Ni kitu gani uliambiwa hutoweza kukifanya na sasa unakifanya freshi tu?

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
STEVE HARVEY:

Mtangazaji maarufu wa Marekani Steve Harvey hununua zawadi ya TV kila mwaka na kumpelekea Mwalimu wake wa zamani ambaye aliwahi kumwambia kamwe hatokuja kuonekana kwenye TV.
Steve anasema Mwalimu alimwambia kauli hiyo akiwa mdogo baada ya kuwapa Wanafunzi maswali ya kutaka waeleze wanataka kufanya kazi gani ukubwani au wanataka kuwa nani.

Steve ambaye alikuwa na tatizo la kigugumizi kikali wakati huo aliandika anataka kuwa Mtangazaji mkubwa atakayeonekana kwenye TV lakini Mwalimu akamwambia hiyo ni ndoto na haitowezekana.
Ni kitu gani uliambiwa hutoweza kukifanya na sasa unakifanya freshi tu?
.
20230814_221237.jpg
 
Yeah, this album is dedicated
To all the teachers that told me I'd never amount to nothin'
To all the people that lived above the buildings that I was hustlin' in front of
Called the police on me when I was just tryin' to make some money to feed my daughter (it's all good)
And all the niggas in the struggle
You know what I'm sayin'? It's all good, baby baby
 
Mimi mama yangu mkubwa aliniambia sitokuja kuolewa ntaishia kupata mimba na kurudi kwa bibi yangu.... akaniitia na wafanyakazi wenzie (workmate) siku ya mahari ya mwanae wa kwanza nakuanza kunisema kua mwanae amepata mwanaume mwenye hela zake (ni kweli mkwewe uyo alikua akifanya kazi mwadui 2008 (nlikua form 3)...matokeo yake mwanaume alikuja kumterekeza ndani (baada yakuishi miaka 3)

Anyway leo nmejisikia tu kutoa ya moyoni

Nmejifunza nikiishi na mtu asiye damu yangu nisimnyime chakula wala kumsemesha maneno yakukatisha tamaa haijalishi amenikwaza vipi
 
Yeah, this album is dedicated
To all the teachers that told me I'd never amount to nothin'
To all the people that lived above the buildings that I was hustlin' in front of
Called the police on me when I was just tryin' to make some money to feed my daughter (it's all good)
And all the niggas in the struggle
You know what I'm sayin'? It's all good, baby baby
dah! Kuna nyimbo ukisikiliza unapata reflection na hisia kali sana! Respect B.I.G
 
Niliambiwa siwezi kuwa hivi nilivo leo
Kauli kama hizo zilinikatisha sana tamaa
Maana aliyesema nilimtegemea sana tena alitamka mbele ya wazazi Wangu.
Ila Leo namshukru Mungu na yeye pia Kwa kauli nzuri kama Ile ya ujenzi.
Wazazi msidharau sana watoto wa wengine na kuona watoto wenu ni Bora kuliko wa wengine mtadharirika.
Na Bado sijamaliza Kikubwa uzima.
Bado sijamaliza.
Glory to The most High Alone.
The Supreme Being.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom