hapa Iringa palikuwa hapatoshi!
ila Nilikuwa angalizo moja tu!
kwa kweli niwapongeze wapambanaji kwa kazi nzuri wanayoifanya! ILA!!!
hotuba nyingi na muda mwingi wanautumia kuwaambia WaTz juu ya sera mbovu za CCM na serikali yake, udhaifu kwenye usimamizi wa rasilimali za TaTz, hii inawachochea vijana na wapenda mabadiliko kuwa na hasira na serikali iliyo madarakani! lakini hii sioni kama ni sawa kutumia masaa 2 kusema juu ya ufisadi H/W, sijui Twiga wameuzwa, sijui Maige amenunua nyumba ya bil 1.4. halafu tunatumia dk 25 kusema juu ya sera za CDM na manifesto! yake.
Sikusudii kuwafundisha viongozi wangu siasa wala kuhutubu, lakini nionavyo mm hii si sahihi, tutumie muda mwingi kusema juu ya sera za CDM ili waTz waijue CDM, waelewe sera za majimbo zinafanyaje kazi na wazizoee!! MMwanakijiji aliwahi kushauri hili pia lakini naona bado hakuna mabadiliko. Kusema juu ya kushindwa kwa CCM ni sahihi kabs lkn iwe inatokea wakati wa kuelezea mifano ili wTZ wajue ni nini sera mbadala za kuwatoa hapa tulipo.
Tunapowaambia tu twiga, EPA, Maige, Madini.. halafu tunaambiwa asanteni kwa kunisikiliza Hell no!!! no kwa chama Makini na viongozi makini kama wa CDM!!
Please make use of this kama mmtaona inafaa!!