maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Mwaka jana serikali ya Marekani ilikiri na kuomba msamaha kwa kosa ililofanya kwa kutekeleza kimakosa adhabu ya kifo kwa watu wawili.
Rais Obama alikiri kwamba kitendo cha jeshi la Marekani kuishambulia Libya na hatimaye kumuua Rais wa nchi hiyo Muammar Gaddaf hakikuwa kitendo cha haki kwa sababu Gaddaf hakuhusika hata punje na makosa aliyotuhumiwa, kwa hiyo hakuwa na hatia.
Pia serikali ya Marekani ilikiri kwamba hukumu ya kifo iliyokuwa imetekelezwa miaka mitatu nyuma kwa mmarekani mmoja mweusi ilikua imefanywa kimakosa kwa sababu upelelezi ulithibitisha baadaye kwamba kijana yule hakuwa amehusika na mauaji ya watu wawili kama alivyoshtakiwa na hatimaye kuhukumiwa kunyongwa.
Matukio haya yamenipelekea niamini bila mashaka kwamba hata hao watanzania zaidi ya 1000 aliowasema Rais kwamba wamefungwa kwenye magereza ya nchi za nje si wote walio na hatia za kweli. Na kitendo cha kusema yeyote anayekamatwa na madawa ya kulevya hatamsaidia na akaomba wanyongwe ni kiburi tu cha mamlaka aliyonayo kinachompa nguvu ya kuyatamka yale.
Kwa tunaozijua tabia na misimamo ya hawa watu weupe kwa weusi watokao bara la Afrika tunajua kinachoendelea huko nje.
Nakumbuka miaka mitatu iliyopita tukiwa uwanja wa ndege wa Amsterdam ulikamatwa mkoba uliokuwa umetelekezwa kwenye ndege ukiwa na dawa za kulevya. Lakini cha ajabu katika abiria wote zaidi ya 230 tulioshuka ni abiria weusi tu wanane tulioshikiriwa na mamlaka ya uwanja wa ndege kwa ajili ya kuhojiwa. Tulihojiwa kwa siku sita na baada ya kukosa ushahidi wa kutosha tuliachiwa lakini wenzetu watatu wa nchi ya Ghana na Nigeria walishikiliwa na baadaye wakashtakiwa kwa makosa yaliyohusiana na hati zao za kusafiria lakini pamoja na kupatikana na madawa ya kulevya, mghana baadaye aliachiwa lakini wanaigeria wawili mmoja mwandishi wa habari walifungwa kifungo cha muda mrefu ingawa mwaka jana waliachiwa kwa rufaa baada kuonekana hawakuhusika na zile dawa.
Ni kwa maana hii namlaumu mheshimiwa Rais kwa kauli ile kwamba hatawaombea msamaha eti ni heri wanyongwe tu. Hii ni kitu mbaya sana kwa Rais wa nchi kutoa matamshi makali kiasi kile ya kuwatosa watu wake kwa namna ile wakati nchi nyingine pamoja na watu wao kukamatwa na dawa za kulevya ugenini huwawekea mawakili hadi dakika ya mwisho ili kuhakikisha mtu wao anatendewa haki. Kwa kweli hata sura tu za makamanda waliokuwa kwenye mkutano ule zilionyesha jinsi walivyoshtuliwa na tamko lile la Rais, kwa kweli liliudhi sana.