Ni kipi chakula bora cha mbwa?

Ni kipi chakula bora cha mbwa?

Malapulapu ni nini wakuu mbona siyajui?

Au ndio sisi tunaita mawashiwashi yani yale mapafu na koromeo la ng'ombe?
 
Katika pitapita yangu na kutafuta majibu kama wewe nilikutana na hii link naona majibu yanapatikana kwa huyu jamaa kangámua vizuri sana.

MLO KAMILI WA MBWA UNATAKIWA KUWA NA VITU GANI?
★ Utangulizi
Lishe/chakula/mlo kamili kwa mbwa ni muhimu sana kwani humpa mbwa afya nzuri na pia huwakinga mbwa na mashambulizi mbalimbali ya magonjwa na hivyo kuwafanya wavutie muda wote
Kwa sasa vyakula vingi vya mbwa hupatikana madukani kutoka viwandani maana vimefanyiwa utafiti na kuzingatia afya ya mlaji ambaye ni mbwa na wanasayansi wameenda mbali zaidi wameweza kutengeneza chakula kutegemea aina ya breed ya mbwa
Lakini hayo yote hayakuzuii wewe mmliki wa mbwa kujitengenezea chakula mwenyewe ambacho kitakuwa kimekidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa mbwa ili kuepuka gharama ya chakula kwa namna moja ama nyingine kama nitakavyoelezea hapa chini
★ Umuhimu wa maji kwa mbwa
+ Vyakula vyote hata vile ambavyo hukaushwa na hewa maalamu kiwandani huwa na kiwango kidogo cha maji, ingawa mbwa anaweza jipatia maji kwa njia ya kunywa lakni kiwango kingine cha maji kinatokana na chakula
+ Mbwa anaweza kukaa muda mwingi bila kula chakula ( Hunger tolerance) lakni hawezi kukaa muda mrefu bila kunywa maji kwa maana hiyo mbwa asipokula chakula hutumia mafuta na baadhi ya nyama za mwili kama mbadala wa kupata nishati ya nguvu lakni akipoteza moja ya kumi ya maji yake mwilini mbwa hupoteza maisha
+ Bila maji ya kutosha mbwa hatoweza kumeng'enya chakula chake na hata kama akifanikiwa kwa hilo chakula hakitoweza kunyonywa vizuri katika mfumo wa chakula hivyo anahitaji maji muda wote na unywaji wa maji hutegemea na mazingira na wingi wa chakula
★ Sifa za mlo kamili wa mbwa
+ Chakula cha mbwa kinatakiwa kuwa na ladha na harufu ya kuvutia
+ Chakula kikidhi kiwango cha nguvu (wanga) kinachohitajiwa na mbwa
+ Chakula kiwe na kiwango cha protini cha kutosha kuwezesha ukuaji wa mbwa na kumkinga na magonjwa
+ Chakula kiwe na kiwango cha madini na vitamini cha kutosha
Zingatia: Mbwa ni jamii ya wanyama wanaokula nyama (carnivores) lakni tukija katika suala la mchanganyo wa chakula ulio kamili ni lazma uwe na protini, wanga, vitamini na madini na hata mbwa mwitu wanapowinda mbugani mara nyingi wanawinda jamii ya wanyama wanaokula majani na wakifajikisha kumuua hula kitu ukijumuisha matumbo ambayo huwa na majani yaliyomeng'enywa na mifupa yote hivyo kuwawezesha kupata madini na vitamini kwa njia hiyo hivyo basi kwa mbwa wanaofungiwa ndani ni lazma wapate mlo kamili kama nitakavyoelezea hapa chini
★ Vyakula vinavyotakiwa na mbwa na jinsi ya kuandaa vyakula hivyo
a) Nyama
Nyama ndio chanzo kikubwa cha protini kwa mbwa na katika mchanganyo inatakiwa kuwa zaidi ya 50%. Nyama hii yafaa ichemshwe kwanza ingawa mbwa wanapendelea nyama mbichi lakni kwa hili lazma ichemshwe na baada ya hapo ndio inatakiwa kuchanganywa na vyakula vingine
Kama nyama ina mifupa ni vyema mifupa ikaondolewa hasahasa kama nyama ni ya mbuzi/kondoo au kuku maana mifupa yao huwa ni midogo na hivyo inaweza kuleta shida katika mfumo wa chakula wa mbwa baada ya kuondolewa mifupa inatakiwa kuchemshwa pekee hadi pale itakapotoa supu ambayo itatumiwa kuchanganywa na vyakula vingine
b) Maziwa na Mayai
Maziwa na mayai hutumiwa kama mbadala wa nyama pale nyama inapokosekana hapa unatakiwa kuchukua maziwa kiasi cha lita 1.8 yachemshe yaache yapoe kisha changaya na mayai mawili yaliochemshwa vizuri then malizia kwa kuchanganya na vyakula vingine
c) Wali
Wali hutumika kama chanzo cha wanga na mchele unaotakiwa hapa ni ule unpolished (mchele mchafu) maana huwa na virutubisho vingi zaidi tofouti na ule Polished (mchele safi) na unaadaliwa kwa kuchemsha na maji kutengeneza bokoboko ambalo huchanganywa na vyakula vingine
d) Unga wa ngano
Unga wa ngano hutumika kama mbadala wa mchele endapo utakosekana hapa unatakiwa kuuchanganya kutengeneza uji mzito ambao utatumiwa kuukaanga kutengeneza chapati au pancakes ambazo utazikatakata na kuchanganya na vyakula vingine
e) Uji
Uji pia hutumika kama mbadala wa mchele na uji unatakiwa hapa ni ule ambao umetengenezwa na unga wa mahindi ambao haujakobolewa unauacha upoe kisha changanya na vyakula vingine. Mbwa wanaupenda sana uji huu.
f) Mbogamboga
Ingawa mbwa hawapendi mbogamboga lakni ni muhimu kuwemo kwenye mchanganyo maana ndio chanzo cha vitamini na madini mbalimbali mboga kama sukumawiki, chinese ni nzuri lakni ukikosa hizo unaweza chemsha carrot au beetroots na ukachanganya kwenye vyakula vingine na ikumbukwe kuwa kiwango cha mboga kitengeneze 1% ya mchanganyo wote.
g) Matunda
Mbwa pia Anaitaji Matunda Kama ilivyo kwa wanyama wengine, matunda umwongezea vitamin na kuimarisha mwili, hapa matunda mbalimbali yanaweza kutumika kulingana na ulivyomzoelesha toka mwanzo, Mbwa wanapenda Banana, parachichi ,tikitimaji na matunda mengine kadiri ya utakavyowazoesha.
★ Vitu vya kuzingatia katika ulishaji wa mbwa
* Kwa kawaida tumbo la mbwa ni kubwa kulinganisha na viungo vingine vya mfumo wa chakula hivyo anatakiwa kula ambacho kitaweza kukaa mwilini kwa muda mrefu na kwa kawaida mbwa anayakiwa kula mara moja kwa siku ingawa watu wengine huwalisha mara mbili ambapo hutenga chakula kama chakula cha kawaida (light diet) au chakula cha kutosha (heavy diet)
* wali kidogo na mbogamboga huandaliwa kivyake baada ya hapo huchanganywa na supu na nyama kidogo na hii tunaita light diet na chakula kamili huwa na nyama,mbogamboga,wali au chapatti na vyote hivi huchanganywa na supu ya mifupa
* Na mbwa aina ya chakula kutegemea na majukumu yake yako muda gani ' Kama mbwa analinda usiku basi asubuhi anatakiwa kula heavy diet na jioni masaa machache kabla ya kuingia lindoni anatakiwa kula light diet na kama mbwa anaingia lindoni mchana basi jioni anatakiwa kula heavy diet na asubuhi kabla ya kuingia lindoni ale light diet
* Chakula cha mbwa kinatakiwa kuandaliwa muda kidogo kabla ya mbwa kula na kama chakula kikibakizwa na mbwa hatakiwi kulazimishwa kula na chakula hicho kiondolewe ndani ya dakika 10-15
* Vyombo vya chakula na maji vinatakiwa kuwa safi na salama muda wote na hakikisha maji hayaishi ndani ya chombo cha maji na kinatakiwa kuwa karibu na bakuli la chakula muda wote
* Mbwa wasipewe vyakula vya sukari au chumvi maana vyakula hivyo huwapunguzia umri wa kuishi na pia huwasababishia magonjwa mbalimbali ya ngozi
* Muda na mahali pa kulia chakula uwe/pawe sehemu moja hakuna haja ya kubadili ratiba ya chakula kama ni asubuhi ya saa 11 na jioni ya saa2 iwe hivyo muda wote hakuna haja ya kubadili ratiba ya chakula
* Kwa siku mbwa anatakiwa kuwa gm 400 za chakula na mara moja unaruhusiwa kumpa mbwa maji yaliyochanganywa na glucose na iwe kila siku.
©Championsveterinarycenter
Wadau natafuta mtu anaeuza au animegee kidogo kafomula kakutengeneza chakula cha mbwa. super dog ya supermarket kama inazingia hivi

nami niulize ukiweka order kwa aina fulani ya mabaki ya chakula kutoka hotel kubwa ambazo kuku kubaki na vipande vikatupwa ni kawaida inaweza kuwa sio mzuri kwa ajili ya chakula cha mbwa?
Ni vema ukayachemsha kwanza ukiweza kuepuka mbwa wako kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo minyoo.
 
Championsveterinarycenter

Asante,maelezo mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dagaa kiasi zichemshe kwenye maji
Kisha weka chenga za mchele ulizoloweka nusu saa kiasi cha kipimo utakacho maana kilo moja chenga mbwa 3 wanakula na kusazaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom