Ni kosa kugundua na kutengeneza Bunduki?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,118
2,000
Naomba kujua kutoka kwenu wadau kwani nimeanza mchakato wa kutengeneza Bunduki ambayo natarajia kuwa itakuwa bora na ya kisasa sana kwa self defence,vita n.k.

Ni mwezi wa 9 sasa niko kwenye mchakato huo lakini kuna mtu kanitahadharisha na kuniambia kuwa nikikamilisha tu mpango huo nijiandae kwa maisha ya gerezani au kufuatwa fuatwa kwani ni jambo lisilotakiwa kabisa.

Kwa kuwa aliyeniambia ni mwanasheria na hatukupata muda wa kuongea zaidi kwani kwa sasa ni marehemu nataka kujua kutoka kwebnu wadau hili nalo ni kosa?
 

Uledi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
583
500
Nenda Costech ukawaeleze kuhusu huo ubunifu wako na ikiwezekana uwekee hati miliki huo ubunifu. Ukifanya hivyo unaweza kuwa salama
 

Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,200
2,000
Si kosa. Ila ukimaliza kaionyeshe kwa vyombo vya usalama isajiliwe. Mbona Alexander Kalachnikov-AK47 alianza hivyohivyo_Onana na vyombo vya usajili na hatimiliki ili wasajili na wakumilikishe utafiti na uvumbuzi wako.itakusaidia unachofanya kisichukuliwe illegal na wasije iba
ujuzi wako!
Pia si vibaya wakati huu unaendelea na utafiti,shirikiana na maafisa wetu wa pale Mzinga,wata add value kwenye utafiti wako.
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,160
1,250
Si kosa. Ila ukimaliza kaionyeshe kwa vyombo vya usalama isajiliwe. Mbona Alexander Kalachnikov-AK47 alianza hivyohivyo_Onana na vyombo vya usajili na hatimiliki ili wasajili na wakumilikishe utafiti na uvumbuzi wako.itakusaidia unachofanya kisichukuliwe illegal na wasije iba
ujuzi wako!
Pia si vibaya wakati huu unaendelea na utafiti,shirikiana na maafisa wetu wa pale Mzinga,wata add value kwenye utafiti wako.


Kama ataweza kusajili na kuoata kibali cha utafiti huo basi ndio ashirikishe watu la sivyo!!!!!!
 

Pampula jr

JF-Expert Member
May 2, 2013
609
195
Naomba kujua kutoka kwenu wadau kwani nimeanza mchakato wa kutengeneza
Bunduki ambayo natarajia kuwa itakuwa bora na ya kisasa sana kwa self defence
vita n.k.

Ni mwezi wa 9 sasa niko kwenye mchakato huo lakini kuna mtu kanitahadharisha
na kuniambia kuwa nikikamilisha tu mpango huo nijiandae kwa maisha ya gerezani
au kufuatwa fuatwa kwani ni jambo lisilotakiwa kabisa.

Kwa kuwa aliyeniambia ni mwanasheria na hatukupata muda wa kuongea zaidi kwani kwa
sasa ni marehemu nataka kujua kutoka kwebnu wadau hili nalo ni kosa?
kwanza umeshatengeneza ngapi na ulizitumia kwenye nini?maana hizo kitu mtaani zishakua nyingi na tunashangaa zinatoka wapi ila usijal kavione vyombo huska ili uvumilie maswali utakkayo kumbana nayo kila lahel mkuu
 

Iron Lady

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
4,070
1,750
ni vizuri ukawaomba ushauri vyombo vya usalama kwa matumizi ya ubunifu wako ili kuwa mikono salama. kwani kitu unachotengeneza sio mwanasesere ila kina uwezo wa kuja kuharibu maisha yatu na mali zao.
 

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
13,154
2,000
Kwa hali ya usalama ilivyo ya mashaka duniani kwa sasa,mwenye heri ni yule anayeweza kugundua chombo cha kuwaunganisha watu duniani kwa maana ya kureinstall upendo na utu mwema kuliko kuendelea kufanya tafiti zinazopelekea kugundulika kwa zana imara zaidi za kufarakanisha dunia!
 

cha'

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
466
195
Kama ya kujilinda, ukifanikiwa kutengeneza yenye recoil ndogo kupita Colt, mteja nipo.
Silaha nyingi zinanunuliwa kutoka makampuni binafsi zilizobuniwa na watu binafsi huko nje. Ukifuata taratibu unaweza fungua kiwanda, soko la Afrika pekee ni kubwa mno.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom