Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,872
Kuna watu ambao wanaonekana kushangazwa au hata kukwazwa na jinsi Magufuli anazungumza au anavyosema mambo; wengine wanakwazwa kwa jinsi alivyo 'straight shooter' asiyemung'unya maneno; na wakati mwingine kuonekana kauli zake zinamleta matatizo. Baadhi yetu ambao tumefuatilia utendaji kazi wake miaka hii ishirini hatujaona tofauti ya Magufuli huyu na yule. Ni mtu yule yule.
Wengine wanataka awe tofauti; awe tofauti na Magufuli yule. Wanasahau kuwa alichaguliwa na mamilioni ya Watanzania kwa sababu hakubadilika; alikuwa ni yule yule. Mitazamo yake inaeleweka, utendaji wake unaeleweka na namna gani wakati mwingine kwa kauli zake anaweza kujiletea matatizo inaeleweka. Ni sawasawa na Trump huko Marekani. Leo watu wanamuona Trump alivyo, jinsi anavyozungumza na kauli zake kwa mtu mwingine hakupaswa hata kufikiriwa kuwa Rais lakini mamilioni ya Wamarekani wanaamini kuwa Taifa lao linamhitaji mtu kama yeye; mtu asiyejali sana siasa na kufurahisha vikundi vidogovidogo au kuwafurahisha wasomi kwa maneno matamu, yaliyopangwa vizuri na kusema vitu ambavyo vitamfanya aonekane "more presidential".
Wamarekani wameshawahi kuwa na wanasiasa wazuri, wenye maneno mazuri na wenye kupima kila herufi ya kila neno na matokeo yake karibu wote - kwa upande wa Republicans - wametupwa pembeni; anaenda kupewa rungu kichaa... Magufuli hivyo hivyo.. nilisema mwanzoni kabisa kuwa Magufuli ni kama kichaa kupewa rungu; lakini kichaa chake kizuri. Hajali sana hisia za kisiasa za watu au kudekeza kwa maneno ya kupoza na kufurahisha genge.
Tulishawahi kuwa na mtu anayezungumza kwa kufurahisha genge, asiyetaka kuudhi watu na ambaye alijaribu kujenga urafiki na kila mtu ili asiwe na adui. Matokeo yake Watanzania tukachoka tukasema imetosha...
Itabidi watu wazoee tu kwa miaka hii mitano kwani Magufuli huyu ni yule yule na labda sasa ana uthubutu zaidi wa kusema na kufanya mengi. Kama kuna vikwazo na anaonekana kuvuruga watu.. tutumie Bunge au Mahakama kuhoji maamuzi yake lakini binafsi naona Magufuli huyu hana tatizo na wanaokwazika wanakwazika kana kwamba walikuwa hawamjui alivyo...
#MtazoeaTu