Katika Injili ya Bwana Yesu Kristo tunaweza kujifunza matumizi ya Namba 3. Hii ni namba yenye kuonyesha kusudio la Mungu linalokwenda kutimilika kama ambavyo lilivyokusudiwa.
Mathalani, tukio zima la kusulubiwa kwa Bwana Yesu, hilo lilikuwa ni kusudio la Mungu mwenyewe. Nalo linapata kufikia utimilivu wake wote kupitia nambari 3
Kumbuka Petro alimkana Bwana Yesu mara 3 rejea Marko 14:66-72
Bwana Yesu aliomba mara 3 muda mfupi kabla ya kukamatwa na kwenda kusulubishwa, rejea Marko 14:32-41
Jina “YESU WA NAZARETH MFALME WA WAYAHUDI” Liliwekwa msalabani kwa lugha 3 rejea Yohana 19;19-20.
Bwana Yesu alikaa msalabani kwa masaa 3 kutoka saa 6 mpaka saa 9 mpaka pale alipokata roho rejea Mathayo 27:45
Kwa matukio yote hayo machache hii namba 3 inayojirudirudia kwa kusudi maalum.
Namba 3 hapa inatuonyesha kwamba tukio lote la kusulubiwa kwa Bwana Yesu ilikuwa kwa Makusudi ya Mungu juu ya wokovu wa wanadamu dhidi ya kifo , mauti, na kuzimu, na jukumuu hili kuu lipate kutimia Mungu kajidhirisha kwetu kwa ofisi ama hadhi kuu 3, yaani Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu