Ni kikao cha aina gani usichopenda kukaa?

karume kenge

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
568
421
Habar wadau

Binafsi kikao cha kuitisha ndugu au wazazi wa pande mbili labda umemfumania mkeo ni kikao nisichokipenda maisha yangu yote kwa sababu huwa kuna lawama za kiwango cha juu kama sio kwa mke basi kwa mme kama sio mme ndugu wa mke kama sio mke ndugu wa mke.

Nishakaa kikao hicho na kusimamia ukweli mpaka leo huwa na lawama ya kuachanisha mke na mume kwa sababu ya ukweli.
 
Kikao cha kusutwa hicho noma
 
Sipendi vikao vya wanasiasa na mikutano yao. Kila siku mada ni zilezile na hazitekelezeki...sipendi sipendi
 
Inakuwaje mwanaume uitishe kikao cha ndoa? (ugomvi na mkeo) kama mke kafanya kosa kaa nae kitako muelezee hali halisi. Hakuna familia isiokuwa na makosano, wengi wa wana familia hutoa machungu yao kwenye ndoa zao kwenye vikao vya ndoa ya wenzao.

Ndukiiiii
 
Kuna kikao cha kukabidhiwa mke faster faster ile mnaita ndoa ya mkeka! Nilishachoropoka kimoja huko Rufiji sirudii tena!
 
Back
Top Bottom