Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
1. Makampuni mengi makubwa ikiwemo TBL wameweka wazi kwamba mwenendo wa biashara si mzuri na hawa ni wazalishaji wa ndani ya nchi ambao pia kwa asilimia kubwa wanatumia malighafi na nguvukazi za ndani kwa maana ya rasilimali watu. Kwa mantiki hiyo makampuni ya ndani yanaposhuka kimauzo ni dalili za mwanzo za kushuka kwa pato la ndani ya nchi (Gross Domestic Product)
2. Taasisi za kifedha zimekuwa katika reconciliation tata na wateja wao ambapo katika taasisi nyingi za kifedha wakopaji hawarejeshi kama inavyotakiwa kwa maana excuse zimekuwa nyingi. Aidha wanachelewesha au kutolipa kabisa hivyo huishia kufilisiwa mali zao ama dhamana zao kuuzwa. Licha ya ukweli kwamba taarifa za kibenki ni siri kubwa isiyotakiwa kuenezwa nje lakini habari mbalimbali kutoka kwa wadau wa mabenki zinabainisha hivyo.
3. Udumavu wa thamani ya shilingi dhidi ya dola. Ni wazi kwamba Tanzania inanunua sana kutoka nje kuliko inavyouza hivyo si sawa kwamba shilingi itapambana na dola katika uthabiti wake hususani katika biashara ya kimataifa. Lakini jambo moja linaloashiria ukakasi katika mwenendo wa uchumi wetu ni kwamba bado shilingi nyingi hununua bidhaa kidogo huku bidhaa nyingine zikiadimika kabisa ikiwemo sukari.
Pamoja na hayo, kwa miezi mitatu mfululizo serikali imekuwa ikitoa taarifa kuhusiana na ukusanyaji mapato ambapo kiwango cha ukusanyaji mapato kimekuwa kimekuwa na ni ishara nzuri ya maendeleo. Jambo linalinipa wasiwasi ni kwamba, je ni wakati wa serikali kutajirika na wananchi kuwa masikini au kuna kitu gani kinaendelea nyuma ya uchumi wa Tanzania kiasi cha wananchi kuanza kulalamikia ugumu wa maisha?