
Mwaka 1988, Israel ilirusha satelaiti yake ya kwanza ya upepelezi angani, na kuingia katika kundi la mataifa nane yenye uwezo wa kurusha satelaiti angani.

Hadi sasa nchi hiyo inaendesha zaidi ya satelaiti nane angani na kuipa uwezo mkubwa wa kukabiliana na tishio kutoka kwa mataifa kama Iran, ambayo inadhaniwa kwamba siku moja inataka kuunda bomu la kinyuklia.

Ndege zisizo na rubani, ama Drones
Inajulikana kama ndege isiyo na rubani ambayo inaweza kufika Iran. Heron TP ni ndege kubwa zaidi isiyotumia rubani ikiwa na bawa lenye urefu wa futi 85, sawa na ndege ya Boeing 737. Ina uwezo wa kukaa angani kwa masaa 24 na kubeba silaha zenye uzito wa tani moja.

Wakati nchi hiyo haisemi hilo wazi, Heron TP inasemekana kuwa na uwezo wa kurusha makombora kwenda ardhini.

Israel ni taifa la kwanza duniani kuanza kutumia drones katika mapambano ya kivita. Matumizi ya kwanza yalikuwa mwaka 1969 wakati iliporusha ndege hizo zikiwa na kamera kando ya mfereji wa Suez ili kuipeleleza Misri.

Israel-3.jpg

Drone aina ya Heron TP ikiruka nchini Israel.

Kifaru cha siri
Hadi leo, kifaru aina ya Merkava ni moja ya miradi ya siri kabisa ya nchi hiyo. Inasemekana kuwa huenda kikawa ni kifaru hatari zaidi duniani, na uundwaji wake kuwa ni muhimu – Uingereza na mataifa mengine yalikataa kuiuzia nchi hiyo vifaru. Mwaka 1970 ilianza kuunda vifaru vyake.

Aina mpya – inayofahamika kama Merkava Mk-4 – kinavutia zaidi. Kinaweza kufikia mbio ya kilomita 40 kwa saa na hufungwa ngao kulingana na aina ya operesheni ambayo kinaenda kufanya.

Hollande-na-Merkel.jpg

Kifaru cha Merkava wakati wa mazoezi na jeshi la Israel kaskazini mwa nchi hiyo. IDF

Mfano, katika eneo ambalo linafahamika kuwa na mabomu maalumu kwa ajili ya kulipua vifaru, ngao nzito hutumika wakati operesheni isiyokuwa na tishio la aina hiyo huhitaji ngao kidogo.

Mwaka 2012, kifaru cha Merkava kilifanyiwa mabadiliko makubwa – kwa kuwekewa mfumo mpya unaofahamika kama Trophy. Mfumo huu ni maalumu kwa ajili ya kulinda kifaru hicho na shambulizi lolote la kombora.

kwa hisani ya gazeti la raia mwema.
 
Umempaisha saaaana israel hakuna kitu kama icho.... israrl kijeshi ni mpumbav saaaana hana lolote... tulikalilishwa vibaya tukiwa wadogo shulleni.....

Anauzaje silaha na anaongezaje teknologia na kila siku tunaskia anapewa msaada wa silaha na marekani...


Hana inshu
Tulishawazoea watu kama nyie, na duniani ni muhimu muwepo pia so endelea kubwabwaja chuya za mchele tu
 
Umempaisha saaaana israel hakuna kitu kama icho.... israrl kijeshi ni mpumbav saaaana hana lolote... tulikalilishwa vibaya tukiwa wadogo shulleni.....

Anauzaje silaha na anaongezaje teknologia na kila siku tunaskia anapewa msaada wa silaha na marekani...


Hana inshu
Unaumiiiiia dah sidhani kwa roho mbaya hii km una hata kg 40 za uzito wa mwili,hao jamaa wangekuwa weupe km unavyodai wasinge survive na kutoa vipigo daily kwa adui zake walomzunguka pande zote,
 
Sijawai kusikia israel katengeneza ndege zaid ya kununua vifaa vya kivita kwa makampuni ya Lookheed martin, Boeing Defense , Space & Security na Northrop Grumman shirika pekee la vifaa vya kijeshi ndani ya Israel ni Israel Aerospace Industries (IAI) hili ndio shirika pekee ndani ya israel wana deal na Aerospace ,Defence na Tech na walikuwa project Lavi mwaka 1980 project ya Lavi ambapo ni kutengeneza ndege za kijeshi project hyo ilikuja kushindwa mwaka 1987 baada ya bunge la israel kuachana nayo kutokana na bajeti ya program yani program cost kuwa kubwa sana ndio maana siku hizi kuna joint strike project kwa ajili ya kupunguza mzigo wa project cost


Hakuna ndege ya kijeshi mbayo hipo kwenye service mpaka sasa iliyotengenezwa Israel taasisi pekee iliyondani ya israel ni (IAI) ambayo kwa sasa inadeal na Aircraft maintenace na Aircraft upgrade hizi ni ndege za kiraia yani Business Aircraft
kampuni zote kubwa dunian za mambo ya kutengeneza vifaa vya kijeshi na mambo ya Tech za kjeshi hakuna hata moja ipo israel top 20 zote
1 Lockheed Martin Corp.
2 Northrop Grumman Corp.
3 Raytheon Co.
4 Boeing Co.
5 General Dynamics Corp

Hizo ni kampuni Tano kubwa za vifaa vya kijeshi na ulinzi umezungumzia gari la Unmanned Ground Vehicle (UGV) hiyo ni project ya Kampuni ya Lockheed Martin Corp. ya nchini USA , Israel mpaka leo bajeti ya nchi yao 50% inachangiwa na US na kila mwaka Israel wanapokea fund ya Us $ 4 billion kwa ajili ya jeshi pekee


Kitu kingne uchumi wa israel na sifa mnazoipa mbona haviendani???? kwa taarifa yenu South africa ni tajiri na inauchumi mkubwa kuliko israel Nigeria pia ina uchumi mkubwa kuliko israel kwenye nchi zenye nguvu za kijeshi Israel inaweza kuwa ya 6 au 7 hizo UAV zote za US ambazo ni MQ-1 Predator hyo kwenye picha yako na imetengenezwa na General Atomics Aeronautical Systems mwaka 1995 na kuna nyingne inaitwa MQ-9 Reaper ambazo ndizo zinatumiwa kufanya Ops kwa majeshi ya US na Israel hii MQ-9 Reaper ni kwa ajili ya Border Protection's
 
we unajidanganya sana...kama unaongea kwa chuki basi chuki zako ni hatari sana kwa ustawi wako. unawezaje ongea maneno haya mbele ya wanaume dada? yaani unasema israel hana lolote? na huu uchambuzi umeusoma? aisee... ni kwa nini hata ukweli huwa hatuukubali? israel taifa dogo limezungukwa na maadui kona zooooote nne za dunia. inasurvive inawagonga kila mara huoni kuwa hawa si watu wa kawaida?

israel watakuwa ni aliens. uwezo wao ni wa kiwango cha juu sana. hilo tukubali mimi siwapendi sababu ya ubabe wao pamoja na kuwa ni kainch kadogo lakini kapo vizuri asikwambie mtu. siwapend sabab ya wivu tu. nikilinganisha na mataifa mengine na taifa letu naona kuwa jamaa wana akili ya ziada.

Umempaisha saaaana israel hakuna kitu kama icho.... israrl kijeshi ni mpumbav saaaana hana lolote... tulikalilishwa vibaya tukiwa wadogo shulleni.....

Anauzaje silaha na anaongezaje teknologia na kila siku tunaskia anapewa msaada wa silaha na marekani...


Hana inshu
= umesoma mpaka ju...ya ngapi? ni issue
 
Israel ni noumaaaaa sana,, wengine wamezoea kubisha tuuu... Adi mmarekan ameweka program ya baadh ya wamama wa kimarekan watakaothubutu wazalishwe na waizrael mtt atakuw offered kimasomo na serikal ya USA
 
Israel ni noumaaaaa sana,, wengine wamezoea kubisha tuuu... Adi mmarekan ameweka program ya baadh ya wamama wa kimarekan watakaothubutu wazalishwe na waizrael mtt atakuw offered kimasomo na serikal ya USA
Dah mkuu uongo mwingine mpaka wasomaji wanaona aibu wao badala ya ww kuona aibu kwa uongo mkubwa mamna hii Waisrael ni watu wa kawaida sana ktk swala la matumizi sahihi ya ufahamu

Wengi kinachowafanya muwaone jamaa ni hatari ni kutokana na vita vya siku 6 lakini nataka kuwambia mchango wa Ufaransa,England na US ulikuwa mkubwa sana kwenye vita ile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom