Wenaya
Member
- Feb 28, 2015
- 14
- 9
Matumizi ya Teknolojia yameshika kasi sana katika ulimwengu huu na imekuwa ni chanzo cha kutatua baadhi ya changamoto mbali mbali zikiwemo kubwa na ndongo ambazo kimsingi zimekuwa zikizisumbua jamii zetu. Kila sehemu katika Tanzania yetu kuna changamoto zake kutokana na idadi ya watu, miundombinu, rasilimali n.k Pia kuna vijana au watu ambao wana uwezo wa kuitumia teknolojia kuzipunguza kama si kuzimaliza changamoto hizi kwa kubuni vitu mbali mbali ambavyo vitarahisisha kazi.
Sasa basi naomba Uniandikie hapa kwenye hii thread ni changamoto gani inayoikabili sehemu uliyopo ambayo unafikiri inaweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya teknolojia au hata nje ya teknolojia, Naamini tupo wengi ambao pengine hatujui hizo changamoto ila kutokana na michango yenu ya kimawazo hapa wajuzi wa mambo wataumiza vichwa vyao kuja na njia mbadala za kupunguza changamoto hizo na tutakuwa tumeisaidia jamii yetu kimaendeleo na kuwatengenezea fursa za ajira wadogo zetu kwa maana uwepo wa teknolojia pia ni chanzo cha utengenezaji wa Ajira kwa jamii mfano uwepo wa MAX Malipo n.k
Itakuwa vyema ukiandika CHANGAMOTO hiyo pamoja na SEHEMU husika tuone ni sehemu gani inahitaji usaidizi wa haraka zaidi.
Kwa pamoja tutoe michango yetu ya kimawazo jamii yetu iepukane na usumbufu wa aina yoyote iwe Afya, au Sekta nyingine ambazo zinaweza kufanyiwa kazi.
Pia usisahau kupakua App hii ya SIKILIZA uweze kusikiliza Redio popote pale ulipo kwa urahisi zaidi.
Natanguliza Shukrani.
Jalilu Zaid.