Uchaguzi 2020 Ni kipi kinachokwamisha mdahalo kwa Wagombea mwaka 2020?

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
819
789
Wakuu, heshima kwenu.

Kuna baadhi ya nchi nimeona wagombea wanapokuwa wanawania nafasi ya cheo kikubwa kama uraisi, huwa wanapewa nafasi ya kufanya mdahalo. Mdahalo kwa wagombea unazo faida nyingi ikiwa ni pamoja na;

1. Kupima maono ya mgombea mmoja mmoja katika kutetea hoja yoyote ile iwe mbaya au nzuri kulingana na ilani ya chama chake kama mwongozo wa yale anayopanga/aliyopanga kuyatekeleza katika kipindi cha uongozi wake.

2. Kwa wingi wao, mdahalo ni chachu kupima ni nani hasa anaweza kutetea hoja za ilani yake kulingana na matakwa ya wapiga kura wake. Kujibu na kutengua maswali kunaweza kudhihirisha umahiri wake.

3. Kumpa changamoto ya kuboresha namna ambavyo inabidi aendeshe kampeni zake au kuhariri ilani yake endapo tu itaonekana kupingwa ama kukosolewa na idadi kubwa ya watu.

4. Mdahalo ni burudani kwa wapiga kura kuona ni nani anaweza ku-defend chama chake na ilani yake. Lakini pia kuna watu huwa wana-panic kama hivi juzi kati niliona kiongozi fulani hivi wa nchi kubwa ali-panic kwenye mdahalo nadhani ni kwa sababu ya maswali ambayo hayakuwa rafiki kwake au kwa mtazamo wa mrengo wake. Sitaki sana kuongelea huko maana tupo Tanzania.

5. Mdahalo ni kipimo cha kupima ni nani anayo influence kubwa kwa wananchi kuliko mwenzake kwa namna ambavyo atakuwa mzuri kujenga hoja na kujibu hoja ziwe za kejeli au serious.

Naomba kufahamu ni kipi hasa kinachokwamisha mdahalo kwa wagombea hapa Tanzania kuelekea uchaguzi Mkuu 2020? Je, ni kwasababu tuna vyama vingi kiasi cha kushindwa tuweke mgombea huyu au yule wafanye mdahalo? Au katiba yetu ndiyo haitaki/hairuhusu mdahalo kwa wagombea?

Tume ya uchaguzi tunaomba mfanye mchakato hata kuwepo na debate kati ya Mh. Rungwe na Mbatia tu endapo watakuwa hiari. Kama hiyo haitoshi, tuwachukue wagombea wawili wanaochuana vikali kwa sasa ili waje mbele ya umma kuonesha umwamba wao.

Am out...
 
Magufuli Mweupe sana kichwani hamna kitu. Hata PHD yake ya magumashi, NDIO MAANA HAWEZI KUONGEA HATA SENTENSI MOJA KWA KIINGEREZA.

Anajua kutumbua watumishi.

Sidhani kama umeandika ukweli maana ni mara nyingi huwa namwona Dkt akizungumza Kiingereza na hata kama tatizo ni Kiingereza, mdahalo unaweza kufanyika hata kwa lugha yetu ya Taifa (Kiswahili).
 
Magufuli Mweupe sana kichwani hamna kitu. Hata PHD yake ya magumashi, NDIO MAANA HAWEZI KUONGEA HATA SENTENSI MOJA KWA KIINGEREZA.

Anajua kutumbua watumishi.

Kwani mdahalo ni lazima uwe kwa kingereza? In fact Magufuli anaweza sema kuwa mdahalo lazima uwe kwa lugha ya Taifa ambayo inaeleweka vizuri na wapiga kura walio wengi!

Nakumbuka ni mara moja tu enzi ya marehemu Mkapa kama mgombea ndio ccm walikubali kushiriki mdahalo na walifanya hivyo kwa kuona wagombea wengine walikuwa watupu!!! Toka wakati huo ikawa ndio mwisho, wakati wa Mkwere walikacha mdahalo kwa vile nae alikuwa wasiwasi na hivi sasa tena sidhani kama wana ujasiri wa kumuweka Jiwe ulingoni apambane na Majabari!
 
Kwani mdahalo ni lazima uwe kwa kingereza? In fact Magufuli anaweza sema kuwa mdahalo lazima uwe kwa lugha ya Taifa ambayo inaeleweka vizuri na wapiga kura walio wengi!!

Hakika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom